Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,743
Ndugai amesema huyo mandishi anatafuta cheap popularity..........a new term in the hood.
Wanabodi,
Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).
Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.
Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.
SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012
Hii nchi kweli shamba la bibi mpaka wakati wa Nyerere napo watu wamefanya ufisadi, tatizo muandishi kaficha majina.
kwangu mimi hii si habari,,,,,NAHITAJI HABARI,HABARI YENYE MAJINA YA WALIOFICHA,,,,NA SI KUWATAJA PIA WAFIKISHWE MAHAKAMAN,NA SI TU KUWEKWA MAHAKAMAN PIA WAPOKWE HAYO MAHELA,NA SI KUPOKWA TU WANAPASWA KUHUKUMIWA JELA,NA SI KUHUKUMIWA TU PIA WAFILISIWE
Nakumbuka clearly kwenye mahojiano ITV, alikuwepo Dr Slaa, Sita na some other guys, Dr. Slaa akaonyesha jinsi gani fedha zimeibiwa na kuonyesha evidence mpaka za receipt na scanned letters.Wewe ukiona wanatumia terms zenye utata, mwenye akili unajuwa kwamba kuna kitu pale si bure! Kumbuka spika SITA alivyo brush aside list ya mafisadi iliyo andikwa na wazalendo mtandaoni - nini kilitokea baadae, ikaja gundulika kwamba taharifa hizo za mtandaoni ni za kweli.
Watanzania tulivyo wa hajabu wakati mwingine kwa kushindwa kutabirika, SITA huyo huyo kahanza kulivalia njuga swala la ufisadi ambalo aliwahi kulipinga na kubeza sources zake, si ajabu historia ikajirudia tena katika suala hili - time will TELL.
Huyo ni Jakaya Kikwete tu
Wanabodi,
Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).
Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.
Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.
SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012
Watanzania tulivyo wa hajabu wakati mwingine kwa kushindwa kutabirika, SITA huyo huyo kahanza kulivalia njuga swala la ufisadi ambalo aliwahi kulipinga na kubeza sources zake, si ajabu historia ikajirudia tena katika suala hili - time will TELL.
Hii nchi kweli shamba la bibi mpaka wakati wa Nyerere napo watu wamefanya ufisadi, tatizo muandishi kaficha majina.
Hivi mpaka hizi propaganda ziishe,hawa wezi si watakuwa wameshahamisha hizi fedha kwenda kwenye account nyingine mbili tatu?
Kuwa na fedha nyingi si tatizo. Watu wangependa kujua zilivyopatikana.
Pili, kama kiasi kinajulikana kwa nini majina yasiwekwe hadharani ili nao wapate kutueleza jinsi walivyopata utajiri huu?
Ni vyema majina yakawekwa wazi hususan yale ya wanasiasa na maofisa Wa Serikali.