kingphisher
Senior Member
- Nov 30, 2024
- 144
- 256
Wakuu, naomba msaada kwa wenye uzoefu kuhusu mada tajwa hapo juu.
Nimeona baadhi ya nafasi za ajira zinazotangazwa kupitia Ajira Portal, hasa upande wa ICT/Software Development, mfano nafasi za Systems Analysis. Kwenye baadhi ya nafasi hizo, moja ya vigezo vinavyotajwa ni mwombaji kuwa na portfolio inayoonyesha baadhi ya projects alizowahi kufanya.
Tangu nimemaliza chuo, nina takribani miaka miwili sasa mtaani, na sijawahi kuomba ajira serikalini. Kazi niliyokuwa nafanya kwenye kampuni fulani ilikuwa ya IT, lakini haikuhusisha moja kwa moja na software development.
Kadri muda ulivyokwenda, nilibadili mtazamo wangu na kuanza kujikita zaidi kwenye software development. Sababu kubwa ni kwamba kwenye kampuni niliyokuwa nafanya kazi, niliona developers wakitumia AI kama sehemu ya development tools zao ili kuharakisha kazi mbalimbali za utengenezaji wa mifumo.
Hilo lilinifanya nitambue kwamba inawezekana kujifunza programming, kuelewa development vizuri, na pia kutumia teknolojia kama AI kama nyenzo ya kusaidia katika development.
Nilitumia takribani miezi mitatu, mchana na usiku, kujifunza na kutengeneza project inayofanya kazi. Lengo langu halikuwa tu kumaliza project, bali kujenga kitu kinachoweza kufanya kazi katika mazingira halisi.
Nilianza kwa kutengeneza portfolio website yangu. Kwa upande wa development, sehemu kubwa nilifanya kwa uelewa na uwezo wangu, huku pia nikitumia AI kama development assistant. Baadaye nikatengeneza School Management System pamoja na POS (Point of Sale) System.
Kwa sasa nina portfolio website ambayo ina baadhi ya projects nilizotengeneza. Projects hizo zipo live 24/7, na pia nimeweka link ya website pamoja na GitHub account yangu kwenye CV.
Swali langu ni hili:
Kwa interview za ajira za Serikali, hasa nafasi zinazohusiana na Software Development au Systems Analysis, kuwa na projects zinazofanya kazi pamoja na portfolio nzuri kunaweza kuwa faida kubwa katika kupata kazi?
Au kinachoangaliwa zaidi ni ufaulu wa written/oral interview, bila kujali sana projects ulizonazo?
Na pia, kama interview panel itaona portfolio/GitHub yangu, kuna uwezekano wakauliza maswali moja kwa moja kuhusu architecture, database, technologies au namna nilivyotengeneza projects hizo?
Naomba mwenye uzoefu wa interview za ICT serikalini au aliyewahi kupitia mazingira haya anipe mwanga.
Asanteni wakuu.