Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,803
35,793
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Siyo siri tena zama zimebadilika na matukio yanakwenda kwa kasi sana. Taifa letu likipita katika kipindi kigumu ambapo kwa bahati mbaya kumezuka hata makundi katika jamii ambayo yamelenga kupiga makelele tu yakijaribu kulazimisha kuufanya uongo kuonekana kuwa ukweli au ukweli kuwa uongo. Mithili ya kujidanganya mchana kuwa ni usiku au usiku kuwa ni mchana.

Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi.

Ikumbukwe kuwa ukweli ni ukweli na uongo ni uongo na utabakia kuwa hivyo bila ya kujali nani kasema nini au nani atasema nini.

Ukweli mchungu hulka mpya hii haikuwahi kushuhudiwa katika awamu yoyote ya uongozi kabla ya awamu ya hii.

Hivi karibuni tumeondokewa na mzee wetu rais mstaafu mzee Mkapa (rip). Pamoja na sisi kushiriki sana katika shughuli zote za wenzetu, ni Burundi peke yake ndiyo walioweza kutuma ujumbe wao rasmi kuja kutuhani kwenye msiba huu mkubwa kutoka nyumbani kwao.

Si Malawi tulikokwenda kwenye kuapishwa kwa rais Chakwera. Si Zimbabwe tulikokwenda kumhani raisi wao Mugabe (rip). Si Afrika kusini tulikokwenda kumhani Mandela (rip) wala Winnie (rip). Wote hawa, hawakutuma wawakilishi wao rasmi tokea makwao kuja msibani sisi yalipotukuta.

Si Kenya tulikotuma ujumbe wetu mzito kabisa wakiwamo marais Kikwete na Mkapa (rip) kwa pamoja kuwahani kwenye msiba wa rais Moi (rip), kuwa walikuja kutuhani sisi yalipotusibu miezi michache tu baadaye.

Si Zambia, si Mozambique, si Rwanda, si Congo wala Uganda waliofika msibani.

Si nchi za Comesa, SADC, Ulaya, Marekani kaskazini wala kusini, Si Asia zikiwamo Uarabuni, Afrika wala Australia waliotukumbuka.

Hamkani si shwari tena bila ya kujali makelele yetu yote, kwa hakika hatuko vizuri. Kama waungwana tunapaswa kujiangalia. Vinginevyo makelele yetu mengi yanaweza kuwa ni kutokea kwenye madebe matupu yasiyoacha kuvuma.

Tukumbuke maneno matupu hayavunji mfupa.

Alipotutoka baba wa taifa (rip), Afrika yote hata dunia walikuwa hapa. Marais karibia wote, SADC, COMESA, ECOWAS, nk achilia mbali wawakilishi wazito wazito wa mabeberu walikuwa hapa kutuhani msiba ule.

Walikuwapo hapa hadi kina Madeline Albright waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Hiyo ndiyo Tanzania iliyokuwa ikisomeka vilivyo duniani kote chini ya rais Mkapa (rip).

Uzi huu kwa hakika tulipo upo, unatuhusu sana na hasa katika zama za leo:

Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Matatizo hayatanzuliwi kwa kuyakimbia, kujificha au kuyafumbia macho.

Kupafahamu wapi tulipojikwaa ni hatua njema katika kujipanga vizuri zaidi. Kujitenga au kuruhusu kutengwa kamwe hauwezi kuwa uchaguzi ulio bora.

Kujikwaa si kuanguka.

Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Matatizo hayatanzuliwi kwa kuyakimbia, kujificha au kuyafumbia macho.

Kupafahamu wapi tulipojikwaa ni hatua njema katika kujipanga vizuri zaidi. Kujitenga au kuruhusu kutengwa kamwe hauwezi kuwa uchaguzi ulio bora.

Kujikwaa si kuanguka.
Mungu ambariki Mzazi aliyekulipia ada, hakulipa bure! Mungu akajibu kila ombi la moyo wake!

Tunajiona tuko sahihi sana, tukikosolewa tunakua Wakali kama nyigu mjamzito! Kejeli, vijembe, ulimbukeni, kujikweza na kujiona kuwa tuna kila kitu na hakuna wa kutubabaisha....! Tutakuja kuanguka vibaya tukose wa kutusaidia
 
mkuu brazaj majirani wivu tu unawasumbua,si unajua tupo uchumi wa kati,hao wanatuonea gere hawajaja lakin mzee wetu tumempumzisha kwa amani nyumba yake ya milele

Mkuu nakusoma na hasa kwa mistari kwa mstari kama ulivyoandika.

Subiri waje na vibwagizo zaidi na mapambio ya kujazia. Huwezi kuamini!

Heshima kwake aliyeandika hili:

IMG_20200801_100446_674.jpg


Natamani ingekuwa ni jinamizi, lakini kwa bahati mbaya ndiyo ukweli wenyewe.
 
Katika hili nani mwenye sauti hii ni sawa na kuziba kwa wenzetu wakati kwetu kunatobo,
kama tumeshindwa kujenga umoja baina yetu na kutengeneza matabaka kati ya wananch na wananch, wananchi na viongozi, viongozi na viongozi unazani unaweza vipi kuweka usawa wa nje
wananchi na viongozi wanaoishi Tanzania Hawana sauti juu ya ardh Yao wenyewe lakin pia wanaishi kwa uoga usio kifani lakini pia hakuna umoja baina yao
TZ
Sikia usiongee
ona usitende
 
Umeongea vitu vya msingi

But points of correction katika msiba wa Mandela JK Alienda na alitoa speech

Mkuu hiyo ni point of addition (badala ya correction) zaidi sana ya kuwepo tu. Tulikuwapo tukapewa na heshima zaidi kutoa speech.

Hata kwenye msiba wa rais Moi (rip) zaidi sana ya kuwapo, tulipewa pia heshima kama hiyo ya kutoa speech.

Hii ni kama ilivyokuwa kwa Madeline Albright mwakilishi wa beberu kwenye msiba wa mwalimu (rip).
 
Muwe wazalendo basi. Au mmetumwa na mabeberu? Hii ni vita ya kiuchumi. Bro Magu chapa kazi. Usisikilize kelele za chura. Hongera sana kwa kulijengea taifa heshima

Mkuu nakusoma kwa mstari kwa mstari.

Inafahamika kuwa kuna tofauti za wazi baina ya kujifanya mzalendo na kuwa mzalendo.

Kwa maneno ya mwalimu (rip), "kama anachukia rushwa, mwangalie usoni, siyo kwa maneno matupu."

IMG_20200801_100446_674.jpg


Ni kwa kutambua hayo ndiyo maana vibwagizo pendwa vya mapambio vimechelewa.

Watakuwa wamenuna wakitokwa mapovu utadhani wamemeza "OmO."
 
Back
Top Bottom