Watanzania baadhi tuepuke kujichukulia sheria mkononi

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
Kuna video clip ninaiona mtandaoni ikisambaa ,Mtu akimkata mtu na panga aliyemshukia kuwa ni mwizi. Na watu husema hapo ni Tanzania,pia hata Kama sio Tanzania.

Huu ni ukatili wa hali ya juu ,huu ni ukatili wa hali ya juu sana.

Haijalishi huyu Mtu anayepigwa amefanya kosa gani ,haijalishi kabisa kabisa! ,ni kinyume kabisa na haki za binadamu ,haya ni mateso,huo ni unyama,ukatili,na kunaweza pelekea kifo cha watu hao,hii ni Mob Violence.

Hili ni jambo ambalo kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) wamekuwa wakikemea na kuandika katika Ripoti zao za kila mwaka (Mob violence),haipaswi watu kujichukulia sheria mkononi.Haipaswi kabisa kabisa.

Tuna vyombo vya usalama na haki,tuna @policetanzania ,tuna mahakama .Nchi hii inaongozwa na sheria na taratibu hakuna yeyote anayeruhusiwa kuchukua sheria mkononi ,haitakiwa kabisa.

Ukimsoma Thomas Hobbes ,kitabu chake Cha Leviathan amezungumzia juu ya hali hii , amezungumzia juu ya "state of Nature" anasema hali ingekuwaje Kama kusingekuwa na mamlaka au Serikali (Anarch state/system) . Anasema kusingekuwa na mamlaka kila Mtu angekuwa na haki ,uwezo wa kufanya chochote anachopenda sababu binadamu ni mbinafsi ,(egoist,selfish) na hii ingepelekea Vita miongoni mwa watu dhidi yao wenyewe ,yaani A war of all against all (Bellum Omnium Contra Omnes),watu tungeuwana tungechinjana kungekuwa hakuna shughuli za uzalishaji.

Ndio maana akaongelea theory ya Social contract ,kuwa tunachagua serikali kwa kupunguza mamlaka yetu kuipa serikali na serikali ina tulinda ,ndio maana kuna ulinzi ,polisi , mahakama lazima vyombo hivi tuvitumie na sio kujichukulia sheria mkononi Kama hivi, sio rahisi kujua kama huyu ni mwizi au sio mwizi isipokuwa Mahakama tuu.

Ni sawa upite barabarani Mtu anaweza kukuita Mwizi , mwizi!!! Ila hujaiba chochote, tuseme tukupige kwa mapanga tuu sababu umeitwa mwizi? ,Ndio maana tunasema vyombo vya sheria vipo kuthibitisha na kutoa adhabu ila sio huu ukatili.

Watanzania wenzangu kwa umoja wetu tukemee swala hili ,tufichue wahusika,tuwaweke wazi wachukuliwe hatua Kama hii imetokea Tanzania.Tukemee sana vitendo vya kuchukua sheria mkononi.

Abdul Nondo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo jikite kwenye masomo bana. Wezi wanakera sanaa. Mfano mtu unaiba na kukwapua hela ya walipa kodi hazina halafu unazitapanya bila aibu na huruma. Huyo ni wakuhurumiwa?
 
Dah nilijua unamsema Ndugai anayejichukulia katiba mkononi kumkejeli CAG kwa maneno ya kipuuzi yaliyosheheni wendawazimu wa madaraka asiyo na sifa nayo.Kwakweli hili lispeaker linatupa majaribu tumtandike humu kwa lugha gani maana tunaogopa bhana....Mungu atusaidie tumsitir na unorganised mishav
 
Abdul Nondo hapa ungejikita kuelezea pia sababu na chanzo cha mob violence/justice kuliko kutuelezea matokeo/effect! Unatoka zako kibaruani umechoka hoi,mfukoni huna hata nauli ya basi/daladala/hiace! Unaamua kutembea kwa miguu,mara wanakutokea hao vibaka na kukuamuru uwape pesa! Unawaambia huna na wanaanza kukutoboa toboa kwa visu huku wakikucharanga mapanga bila huruma kama vile wanakudai roho ya mama yao au baba yao!! Hapo nyumbani familia inakusubiri ufike ufanye maujanja ili wapate angalau mlo,badala yake wanaletewa taarifa ya msiba wa Baba!!!! Imagine! Think twice! Kama huwezi kuwaua niite mimi ntakuja na petrol yangu na kibiriti kabisa!! Nimeshuhudia mengi hadi nikahisi kama Mungu ametutenga!! Acha wauliwe tu mkuu!tenna wafe kabisa,asiachwe hata ashushe pumzi ya mwisho kwa amani!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom