Watanzania Abroad mnani??

Watanzania Abroad mnani??

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,160
Wakuu heshima mbele.

Nimefikia uamuzi wa kuuliza hili kutokana na tafiti zangu binafsi kupitia kusoma blog mbali mbali na kuongea na baadhi ya watanzania waishio majuu.

Je kwanini watanzania wengi walioko majuu wanaonekana kuwa na mtizamo mbaya kuhusiana na kujichanganya na watanzania wenzao wanaoishi nje kwamba wengi wao ni nuksi, majungu na majanga?? je ni kweli watanzania (walio wengi) ni nuksi, wambea na wajaa majungu wakiwa huko majuu? Ni juzi tu mke wa mzungu aliweka mada kuhusu wabongo majuu na watu walitiririka kwa kina kabisa kuonyesha kwamba Watz walio wengi huko majuu ni nuksi na si watu wazuri kujichanganya nao na kujenga urafiki.

Binafsi siishi huko hivyo sijabahatika kuishi nao wakiwa huko nje na kuona tabia zao. Je shida ni nini haswa?

Kibongo bongo (ki hapa hapa home) najua kweli wabongo ni nuksi, ila kwa majuu nilidhani kwa kujichanganya na wengine ule unuksi wa kibongo utapotea.

Nawasilisha.

CC Wabeba box na walea vibibi wote.
 
What do you mean kibongo bongo (yaani huku home) wabongo ni nuksi? Chunguza entourage yako maana wadhungu wanasema birds of a feather...
 
neno nuksi si zuri ila umbea sawa mjaasili haachi asili.sijui nchi nyingine ila nilikopita mm mmh umbea upo asikwambie mtu.
kujichanganya na wazungu hakubadilishi chochote unless uzaliwe huko. wanasengenyana sana mtu usifanye kitu kila mtz aliyeko eneo hilo atajua.ila jamani hata wazungu wanaumbea kaa nao utawajua vizuri
 
Hiyo ni dhana potofu tu.

Ni potofu kwa sababu umbeya, upikaji majungu, na fitna ni tabia za kibinadamu.

Katika jamii nyingi kama siyo zote, watu wa aina hiyo wapo.

Sasa kudai hujichanganyi na wabongo walio majuu sababu eti wana tabia hizo ni kupotoka kwa sababu hata watu wa mataifa mengine wanazo hizo tabia.

Na mtu yeyote anayeamini kwa ujumla dhana kama hiyo basi huyo si 'observer' mzuri wa tabia za watu.
 
.. kusengenya au umbea ni hulka na sidhani inasababishwa na utaifa wa mtu, bali mazingira anayoishi na pia background yake!
.. watz wanasemekana sana kuwa na katabia hako, labda ndo mazingira wengi tuliokulia ila nadhani kama umejichanganya na waafrika utaelewa kuwa si tatizo la watz pekee, waafrika wengi wana katabia hako!
.. Mrembo by Nature siku ukienda kubeba maboksi jaribu kujichanganya na wadhungu, hakika utapata picha nyingine ya hawa watu. Hata wao wanasengenya, wanasemana na pia ni wambea! (binamu yangu ndo kasema haya, nae anabeba zege huko)
 
Last edited by a moderator:
Labda kwa wanawake ila kwa wanaume maisha huwa ya furaha na kusaidiana.
 
Wakuu heshima mbele.

Nimefikia uamuzi wa kuuliza hili kutokana na tafiti zangu binafsi kupitia kusoma blog mbali mbali na kuongea na baadhi ya watanzania waishio majuu.

Je kwanini watanzania wengi walioko majuu wanaonekana kuwa na mtizamo mbaya kuhusiana na kujichanganya na watanzania wenzao wanaoishi nje kwamba wengi wao ni nuksi, majungu na majanga?? je ni kweli watanzania (walio wengi) ni nuksi, wambea na wajaa majungu wakiwa huko majuu? Ni juzi tu mke wa mzungu aliweka mada kuhusu wabongo majuu na watu walitiririka kwa kina kabisa kuonyesha kwamba Watz walio wengi huko majuu ni nuksi na si watu wazuri kujichanganya nao na kujenga urafiki.

Binafsi siishi huko hivyo sijabahatika kuishi nao wakiwa huko nje na kuona tabia zao. Je shida ni nini haswa?

Kibongo bongo (ki hapa hapa home) najua kweli wabongo ni nuksi, ila kwa majuu nilidhani kwa kujichanganya na wengine ule unuksi wa kibongo utapotea.

Nawasilisha.

CC Wabeba box na walea vibibi wote.

Hii ina ukweli kwa sababu hata ukiangalia hapa Bongo asilimia kubwa ya watanzania majungu na umbea ni jadi yao na ndiyo maana hata wakienda nje wanazidi kuendekeza ujinga ule ule.
 
Umbea hauna shule. Umbea ,majungu , masengenyo havina ukabila ,udini,utaifa ,labda umri tu. watoto chini ya miaka 15 labda ,vinginevyo wote tumo kwenye kundi hilo. Hata hii mada imo ndani.
 
Labda kwa wanawake ila kwa wanaume maisha huwa ya furaha na kusaidiana.
maisha ni kujichanganya bwana...maneno yapo hata kwenye kanga yapo...aani uogope kujichanganya kisa utasemwa..kwani ukisemwa wewe wa kwanza? huko ni kutojiamini na ushamba tu...
 
Hiyo ni dhana potofu tu.

Ni potofu kwa sababu umbeya, upikaji majungu, na fitna ni tabia za kibinadamu.

Katika jamii nyingi kama siyo zote, watu wa aina hiyo wapo.

Sasa kudai hujichanganyi na wabongo walio majuu sababu eti wana tabia hizo ni kupotoka kwa sababu hata watu wa mataifa mengine wanazo hizo tabia.

Na mtu yeyote anayeamini kwa ujumla dhana kama hiyo basi huyo si 'observer' mzuri wa tabia za watu.
ndo maana sometimes nakupenda super mbabebs....labda wataje mataifa ambao hawana hizo tabia...
 
........It begins with you.........
Naupenda sana huo msemo, na sijui kwa nini kila kunapotokea kitu katika maisha yangu kabla sijaona mwenzangu kakosea huwa naanza kujichunguza mimi, that is me!
kuna watu maisha yao ni drama tupu, sasa anaona akiwa nje bora ajichanganye na watu ambao hawamjui ili hata anapofanya drama zake hajali, maana anajua siyo wengi watajua, lakini sasa akijichanganya na wabongo halafu akafanya hayo mambo basi bongo yote watajua. Binadamu wote tunasema, ila sasa unaangalia je huyu atasema kwa population ipi? ina impact gani katika maisha yangu? hata wale wanaosema hawa-mind kusemwa lakini kitu kinaposema kuhusu wao wana-mind sana, hata kama ni kimya kimya
 
Inategemea una deal na watu wa class gani.

Unaweza kujichanganya na kina Shanikwa huko ukakuta ndo kuna umbeya na ma beef kuliko wabongo.

Na unaweza ku deal na class ya wabongo waliotulia na kustaarabika kitambo.

I don't go out of my way to meet wabongo just because they are from bongo.

And similarly, I don't go out of my way to avoid meeting wabongo, just because they are from bongo.

I treat all people with a sober equanimity like the scales of a magistrate.

And discern according to the content of their character, not the creed of their nationality.
 
Kusemwa kupo jamani ila inategemea unasemwa vipi, kama alivyotangulia kusema FP unapomwoshea mtu kidole kumbuka vidole vinne vinakupoint wewe so jichunguze wewe kwanza.
 
Mrembo by Nature Hii ndiyo sababu kubwa aliyoieleza Fixed Point, nimem-quote hapo. I have several vivid examples, wengi wanakwepa macho ya wabongo wenzao na habari zao kusambaa huko walipo na kwa tanzania pia.

........It begins with you.........
Naupenda sana huo msemo, na sijui kwa nini kila kunapotokea kitu katika maisha yangu kabla sijaona mwenzangu kakosea huwa naanza kujichunguza mimi, that is me!
kuna watu maisha yao ni drama tupu, sasa anaona akiwa nje bora ajichanganye na watu ambao hawamjui ili hata anapofanya drama zake hajali, maana anajua siyo wengi watajua, lakini sasa akijichanganya na wabongo halafu akafanya hayo mambo basi bongo yote watajua. Binadamu wote tunasema, ila sasa unaangalia je huyu atasema kwa population ipi? ina impact gani katika maisha yangu? hata wale wanaosema hawa-mind kusemwa lakini kitu kinaposema kuhusu wao wana-mind sana, hata kama ni kimya kimya
 
........It begins with you.........
Naupenda sana huo msemo, na sijui kwa nini kila kunapotokea kitu katika maisha yangu kabla sijaona mwenzangu kakosea huwa naanza kujichunguza mimi, that is me!
kuna watu maisha yao ni drama tupu, sasa anaona akiwa nje bora ajichanganye na watu ambao hawamjui ili hata anapofanya drama zake hajali, maana anajua siyo wengi watajua, lakini sasa akijichanganya na wabongo halafu akafanya hayo mambo basi bongo yote watajua. Binadamu wote tunasema, ila sasa unaangalia je huyu atasema kwa population ipi? ina impact gani katika maisha yangu? hata wale wanaosema hawa-mind kusemwa lakini kitu kinaposema kuhusu wao wana-mind sana, hata kama ni kimya kimya
ushamba tu dear ..unakimbia ndugu zako kisa kusemwa? kwanza kwa nini uhisi utasemwa? ...kujiona kusipo na maana...
 
Back
Top Bottom