Watanzania adui yetu mkubwa ni CCM na mfumo wake

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Napenda watanzania waelewe vizuri kuwa CCM ndio adui yetu mkubwa. CCM ipo madarakani kwa miaka 60 sasa na bado tunahangaika na maji vijijini, madawati, chakula na magonjwa yanayotibika bado yanaua watu nchi hii.

Blaa blaa za CCM zimeifikisha nchi hii katika umaskini mkubwa hata baada ya kuwa na rasilimali nyingi. Wanasiasa wa CCM ndio wanaofaidika na mfumo CCM, huku mamilioni ya watanzania wakiambulia vumbi, kuwapungia mikono na kuwashangilia wezi ambao wanakuja kwao kwa kivuli cha viongozi.

Ndugu zangu watanzania ni wakati muafaka wa kuondokana na CCM na mfumo wake. Mfumo wa CCM ni mkubwa sana nchini na mtandao wa kimkakati wa kutawala milele na kuiba mali za watanzania kwa visingizio vingi.

Natoa mwito kila mtanzania mwenye akili timamu afanye chochote kuikataa CCM na mawakala wake.
 
Kwa sasa tatizo letu kubwa kabisa ni Samia na ujinga wake, huyu akiachwa bila kuambiwa ukweli anaweza kutupeleka utumwani hata hao CCM wenzake waje kukosa wa kuwatawala.

Kwanza tuanze ku deal na hiki kichwa kibovu kinachotuongoza kilichopoteza mwelekeo, kinachotupeleka shimoni, naamini ni rahisi zaidi kuondoa kichwa kibovu tubaki salama kwa muda, ili baadae ndio tufikirie namna nzuri ya kuondoa huo mfumo mbovu uliotuletea hiki kichwa kibovu kinachotusumbua kwa sasa.
 
Back
Top Bottom