Katika miaka ya hivi karibuni, uzazi wa watoto mapacha umeonekana kuvutia wengi huku baadhi ya wanandoa wakijaribu kutumia njia za kisasa kuhakikisha wanazaa mapacha. Lakini miongoni mwa jamii ya wasukuma huko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, uzazi wa watoto mapacha unaonekana kama laana, na watoto hao ili wakubalike katika jamii hiyo, ni lazima wazazi wao wawafanyie sherehe maalum ya kuwatakasa kwa kuchinja ng'ombe na kucheza ngoma.
Chanzo: BBC Swahili.
Bado washenzi tu pamoja na maendeleo ya teknolojiaUnajua kuwa mpaka leo kuna Wajapan na watu wengi tu waliostaarabika (per your standard) wanaabudu miti na mizimu?. Na wakitoka hapo wanakwenda kukutengenezea Sony Music System na Toyota Land Cruiser. Kwako wewe ustaarabu ni nini?
Pima akili au uelewa wako kwa staha bila unafiki. Hili la mapacha mimi nalisikia leo, lakini ni mara ngapi tunasikia kuuawa vikongwe? Au unajifurahisha mtandaoni? Na albino?BBC wana shida na watu wa huko. Na yote yanayosemwa ni uongo, hakuna ukweli hata kidogo.
Walikuwa wanamwabudu mungu wasiyemjua vemaHiyo ibada ya miti walikuwa wanaabudu lini? Na inaitwaje kwa kilugha? Unafahamu huko walikuwa wana abudu Mungu kabla hata ya kuja kwa wageni..
Nyanzara. Ama una njaa (nzala) ya kisaikolojia na kitamaduni au ni troll tu usiye na mwelekeo wala haja ya kuhojiana. Wabeja!Bado washenzi tu pamoja na maendeleo ya teknolojia
Mimi sijakuuliza habari za kufeli mitihani yako ya shule au madarasa, nakuuliza juu ya yaliyosemwa na BBC na unachotetea hapa. Mbona hao vikongwe wasiuliwe Kilimanjaro au Tanga? Au ndio kusema kuwa vikongwe wako Usukumani tu?Akili na uelewa wangu ni mkubwa, sababu sikuwahi kufeli na sasa nina develop project zangu za kisayansi na zinakaribia kukamilika. Ninavyokwambia nafahamu usukumani siyo sababu ya kabila tu bali ni nimezaliwa huko, nimekulia huko na nitakuja kuwa kiongozi wa huko hapo baadae.
Mauji ya vikongwe yalikuwepo kutokana na imani za kichawi lakini hizo siyo mila za kisukuma. Mila ni mtindo fulani wa maisha ambayo jamii imeamua kuishi, kwa hiyo hatujaamua kuishi ili kuua vikongwe au albino. Hizo ni imani za kichawi kwa baadhi ya watu, na hata albino unafahamu ni sababu gani inapelekea ya wao kuuawa.
we ngabu,kuja msukuma moja mdada aliwahi kuniambia kuwa usije ukaoa wasuka wanyantunzu akidai kuwa ni wengi wao ni wakorofi na wenye kiburi.kuna ukweli wwte kweliBasi kwetu Ntuzu hatuna hayo mambo.
Mimi ni Msukuma 110% na sijawahi kamwe kuusikia huo utamaduni.
Ni wa Wasukuma wa wapi labda?
Nyani Ngabu kweli wewe ni Msukuma unaifahamu sherehe ya wasukuma inayojulikana kama "Mabhasana"? Hiyo ndiyo sherehe anayoongelea mleta mada. Katika sherehe za namna hii, kuna vitu vya ajabu,inaruhusiwa kuongea tusi lolote unalolifahamu, viungo vya siri vyote vya mwanadam vinatamkwa kwa wazi, tendo la kujamiiana linatamkwa katika sherehe nzima. kwa ufupi usiende kwenye sherehe hizo na mzazi wako au mama mkwe. Sitanii, hii ni sherehe mbaya zaidi hapa duniani, kwa kuwa ni sherehe inayotawaliwa na matusi ya nguoni, sio kwamba watu wanatukanana wao kwa wao, ni mzaha na utani fulani wa matusi. Uliza wasukuma wa Mwanza watakwambia
Babu yangu ni Pacha,Baba yangu amefuata mapacha na mimi tumezaliwa mapacha na mdogo wangu wa kike,mashangazi zangu na dada zangu wengi tu wana mapacha,hii sherehe nishafanyiwaga,tena ziko mbili...ile mkiwa vitoto vidogo mama yenu hawezi akaenda ugenini akalala nanyi huko,mpaka mfanyiwe tambiko kidogo,zinachinjwa kondoo kulingana na jinsia yenu (kama ni wa kiume,kondoo atakua wa dume,km sivyo basi kondoo watakua jike na dume) watu wanakula.Kuna ngozi kutoka kwa wale kondoo mnavalishwa kama pete (watoto na mama yenu).Tambiko hilo likiisha basi mnaruhusa ya kulala ugenini.
Pia mtu akijifungua mapacha, kiongozi wa jadi wa kanda (Lugoye) atapiga Kalulu ili kujulishwa wanazengo wote (hii kalulu inaashiriaga majanga au mkosi,mfano ikinyesha mvua ya mawe,mtu kuzaa mtoto mfu au mtu kufa akiwa anazaa huwa wanapiga kalulu pia) hii "kalulu" huwa inapigwa afu mpiga anatamka neno "Boyo" then anataja jina la familia.
Kuzaa mapacha ilikua kama mkosi flani hivi kama alivyosema mwandishi,watoto wa mapacha tulikua tunafichwa sana tulikua tunajulikana kama "Basebu" ikiwa na maana wa "moto" ikimaanisha mapacha wanaweza kufa muda wowote na huwa wanafanyiwa matambiko sana.Kama ulisoma kitabu cha Things Fall Apart,kwenye kabila la akina Okonkwo mapacha walikua wanaitwa "Osu" na walikua dalili ya mkosi katika jamii na walikua wanatupwa porini.
Zamani usukumani mwanamke anayezaa mapacha alikua anaachwa....Natokea Bariadi,wilaya mpya ya Itilima....kwenye ukoo wetu akina saka (mtoto pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa wakati wa kuzaliwa au kufa baada ya muda mchache ni wengi sana.
Majina haya kwetu ni common
1.Kulwa-Pacha wa kwanza kutoka (mkubwa)
2.Doto - pacha wa pili kutoka (mdogo)
3.Kija- mtoto wa kwanza(kiume) kufuata mapacha
4.Hoja-Mtoto wa pili(kiume) kufuata mapacha
*Saka ni mtoto mapacha ambaye mwenzake hayupo (ashakufa) Maana ya neno SAKA ni "BAKI" Kwa hiyo SAKA ni pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa.
Kwa hiyo Nyani Ngabu wewe ni msukuma fake umeongea uongo,mimi ni mshosha ng'ombe halisi,Msukuma grade A,Mnyantuzu pure kabisa na natoka familia ya mapacha kutoka babu yangu hadi mimi.
So low. Mna nini cha kuwafanya muandamwe? Kweli ushamba haujakuisha mista mapolojekti...BBC, dhidi ya wasukuma kwani nyie ndio nani hapa duniani?Soma aya ya pili hapo juu! Nimeshakujibu.
Ndiyo tumia hii JF kuwauliza wenyewe BBC eti wana kisa gani na watu wa huko?
Ila mnyatumzu sio msukuma ana force kuwa msukuma kwanza jamaa wanatabia za kichaga hawa wakorofi pesa mbele afu katili sana kwa wanawakeNtaenda kaka hapo Bujora, lakini hakuna Msukuma wa maeneo mengine anaekubali kuwa mnyantuzu kuwa ni Msukuma, bali huwa wanawaita Wanyantuzu tu kwa nini?
KaribuSawa samahani.
Kuna waseya,wakamba,waminza,wasega..wangolo...wanyantuzu haya yote yamegawanyika kutoka na kanda unayotokaKuna wengine watashangaa humu kama kuna hilo tabaka la Waseya kama ilivyo kwa Wanyantuzu na Wakamba.
NtuzuWewe ni msukuma wa wapi? Kama salamu tu zenyewe huzijui, utawezaje kujua mila za kisukuma?
Basi kwetu Ntuzu hatuna hayo mambo.