Wanaosema Uongo Wanaaminika Na Wanaosema Ukweli Hawaaminiki

Wanaosema Uongo Wanaaminika Na Wanaosema Ukweli Hawaaminiki

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,234
Reaction score
1,743
Yn 8:45 SUV
[45] Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.

Yesu alikuwa anasema ukweli, ila kuna watu walikuwa hawamwelewi kabisa, wao walikuwa na mambo yao wanayoyaamini.

Utakuwa shahidi wa hili, mara nyingi watu huwa wanakimbilia kwenye uongo kuliko ukweli, kwa sababu unavutia na kuwafariji kwenye mambo yao maovu.

Mtu akitokea anadanganya na kuwafariji watu kwenye eneo wanalolipenda, atakuwa na watu wengi sana wanaompenda na kumfuata.

Uongo wakati mwingine unavutia sana kuliko ukweli, ndio maana unapendwa na wengi.

Yn 8:46 SUV
[46] Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?

Watu wanaweza wasikuamini kabisa, si kwa sababu unasema uongo, ni kwa sababu unasema ukweli.

Si kila mtu anayeaminiwa ni mkweli, na si kila mtu asiyeaminiwa ni muongo, watu wanaweza wasikuamini kabisa kutokana na ukweli unaousema.

Haipaswi kukupa shida wewe unayesema ukweli alafu watu hawakuelewi unachosema au kuwaambia, na isikutishe unapokuwa na maadui kutokana na kusimamia ukweli.

Isikupe kuvimba kichwa kwa sababu watu wanakusikiliza na kukufuata, huku unajua unachowaambia watu ni uongo, na yote unayoyafanya ni ya uongo.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 
Back
Top Bottom