Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Rejea kichwa cha habari tajwa hapo juu.

Dini ndio chanzo cha matatizo mengi Duniani. Katika Dunia ya leo raia wanakosa ushirkiano tu kwa sababu wanatofautiana Kidini, Mkristo anambagua Muislamu na Muislamu anambagua Mkristo. Na ubaguzi wa kidini hauzungumzwi sana ila kiukweli ndio unaotendeka kwenye ofisi nyingi na taasisi nyingi, siku hizi ubaguzi wa kikabila unaenda ukipungua, huku ubaguzi wa kidini ukizidi kukuwa.

Je Dini zilianza kuingia Afrika karne zipi;

Dini za Kiislamu na Ukristo zilianza kuingia Afrika muda mrefu uliopita. Ukristo uliingia Afrika kwa mara ya kwanza karne ya 1 BK (Baada ya Kristo) kupitia wamishonari na biashara na Waafrika wa Kaskazini. Ukristo uliendelea kuenea katika maeneo tofauti ya Afrika.

Uislamu ulianza kuingia Afrika katika karne ya 7 BK (Baada ya Kristo) kupitia kazi ya Muhammad na Waislamu wa kwanza. Kupitia biashara na uvumbuzi wa safari za jangwani, Uislamu ulienea kwa kasi katika maeneo mengi ya Afrika, haswa katika Afrika Kaskazini.

Je Kabla ya Dini hizi waafrika tulikuwa tunaabudu nini?

Kabla ya kuingia kwa dini za Kiislamu na Ukristo, tamaduni za Kiafrika zilikuwa na dini na imani za kiasili zilizojumuisha ibada ya miungu ya asili, roho za wafu, na nguvu za asili. Dini za Kiafrika zilitofautiana sana kutoka eneo moja hadi lingine na kati ya jamii tofauti za Kiafrika.

Mara nyingi, dini za Kiafrika zilijumuisha ibada ya miungu au roho za wakubwa wa kale, kama vile mababu au wazee wa kabila. Kwa mfano, jamii nyingi za Kiafrika ziliabudu miungu ya jua, mvua, na ardhi, kwa sababu vitu hivyo vilikuwa muhimu kwa maisha yao ya kila siku.

Dini za Kiafrika pia zilijumuisha ibada ya wazee na mababu waliokufa, kwa kuwa waliona kumbukumbu na heshima kwa wafu kama sehemu muhimu ya utamaduni wao. Imani hizi za kiasili zilikuwa sehemu ya utamaduni wa Kiafrika na zilisimulia hadithi za uumbaji, maisha, na mazishi.

Kwa hiyo, kabla ya kuingia kwa dini za nje, Waafrika walikuwa wanaabudu miungu yao ya asili na walikuwa na imani za kiasili zilizohusiana na maisha yao ya kila siku na utamaduni wao, na maombi yalikuwa yanafanya kazi.

MY TAKE: Ukitizama Dini hizi za Ukristo na Uislamu ni dini zilizoletwa tu Afrika. Walikuja na kutuambia Imani zao ni bora kuliko zetu, hivyo tuache Imani zetu tufate Imani zao. Dini hizi mbili zinaimiza katika Kusameheana, kutokuua, kutokudhuru, na zinaamini katika Kupendana. Inasikitisha sana hawa wenye dini zao wamekuja Afrika na kutuhubiria Amani lakini wao hawafuati hiyo Amani wala hayo mafundisho. Mbona wenye dini zao wenyewe Waisraeli na wapalestina wameshindwa kufuata maandiko na wanauana kama kuku, inakuaje mimi muhaya wa Bukoba ambaye hapo mwanzo nilikuwa naabudu mizimu nifuate maandiko hayo ambayo wahusika wenyewe wameshindwa kuyafuta.

Mimi kwa mtazamo wangu naona walitumia dini zao kama chambo hili kutuweka katika ukoloni miaka hiyo maana waarabu ndio walikuwa walanguzi wa watumwa kisha wanaenda kuwauzia wazungu. Hivyo walitumia mafundisho ya dini zao kutufanya kutufumba akili na uwezo ili iwe rahisi kututawala.

Mbona hatuoni ishara yoyote kutoka juu kwa muumba mwenyewe baada ya mapigano hayo, maana tunaambiwa maeneo yale ni matakatifu, hivyo kwa akili tu lazima kungetokea ishara ya kukataza mapigano, ila naona tu Aliakibar ndio nyingi huko Gaza, huku Shalom zikiwa nyingi huko Israel.
Kila mtu akiomba mwenyezi hamsaidie.

Sasa tumeona ni namna gani Dini hizi za kuletwa vile hazifanyi kazi, ni bora kurudi kwenye kuabudu Mizimu yetu ambayo hapo mwanzo tulikuwa tukiiomba, mwandishi mashuhuri wa vitabu Yericko Nyerere aliwahi kugusia hili, kwamba turudi kwenye Imani zetu za hawali, na mimi sasa naona umuhimu wake
 
Ukitafakarii sana unaona bora ufanye yako tu, hii dunia ukweli mwingi umefichwa ili mazuzu wawe wengi, Ukirudi back to objectives za kusoma history Olevel ilikuwa kujua tulipotoka, tulipo na tuendako ila it seems most of us hatukuelewa dhima ya lile somo, naambiwa kabisa dini ziliingizwa Africa ili kurahisisha utawala ila bado kuna mazuzu wanajiona waarabu na wengine wanajiona wamissionary na wanataka waconnect na asili kwa utamaduni wa watu

Samehe wakati wao kwa wao wenye dini zao wameshindwa kusameheana .

Bora waafrika turudi kwenye kuabudu Mizimu tu
 
Rudi mwenyewe, tushaijua kweli ambaye ni Yesu na yeye ametuweka huru..
Wewe na myahudi ni nani mwenye Dini yake.... myahudi mwenyewe kwenye torati anaambuwa hasiuwe, yeye kule Gaza anauwa.

Alafu unataka kujifanya mfia dini kuliko Myahudi... Hata waluokuwa wanaabudu Mizimu bado nao maombi yao yalifanya kazi... Wewe hupo leo kwa sababu miungu iliwalinda babu zako huko miaka mingi kabla ya hizi Dini.... Kwa hiyo babu yako aliyefariki karne ya 7 bila kujua ukristo yeye aliwezaje kuishi
 
Wewe na myahudi ni nani mwenye Dini yake.... myahudi mwenyewe kwenye torati anaambuwa hasiuwe, yeye kule Gaza anauwa.

Alafu unataka kujifanya mfia dini kuliko Myahudi... Hata waluokuwa wanaabudu Mizimu bado nao maombi yao yalifanya kazi... Wewe hupo leo kwa sababu miungu iliwalinda babu zako huko miaka mingi kabla ya hizi Dini.... Kwa hiyo babu yako aliyefariki karne ya 7 bila kujua ukristo yeye aliwezaje kuishi
Nina YESU anayekaa ndani yangu...

Dini hiyo ni njia tu...
 
Rejea kichwa cha habari tajwa hapo juu.

Dini ndio chanzo cha matatizo mengi Duniani. Katia Dunia ya leo raia wanakosa ushirkiano tu kwa sababu wanatofautiana Kidini, mkristo anambagua muislamu na muislamu anambagua mkristo...
Mizimu yenu ni ipi ninyi kama Waafrika?

Kwani unadhani hao Waarabu au Wazungu huu Ukristo na Uislamu ndiyo dini zaobza asili?

Unavyodhani wewe Ukristo na Uislamu ndiyo Mizimu yao?

Tatizo katika kufikiri wengi mnaanzia walipoishia wenzenu jana. Huwa hamjisumbui kujiuliza walau maswali mawili matatu kurudi nyuma, halafu ndiyo mnajiibua kuwa Championa and great thinkers...mnafanya vyema thou
 
Back
Top Bottom