Watanzania Kuna haja ya kuwa na uzalendo, uadilifu na hofu ya Mungu

Emmanuel Mkwama

Senior Member
Apr 24, 2013
165
122
"Sipendi kujihusisha na mambo ya siasa wala kuchangia chochote kuhusiana na mambo ya siasa."

Ndugu zangu heri nyingi ziwafikie,nikiwa salimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.........

Ndugu zangu kiukweli siasa sipendi kwa sababu ya michezo michafu iliyopo kwenye siasa. Lakini leo ningetamani kuandika jambo moja nikijaribu kushare nanyi kuhusiana na ya uadilifu,uzalendo + hofu ya Mungu.

Kiukweli kwa sasa tulipo fika kama Taifa kuna haja ya kuwa na katiba yenye kutamka na kuogopewa na wale wote wenye kufanya ama kuingia mikataba ya ovyo pamoja wale wote wenye tabia ya kula rushwa ama kufuja mali za umma. Katiba ingetamka moja kwa moja wale wote wenye kufanya haya ni kupigwa risasi hadharani na kutaifisha mali zake zote.

Kiukweli kuna walaka unaendelea kusomwa wa kanisa katoliki ambao mimi pia ni muhumini huko,ndipo kulipo ni ibua huko na kuja na wazo langu hili la kupigwa risasi hadharani kwa wale wote wenye kuishauri serikali vibaya na kuingiza nchi ama Taifa kwenye shida.

Nahisi taifa kama taifa lingekuwa na hofu na nidhamu ya uadilifu Inge shamiri miongoni mwao viongozi ama wa shauri wa rais.

Nawatakia mapumziko mema na usiku mwema.
 
"Sipendi kujihusisha na mambo ya siasa wala kuchangia chochote kuhusiana na mambo ya siasa."

Ndugu zangu heri nyingi ziwafikie,nikiwa salimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania...
Kwani unafikiri kwanini wanazuga sana kuleta katiba mpya? Wanajua kabisa itaenda kuwaumiza wao wenyewe! Unategemea una washauri kama Kikwete, Chenge ndiyo wakushauri ulete katiba mpya ambayo itasema wote waliojipatia mali kwa njia zisizo halali wafungwe na kutaifisha mali zao? Hawataki sababu ni hiyo kuogopa kupoteza.
 
Hakuna shule wala Chuo wala kozi yoyote inayofundisha hayo! Haki ikitamalaki katika taifa automatically matokeo ndio hayo. Walafi waliovimbiwa na kusaza mali za umma eti wanafundisha uzalendo! Pumbavu.
 
Kiukweli kelele zinapokuwa nyingi za ulaji wa rushwa na kufuja mali za umma plus mikata isiyokuwa na tija kwa taifa, inasababisha amani, upendo na mshikamano kama taifa vinapotea
 
Uadilifu sio kitu cha kutengenezwa bali ni tabia ya mtu ambayo inaweza kutokana na malezi jumlisha imani yake.
Uadilifu wa mtu unatoka moyoni kama vile mtu anayemuamini Mungu asiyemuona na kuwa na hofu juu ya matendo maana kila mahali Mungu yupo...

Huwezi kutenganisha uadilifu na tabia za mtu ,mtu anakuwa hovyo mpaka kweny familia yake uzinzi na kutowajibika kweny malezi ya familia yake.

Nchi kama china , Japan na iran n.k....Hao wanawekeza kweny maadili na usipokuwa muadilifu unanyongwa kwa sababu unakuwa kama umevunja maadili ya jamii kwa ujumla kama baadhi ya mila za kiafrica watu wanauliwa hata kutengwa wakienda kinyume.

Nchi ya Tanzania haiwezi kuwa na uadilifu kwa sababu watu hawachaguliwi kwa mlengo wa tabia na uwezo wa kielimu ila siasa na vyama ambavyo ni chanzo cha utapeli, wizi na uongo ndo vinawaweka madarakani na kushika nyadhifa mbalimbali.
 
Kiukweli kwa sasa tulipo fika kama Taifa kuna haja ya kuwa na katiba yenye kutamka na kuogopewa na wale wote wenye kufanya ama kuingia mikataba ya ovyo pamoja wale wote wenye tabia ya kula rushwa ama kufuja mali za umma. Katiba ingetamka moja kwa moja wale wote wenye kufanya haya ni kupigwa risasi hadharani na kutaifisha mali zake zote.
Watu tunapambania adhabu ya kifo ifutwe, it's barbaric, mwenzetu unataka tupige risasi!.
Kiukweli kuna waraka unaendelea kusomwa wa kanisa Katoliki ambao mimi pia ni muumini huko,ndipo kulipo ni ibua huko na kuja na wazo langu hili la kupigwa risasi hadharani kwa wale wote wenye kuishauri serikali vibaya na kuingiza nchi ama Taifa kwenye shida.
Suppose hili linakubalika na pia wale wote wanaopinga mipango ya serikali kutuletea maendeleo nao wafanywe hivyo hivyo, tukianzia wale waandika waraka, ungekubali?.
P
 
Uadilifu sio kitu cha kutengenezwa bali ni tabia ya mtu ambayo inaweza kutokana na malezi jumlisha imani yake.
Uadilifu wa mtu unatoka moyoni kama vile mtu anayemuamini Mungu asiyemuona na kuwa na hofu juu ya matendo maana kila mahali Mungu yupo....
Hapa ndipo tunapaswa kuigeukia taasisi ya usalama wa taifa,yenyewe ilipaswa kuanda viongozi wa baadae kupitia makuzi ya chini hatua kwa hatua. Nahisi tusinge kuwa na viongozi wenye upungufu wa maadili.
 
Watu tunapambania adhabu ya kifo ifutwe, it's barbaric, mwenzetu unataka tupige risasi!.

Suppose hili linakubalika na pia wale wote wanaopinga mipango ya serikali kutuletea maendeleo nao wafanywe hivyo hivyo, tukianzia wale waandika waraka, ungekubali?.
P
Mkuu Pascal mayalla heshma yako,maoni yako ni yapi ili kuweza kutibu swala zima la uadilifu na kuwajibika kwa viongozi wa umma?
 
Huu upuuzi unasaidia nini sasa katika nchi ?

Fear of unknown, sijui kwa nini waafrika bado tu fikra za kipuuzi kama hizi
Mkuu binafsi ninapokuwa na hofu ya Mungu,nitashindwa kuiba mali ya umma ama kwenda kinyume na katiba ambayo ipo kwa mfanano wa biblia ama msahafu.
 
Sipendi kujihusisha na mambo ya siasa wala kuchangia chochote kuhusiana na mambo ya siasa."

Ndugu zangu kiukweli siasa sipendi
Sasa kama hupendi hapa umefuata nini sasa ?

Halafu hii tabia ya kijinga kwa mtu aliye balehe anasema hapendi kujihusisha na masuala ya siasa ni ya kipuuzi sana ndio maana mambo ya kijinga yana endelea nchini na watu wapo kama makondoo kwa tabia za kipuuzi kama hizi.

Usipopenda wewe siasa na kutotaka kujihusisha nazo unataka nani sasa azipende kwa faida yako ?
 
Mkuu punguza jazba,twende hatua kwa hatua. Ili nikufundishe siasa,wewe ulihitaji nifanye nini ili kufikisha kinacho nisibu? Pia kama unataka nikuamini njoo na uwalisia wako nitakujibu pasipo kutumia uwalisia uliojificha nyuma ya so special. Karibu mkuu tuendelee
 
Hakuna jazba hapa kusema hupendi siasa kwa mtu aliye balehe ni ujinga na upumbavu uliokomaa siihitaji kujazia zaidi, inatosha.
 
Back
Top Bottom