Watambue madalali wa shetani

Hongera sana mtoa hoja, je kumpa Mungu asilimia kumi ya mali yako imekaaje? Mungu amechoka kiasi cha kuhitaji pesa yako?
 
hii ya leo ni kibokoooo
nimefurahi sana, kumbe uko pande zote mkuu maana naona watu wakishindwa kulala usiku wanakukumbuka sana,
hii imedhihirisha kuwa ushauri pande zote uko makini
big up mkuu
[emoji23] [emoji23] [emoji115] [emoji115] [emoji123] [emoji120] [emoji120]
 
Sawa kwa kutoa unapokea, sipeleki kanisani au msikitini, nawapa mwenyewe watu wanaonizunguka kwani ninawafahamu. Nimekosea?
 
Mukuu naona unamchokoza gwajima jiandae kama bashite koromije malyangili.
 
Hakuna cha kumchokoza mtu toa maoni yako,na uwe huru ,Muumba anapenda watu kama wewe
 
naona maza kashatafunwa tayari,chezea mchungaji anapotamani kondoo.
 
kama Yesu angeamua kutumia hii neema angekua tajiri wa kupitiliza mpaka sasa. aliweza kufufua mpaka wafu na kujifufua mwenyewe.lakini bado aliishi na kufa kimasikini kabisa.
 
Baba umenena kweli.hawa ni wapiga dili wakutupwa.pesa wanazowakamua waumini wao Mungu anawaona
 
Amen kwa somo
 
Dada zetu na mama zetu ndio wahanga wakubwa wa hawa madalali,wanaume ni wachache.
 
Hongera sana mtoa hoja, je kumpa Mungu asilimia kumi ya mali yako imekaaje? Mungu amechoka kiasi cha kuhitaji pesa yako?

Nijuavyo ikiwa sijakosea...kuna Sadaka maalum za aina 3, sawasawa na maagizo ya Biblia Takatifu.

Sadaka ya moja ya kumi (Ten percent) inayotokana na jasho lako la kuajiriwa ama kujiajiri. Inaitwa ZAKA.

Sadaka ya Shukran kwa yale aliyokufanyia Mungu wako, haijalishi ni mazuri au mabaya...Biblia inatuambia Shukuruni kwa kila jambo. Inaitwa DHABIHU

Sadaka ya Mzaliwa wa kwanza wa Mazalia ya mifugo au kilimo chako. Mfano unaanza kufuga ng'ombe au mbuzi dume na jike, watakapozaa kwa mara ya kwanza kabisa...yule ndama usimwache pale zizini mpeleke kama sadaka katika madhabahu ya Mungu....Inaitwa MALIMBUKO.

Sasa katika sadaka hizo...hiyo DHABIHU/SHUKRAN unaweza kuamua kuipeleka kwa Watoto yatima,kwa wagonjwa mahospitali, Masikini na wenye shida na taabu mbalimbali.

LAKINI : Nathubutu kukuambia katika sadaka hizo zote usije ukacheza na ZAKA yaani 1/10. Mungu mwenyewe anasema usipoitoa umemwibia.

Madhara ya kutotoa ZAKA ni makubwa sana na ni mengi kama:-

1) Kufilisika kabisa

2) Pesa/Mshahara wako kutokufanya chochote cha maana mpaka unakwisha

3) Kufutwa kazi / kufa kwa Ajira kabisa kwakuwa unakosa ulinzi na utetezi wa Mungu katika Ajira yako.

4) Kuaibika, kutokutoa ZAKA pia kunakusababishia AIBU katika maisha.

USHAURI: Jitahidi sana usiache kutoa SADAKA haswa ZAKA ila hakikisha unatoa katika MADHABAHU SAHIHI kwa MTUMISHI SAHIHI.


Barikiwa.
 
Kichwa changu kimeathiriwa na kirusi sisiem, hicho kichwa cha habari nilikisoma "Watambue madalali wa madiwani" serious.
 
Kichwa changu kimeathiriwa na kirusi sisiem, hicho kichwa cha habari nilikisoma "Watambue madalali wa madiwani" serious.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
umenena kweli tupu mkuu!
 
umenena kweli tupu mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…