Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Kuna video clip ninaiona mtandaoni ikisambaa ,Mtu akimkata mtu na panga aliyemshukia kuwa ni mwizi. Na watu husema hapo ni Tanzania,pia hata Kama sio Tanzania.
Huu ni ukatili wa hali ya juu ,huu ni ukatili wa hali ya juu sana.
Haijalishi huyu Mtu anayepigwa amefanya kosa gani ,haijalishi kabisa kabisa! ,ni kinyume kabisa na haki za binadamu ,haya ni mateso,huo ni unyama,ukatili,na kunaweza pelekea kifo cha watu hao,hii ni Mob Violence.
Hili ni jambo ambalo kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) wamekuwa wakikemea na kuandika katika Ripoti zao za kila mwaka (Mob violence),haipaswi watu kujichukulia sheria mkononi.Haipaswi kabisa kabisa.
Tuna vyombo vya usalama na haki,tuna @policetanzania ,tuna mahakama .Nchi hii inaongozwa na sheria na taratibu hakuna yeyote anayeruhusiwa kuchukua sheria mkononi ,haitakiwa kabisa.
Ukimsoma Thomas Hobbes ,kitabu chake Cha Leviathan amezungumzia juu ya hali hii , amezungumzia juu ya "state of Nature" anasema hali ingekuwaje Kama kusingekuwa na mamlaka au Serikali (Anarch state/system) . Anasema kusingekuwa na mamlaka kila Mtu angekuwa na haki ,uwezo wa kufanya chochote anachopenda sababu binadamu ni mbinafsi ,(egoist,selfish) na hii ingepelekea Vita miongoni mwa watu dhidi yao wenyewe ,yaani A war of all against all (Bellum Omnium Contra Omnes),watu tungeuwana tungechinjana kungekuwa hakuna shughuli za uzalishaji.
Ndio maana akaongelea theory ya Social contract ,kuwa tunachagua serikali kwa kupunguza mamlaka yetu kuipa serikali na serikali ina tulinda ,ndio maana kuna ulinzi ,polisi , mahakama lazima vyombo hivi tuvitumie na sio kujichukulia sheria mkononi Kama hivi, sio rahisi kujua kama huyu ni mwizi au sio mwizi isipokuwa Mahakama tuu.
Ni sawa upite barabarani Mtu anaweza kukuita Mwizi , mwizi!!! Ila hujaiba chochote, tuseme tukupige kwa mapanga tuu sababu umeitwa mwizi? ,Ndio maana tunasema vyombo vya sheria vipo kuthibitisha na kutoa adhabu ila sio huu ukatili.
Watanzania wenzangu kwa umoja wetu tukemee swala hili ,tufichue wahusika,tuwaweke wazi wachukuliwe hatua Kama hii imetokea Tanzania.Tukemee sana vitendo vya kuchukua sheria mkononi.
Abdul Nondo.
Sent using Jamii Forums mobile app