Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Mbona sisi tumekwenda kuwasitiri wao?

Kwamba shetani hachukiwi na wote?

Bila shaka anachukia na wengi kama ilivyo sisi kwa sasa.

1.Kwenda kuwasitiri ni uamuzi wetu ata tusingekwenda hakuna adhabu ambayo tungepewa

2.SHETANI hajawai kuchukiwa na wote , watu kibao wanampenda kimaneno na kivitendo

Ata Israel anachukiwa na waarabu wengi lakini ameendelea sana kiuchumi na kijeshi kuliko hao wanaomchukia , nimekwambia chuki zinaongeza hasira kuwa mbunifu zaidi mpaka wanaokuchukia wakuheshimu, tulia tuli dawa itawaingia vizuri
 
Hadi sasa bado hakuna maelezo ya kitaalamu yenye kujitosheleza kuelezea kwanini Africa hatujaona athari za corona kama tulivyoona china na ulaya huko(sio takwimu,ni athari) ambako hospitali zilizidiwa wagonjwa na hadi sehemu za kuhifadhi maiti,tukaona china akijenga hadi hospitali ndani ya wiki kwa ajiri ya wagonjwa wa corona,hali ilikuwa wazi kwamba hakuko shwari huko kwa wenzetu hali mbaya.

Corona ilipoingia afrika wengi tuliona sasa waafrika tumekwisha maana kama hao wenzetu wenye huduma bora za afya ila imewapiga vile lazima hali itakuwa mbaya zaidi huku kwetu na wapo waliyotabiri kuwa tutaokota maiti barabarani,lakini hadi sasa hatujui kwanini hayo tuliyoyatizamia kutokea hayajatokea.

Nachokiona kwa Tz kuna watu wanaamini kuwa Tz hali itakuwa mbaya ila inafichwa kwa sababu hakuna takwimu za corona na wengine wao wanaona kama hali ingekuwa mbaya basi athari za corona tungeziona kabla ya hizo takwimu.
 
Watanzania bila kuondokana na hili jiwe linalotufanya tujikwae hatuendi popote. Mtu huyu hana upeo inajulikana wazi ndio maana anaishia hapa hapa hawezi hata kufanya diplomasia na mlevi Uhuru atawezaje na wengine wa Ulaya, Asia, etc
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Siyo siri tena zama zimebadilika na matukio yanakwenda kwa kasi sana. Taifa letu likipita katika kipindi kigumu ambapo kwa bahati mbaya kumezuka hata makundi katika jamii ambayo yamelenga kupiga makelele tu yakijaribu kulazimisha kuufanya uongo kuonekana kuwa ukweli au ukweli kuwa uongo. Mithili ya kujidanganya mchana kuwa ni usiku au usiku kuwa ni mchana.

Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi.

Ikumbukwe kuwa ukweli ni ukweli na uongo ni uongo na utabakia kuwa hivyo bila ya kujali nani kasema nini au nani atasema nini.

Ukweli mchungu hulka mpya hii haikuwahi kushuhudiwa katika awamu yoyote ya uongozi kabla ya awamu ya hii.

Hivi karibuni tumeondokewa na mzee wetu rais mstaafu mzee Mkapa (rip). Pamoja na sisi kushiriki sana katika shughuli zote za wenzetu, ni Burundi peke yake ndiyo walioweza kutuma ujumbe wao rasmi kuja kutuhani kwenye msiba huu mkubwa kutoka nyumbani kwao.

Si Malawi tulikokwenda kwenye kuapishwa kwa rais Chakwera. Si Zimbabwe tulikokwenda kumhani raisi wao Mugabe (rip). Si Afrika kusini tulikokwenda kumhani Mandela (rip) wala Winnie (rip). Wote hawa, hawakutuma wawakilishi wao rasmi tokea makwao kuja msibani sisi yalipotukuta.

Si Kenya tulikotuma ujumbe wetu mzito kabisa wakiwamo marais Kikwete na Mkapa (rip) kwa pamoja kuwahani kwenye msiba wa rais Moi (rip), kuwa walikuja kutuhani sisi yalipotusibu miezi michache tu baadaye.

Si Zambia, si Mozambique, si Rwanda, si Congo wala Uganda waliofika msibani.

Si nchi za Comesa, SADC, Ulaya, Marekani kaskazini wala kusini, Si Asia zikiwamo Uarabuni, Afrika wala Australia waliotukumbuka.

Hamkani si shwari tena bila ya kujali makelele yetu yote, kwa hakika hatuko vizuri. Kama waungwana tunapaswa kujiangalia. Vinginevyo makelele yetu mengi yanaweza kuwa ni kutokea kwenye madebe matupu yasiyoacha kuvuma.

Tukumbuke maneno matupu hayavunji mfupa.

Alipotutoka baba wa taifa (rip), Afrika yote hata dunia walikuwa hapa. Marais karibia wote, SADC, COMESA, ECOWAS, nk achilia mbali wawakilishi wazito wazito mabeberu walikuwa hapa kutuhani msiba ule.

Walikuwapo hapa hadi kina Madeline Albright waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Hiyo ndiyo Tanzania iliyokuwa ikisomeka vilivyo duniani kote chini ya rais Mkapa (rip).

Uzi huu kwa hakika tulipo upo, unatuhusu sana na hasa katika zama za leo:

Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Matatizo hayatanzuliwi kwa kuyakimbia, kujificha au kuyafumbia macho.

Kupafahamu wapi tulipojikwaa ni hatua njema katika kujipanga vizuri zaidi. Kujitenga au kuruhusu kutengwa kamwe hauwezi kuwa uchaguzi ulio bora.

Kujikwaa si kuanguka.

Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
Mkuu brazaj majirani wivu tu unawasumbua,si unajua tupo uchumi wa kati,hao wanatuonea gere hawajaja lakin mzee wetu tumempumzisha kwa amani nyumba yake ya milele
Mungu ambariki Mzazi aliyekulipia ada, hakulipa bure! Mungu akajibu kila ombi la moyo wake!

Tunajiona tuko sahihi sana, tukikosolewa tunakua Wakali kama nyigu mjamzito! Kejeli, vijembe, ulimbukeni, kujikweza na kujiona kuwa tuna kila kitu na hakuna wa kutubabaisha....! Tutakuja kuanguka vibaya tukose wa kutusaidia
Hivi status yetu ikoje kwa mataifa mengine ukiachana na Kenya?
Burundi pekee ndiye mwenzetu aliyebakia. Wa kufa na kuzikana.
Mkuu nakusoma na hasa kwa mistari kwa mstari kama ulivyoandika.

Subiri waje na vibwagizo zaidi na mapambio ya kujazia. Huwezi kuamini!

Heshima kwake aliyeandika hili:

View attachment 1525514

Natamani ingekuwa ni jinamizi, lakini kwa bahati mbaya ndiyo ukweli wenyewe.
dah!
nshajiuliza san hili'
JPM ni mtu wa kujali vitu na sio watu.
Muwe wazalendo basi. Au mmetumwa na mabeberu? Hii ni vita ya kiuchumi. Bro Magu chapa kazi. Usisikilize kelele za chura. Hongera sana kwa kulijengea taifa heshima
Umeongea vitu vya msingi

But points of correction katika msiba wa Mandela JK Alienda na alitoa speech
Mkuu hiyo ni point of addition (badala ya correction) zaidi sana ya kuwepo tu. Tulikuwapo tukapewa na heshima zaidi kutoa speech.

Hata kwenye msiba wa rais Moi (rip) zaidi sana ya kuwapo, tulipewa pia heshima kama hiyo ya kutoa speech.

Hii ni kama ilivyokuwa kwa Madeline Albright mwakilishi wa beberu kwenye msiba wa mwalimu (rip).
 
1.Kwenda kuwasitiri ni uamuzi wetu ata tusingekwenda hakuna adhabu ambayo tungepewa

2.SHETANI hajawai kuchukiwa na wote , watu kibao wanampenda kimaneno na kivitendo

Ata Israel anachukiwa na waarabu wengi lakini ameendelea sana kiuchumi na kijeshi kuliko hao wanaomchukia , nimekwambia chuki zinaongeza hasira kuwa mbunifu zaidi mpaka wanaokuchukia wakuheshimu, tulia tuli dawa itawaingia vizuri

1. Vyema umetambua kuwa kuna kususiwa na nchi zingine. Tambua pia kuwa hata kama na wewe ulimsusia mzee Mkapa, wengine hatukumsusia.

Tulikuwapo Uhuru, JKNIA na wengine hata Lupaso kwa dhati kabisa, achilia mbali ambao hawakuweza kuingia pale Uhuru.

Wewe ulikuwa pande ipi katika sehemu hizo 3?

Hiyo ndiyo Tanzania tunayoijua, tunayoitaka, tutakayoidai na kuipigania siku zote. Hiyo ndiyoTanzania ya Nyerere (rip), Mwinyi, Mkapa (rip) na Kikwette ambayo kila mpenda amani, haki, kweli, ustawi nk, kokote aliko anaitamani. Tanzania inayothamini watu, utu, uhuru na maisha yao. Tanzania ambayo ilikuwa inapewa uzito wake iliostahili kote duniani.

Tanzania iliyokuwa inatambua binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

Tanzania iliyokuwa na tofauti za wazi na ushetani.

2. Usilinganishe Tanzania na Israel kana kwamba Israel inakubaliana na ushetani na mkururo wa hayo yaliyotufikisha hapa.

Fahamuni kuwa hatudanganyiki na wala hamtatunyamazisha. Ukweli mnaujua ila mnajifanya hamnazo.

IMG_20200801_100446_674.jpg


Ushahidi wa kuwa kuna chuki au hasira uko wapi?

Hamtatutoa kwenye hoja za wazi hizi ambazo kila mtu mkiwamo nanyi wameza OmO mnaziona. Wala hatutakubali kuwa sehemu ya kujidanganya.
 
Kuna watanzania wapuuzi sana kama mtoa mada

Hakuna mtanzania mmoja mpuuzi kuliko wewe.

Wapuuzi wote kama wewe huwa tuna ka button kapya ka kuwapumzisha na upumbaav wao.

Huwa tuna wa address wote mmoja mmoja wanaotuandikia kabla ya kujiridhisha na upumbaav wao.

Kelele za vyura nyie hazijapata kuwa issue na wala hazitakuja kuwa issue.

Wenzio wengi tusio wajibu huwa wapo kwenye ka list kale muda mwingi kabla.

Kongole kwenu mods kwa ka function hako. Kwa hakika Mdumu milele!

Hamkufaulu kuwanyamazisha wengine kwa risasi sembuse wa kwenye keyboards?

Bye bye amigo don't even mind to write back.
 
Kwamba kujikombakomba kwa mataifa mengine ndiko kutatuweka pazuri!?

Hii nchi ni huru na ina misimamo yake tangu zamani. Tumeonyesha upendo kwa mataifa mengine pengine kuliko nchi yoyote.
Tumeshiriki ukombozi wa nchi zao dhidi ya ukoloni, tumewahifadhi wapigania uhuru wao hapa kwetu, tumesaidia kulinda amani, tumewapa misaada ya vyakula, kijeshi n.K, tumehani na kushiriki misiba ya viongozi wao kwa heshima kubwa.

KAma yote hayo hawayaoni na mnaendelea kutaka tuwanyenyekee basi tambueni ya kuwa IMETOSHA.

Ni wakati sasa wa Tz kujali mambo yake na maslahi ya watu wake baaaas.

Uliyoyaandika hapa:

Tumeshiriki ukombozi wa nchi zao dhidi ya ukoloni, tumewahifadhi wapigania uhuru wao hapa kwetu, tumesaidia kulinda amani, tumewapa misaada ya vyakula, kijeshi n.K, tumehani na kushiriki misiba ya viongozi wao kwa heshima kubwa.

Mema kabisa si kujikomba komba, yalifanywa na awamu ya 1 - 4.

Huko Afrika ilikuwa moja na binadamu wote walikuwa ndugu zetu. Huko busara, haki, na vyote vya namna hiyo vili tamalaki.

Zama hizo tuliheshimiwa vilivyo. Zama hizo hazipo tena na hapa ndipo tulipo. Hayupo wa kumsingizia kwa hilo.

Ndipo chimbuko la bandiko lilipo. Hatuna haja ya kujidanganya. Mchawi ni sisi wenyewe. Kujidanganya hakutatusaidia.
 
Mkuu kama taifa tunatatizo kubwa,lakini badala ya kuangalia tumeanguka wapi ili tubadirishe strategy na kusonga mbele,kazi yetu ni kunyoshea watu vidole na kuwalaum wengine hasa Kenya.
Tumeanguka wapi?

Tubadilishe strategy zipi?

Nani ana walaumu wa Kenya na kwasababu gani Wakenya wanalaumiwa?
 
Umeraise hoja mwenyewe unashindwa kuzijibu,maana yake hata unachokiongea hukijui bali una payuka na kuropoka.

Ndio maana ukajiita Sijijui
Mkuu ulitaka nijitetee? Kama wewe huwezi kuona kwa direction tuliyochukua kudeal na covid_19 hasa kitendo Cha kuficha data hakikuwa sahihi,why nipoteze muda wangu kuargue na wewe?
 
Mkuu ulitaka nijitetee? Kama wewe huwezi kuona kwa direction tuliyochukua kudeal na covid_19 hasa kitendo Cha kuficha data hakikuwa sahihi,why nipoteze muda wangu kuargue na wewe?
Data zipi mbona huombi data za malaria,Ukimwi,Homa ya Ini magonjwa ambayo yanaua sana kuliko Corona,why unataka data za Corona?
 
Data zipi mbona huombi data za malaria,Ukimwi,Homa ya Ini magonjwa ambayo yanaua sana kuliko Corona,why unataka data za Corona?
Mkuu corona was declared as global pandemic.upo category tofauti na hayo magonjwa uliyotaja
 
Mkuu corona was declared as global pandemic.upo category tofauti na hayo magonjwa uliyotaja
Sawa imekuwa declared sijakataa,sasa kwa nini huombi data za magonjwa kama Malaria,Ukimwi,Homa ya ini nk ambayo yanaua watu wengi zaidi ya Corona?

Au issue ni kuwa declared na si impact (vifo) yake katika MAZINGIRA HAYA YA KWETU.
 
Wewe mbulula kweli, yaani unazurura tumitaani huvai hata barakoa alafu unatufokea kovid itatuua, mbona wewe hufi? Halafu Sasa unalalamika Nini wakati wemwenyewe umesema Tz Kuna korona, Sasa Ukitaka waje waambukizwe? Shwain kabisa.
 
Sawa imekuwa declared sijakataa,sasa kwa nini huombi data za magonjwa kama Malaria,Ukimwi,Homa ya ini nk ambayo yanaua watu wengi zaidi ya Corona?

Au issue ni kuwa declared na si impact (vifo) yake katika MAZINGIRA HAYA YA KWETU.
Ndio maana mkuu nimetoka kueleza kuwa huko kwa wenzetu athari za corona tuliziona haikuhitaji takwimu kuweza kujua kuwa hali ni mbaya.
 
Sawa imekuwa declared sijakataa,sasa kwa nini huombi data za magonjwa kama Malaria,Ukimwi,Homa ya ini nk ambayo yanaua watu wengi zaidi ya Corona?

Au issue ni kuwa declared na si impact (vifo) yake katika MAZINGIRA HAYA YA KWETU.
Mkuu acha umimi hata Kama wewe ni mama wa nyumbani,hivi Kama ugonjwa ulianzia Wuhan china na kusambaa dunia nzima unashindwaje this time around kutokea kwa watanzania ambao ni sugu kwa kila magonjwa na kwenda kuua watu wanaojari maisha yao huko duniani? Au wewe unadhani Tanzania ni kisiwa?kwamba hakifikiwi na mtu mwingine yeyote yule au watu wake hawatembei?
 
Kwani ni kwenye msiba huo tu? Pia umesahau kuwa sisi Corona haipo. Wataogopa vipi kuja kusiko na Corona hata kama kwao ipo?

Kwenye Kuukimbia ukweli, mambo iko huku:

"Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi."

Hakutatusaidia.
Nimekwambia kuwa hata mazishi ya Nkurunzinza hao uliowataja hawakwenda, je pia huko kuna tatizo gani pia?

Mimi naona unakuza mambo tu, kwasasa marais wa nchi zilizojifungia hakuna anayesafiri. Nina uhakika bila corona kuwepo wote wangekuja may be Kenyatta tu ndiyo angekosekana
 
Mkuu acha umimi hata Kama wewe ni mama wa nyumbani,hivi Kama ugonjwa ulianzia Wuhan china na kusambaa dunia nzima unashindwaje this time around kutokea kwa watanzania ambao ni sugu kwa kila magonjwa na kwenda kuua watu wanaojari maisha yao huko duniani? Au wewe unadhani Tanzania ni kisiwa?kwamba hakifikiwi na mtu mwingine yeyote yule au watu wake hawatembei?
Kwani wewe MAMA WA NYUMBANI?

Kweli umeanzia WUHAN,je impact ya WUHAN na Tanzania sawa au wewe unafikiria ktk MAZINGIRA YA WUHAN na si Tanzania?

Au wewe ni MAMA WA KICHINA KUTOKA WUHAN ndio maana una hofu.Tanzani si kisiwa na ndio maana imechukua tahadhari kuanzia partial lockdown na sasa tumefungua kama mataifa (UK,France,Italy na Spain) mengine,wametoa ushauri wa kiafya (kunawa na sanitizer na kuvaa barakoa),wakati tukiwa kwenye shughuli zetu.

Tanzania imeamua kuishi na Corona kama inavyo ishi na Malaria au WEWE ULITAKA TANZANIA IFANYE NINI?
 
Nimekwambia kuwa hata mazishi ya Nkurunzinza hao uliowataja hawakwenda, je pia huko kuna tatizo gani pia?

Mimi naona unakuza mambo tu, kwasasa marais wa nchi zilizojifungia hakuna anayesafiri. Nina uhakika bila corona kuwepo wote wangekuja may be Kenyatta tu ndiyo angekosekana

Burundi ya Nkurunziza ilikuwa na msimamo kama wetu kuhusiana na Corona.

Nkurunziza alisema hadharani kuwa Corona ilikuwa ni kaupepo tu na Yesu aliipenda mno Burundi kuwa Corona isingefika huko. Msimamo sawa sawa na wa Tanzania.

Mbele zaidi alikwenda Nkurunziza, aliwatimua WHO Burundi.

Baada ya Nkurunziza, rais wao mpya kachukua msimamo tofauti wa kuchukua hatua thabiti za kupambana na Corona.

Tanzania tulikwenda kwenye msiba wa Nkurunziza kama wao walivyo kuja kwetu. Ndege wa kufanana huruka pamoja.

Hakuna zaidi yetu aliyekwenda kwa Nkurunziza kwa sababu hakuna aliyejuwa hali halisi ya ugonjwa huko. Kwa nini kwenda kujiweka hatarini?

Sisi na Burundi kabla ya Ndayishimye wote maji ga nyanja. Kutembeleana sisi kwa sisi na kupigwa pande na jamii nyingine pamoja.

Hakuna jipya hapo sababu zilizofanya wengine kutokwenda Burundi ni hizo hizo kuhusiana na Corona kwao na kwetu kufanana machoni pa jumuiya ya kimataifa.

Kuna tofauti ya kutokujua, kutokuelewa au kujifanya hamnazo.

Nina mengi kidogo ya kufanya - kuchapa kazi kuliko kupoteza muda na mmeza OmO au aliyejitoa ufahamu kufanya mchana ni usiku au usiku ni mchana.

Mwendelezo wa kujidanganya ni kipaji si kila mtu anacho.
 
Back
Top Bottom