Watakatifu ni wazungu waliokufa zamani. Waafrika waliokufa zamani eti ni mizimu

Nipo hapa kwenye kanisa la Roma wanafanya harambee mchangishaji anasema kama wewe ni mwanaume kweli tuletee elf 10 hapa ukiendelea kubaki kwenye Viti tutakuangalia mara mbili mbili huku anawahadaa watu kwa kwaya nzuri
Nimekaa hapa huku naangalia misa ila huu ushawishi mkubwa unao tumika kukusanya sadaka unanipa mashaka makubwa

Sadaka nzuri n kwenda kuwapa chakula wenye njaa siyo kuwaletea Hawa wadau wanasukuma ndiga kali
 
Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
Nafikiri tatizo lipo kwako wewe binafsi na sii imani ya ukristo.
Ukristo hauna maombi ya kuomba wafu ama ni weupe au weusi wakuombee.

Ndio maana ukitazama biblia yote hakuna agizo kama hilo. Muombezi na mpatanishi wetu ni mmoja tu yaani Yesu Kristo.
Huyu pekee ndie aliyeonja mauti na kufufuka na kuondoka na mwili wake wa nyama na damu kuelekea mbinguni. Watakatifu wengine

wote miili yao ya nyama na damu imo makaburuni ila nafsi zao ndio zipo hai uweponi mwa Mungu.
Kimaandiko hazijawahi kupewa wala sii kazi yao kuombea wala kupatanisha.
 
#Methali 18:21
"Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua; wanaopenda kuutumia watakula matunda yake.

#370.Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w Bihar al Anwaar J.71 UK. 277.

" Miongoni mwa mambo yote, ulimi unastahili kuwekwa katika mahabusu kwa kipindi kirefu zaidi kuliko kitu kingine chochote. (Kwa sababu madhambi yetu mengi yanatokana kama vile kuwasuta watu, kusema uongo, kuzua mambo, kuwadhihaki wengine, na vile vile kuwatuhumu watu wengi n.k)

#ULIMI NA MAOVU YAKE.
 
Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
Mashahidi wa Uganda?
Bernadeta?
 
Back
Top Bottom