Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Katika miaka ya hivi karibuni, uzazi wa watoto mapacha umeonekana kuvutia wengi huku baadhi ya wanandoa wakijaribu kutumia njia za kisasa kuhakikisha wanazaa mapacha. Lakini miongoni mwa jamii ya wasukuma huko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, uzazi wa watoto mapacha unaonekana kama laana, na watoto hao ili wakubalike katika jamii hiyo, ni lazima wazazi wao wawafanyie sherehe maalum ya kuwatakasa kwa kuchinja ng'ombe na kucheza ngoma.

Chanzo: BBC Swahili.


Wasukuma wa wapi hawa unaowaongelea? Ni wasukuma ama ukoo mmoja?
 
Unajua kuwa mpaka leo kuna Wajapan na watu wengi tu waliostaarabika (per your standard) wanaabudu miti na mizimu?. Na wakitoka hapo wanakwenda kukutengenezea Sony Music System na Toyota Land Cruiser. Kwako wewe ustaarabu ni nini?
Bado washenzi tu pamoja na maendeleo ya teknolojia
 
BBC wana shida na watu wa huko. Na yote yanayosemwa ni uongo, hakuna ukweli hata kidogo.
Pima akili au uelewa wako kwa staha bila unafiki. Hili la mapacha mimi nalisikia leo, lakini ni mara ngapi tunasikia kuuawa vikongwe? Au unajifurahisha mtandaoni? Na albino?
 
Akili na uelewa wangu ni mkubwa, sababu sikuwahi kufeli na sasa nina develop project zangu za kisayansi na zinakaribia kukamilika. Ninavyokwambia nafahamu usukumani siyo sababu ya kabila tu bali ni nimezaliwa huko, nimekulia huko na nitakuja kuwa kiongozi wa huko hapo baadae.

Mauji ya vikongwe yalikuwepo kutokana na imani za kichawi lakini hizo siyo mila za kisukuma. Mila ni mtindo fulani wa maisha ambayo jamii imeamua kuishi, kwa hiyo hatujaamua kuishi ili kuua vikongwe au albino. Hizo ni imani za kichawi kwa baadhi ya watu, na hata albino unafahamu ni sababu gani inapelekea ya wao kuuawa.
Mimi sijakuuliza habari za kufeli mitihani yako ya shule au madarasa, nakuuliza juu ya yaliyosemwa na BBC na unachotetea hapa. Mbona hao vikongwe wasiuliwe Kilimanjaro au Tanga? Au ndio kusema kuwa vikongwe wako Usukumani tu?

Labda wewe unaona BBC wana kisa gani na Wasukuma, eti bwana maproject?
 
Nyani Ngabu kweli wewe ni Msukuma unaifahamu sherehe ya wasukuma inayojulikana kama "Mabhasana"? Hiyo ndiyo sherehe anayoongelea mleta mada. Katika sherehe za namna hii, kuna vitu vya ajabu,inaruhusiwa kuongea tusi lolote unalolifahamu, viungo vya siri vyote vya mwanadam vinatamkwa kwa wazi, tendo la kujamiiana linatamkwa katika sherehe nzima. kwa ufupi usiende kwenye sherehe hizo na mzazi wako au mama mkwe. Sitanii, hii ni sherehe mbaya zaidi hapa duniani, kwa kuwa ni sherehe inayotawaliwa na matusi ya nguoni, sio kwamba watu wanatukanana wao kwa wao, ni mzaha na utani fulani wa matusi. Uliza wasukuma wa Mwanza watakwambia

Mimi ni Msukuma 110% na sijawahi kamwe kuusikia huo utamaduni.

Ni wa Wasukuma wa wapi labda?
 
Nyani Ngabu kweli wewe ni Msukuma unaifahamu sherehe ya wasukuma inayojulikana kama "Mabhasana"? Hiyo ndiyo sherehe anayoongelea mleta mada. Katika sherehe za namna hii, kuna vitu vya ajabu,inaruhusiwa kuongea tusi lolote unalolifahamu, viungo vya siri vyote vya mwanadam vinatamkwa kwa wazi, tendo la kujamiiana linatamkwa katika sherehe nzima. kwa ufupi usiende kwenye sherehe hizo na mzazi wako au mama mkwe. Sitanii, hii ni sherehe mbaya zaidi hapa duniani, kwa kuwa ni sherehe inayotawaliwa na matusi ya nguoni, sio kwamba watu wanatukanana wao kwa wao, ni mzaha na utani fulani wa matusi. Uliza wasukuma wa Mwanza watakwambia

Kusema sherehe hiyo ni utamaduni wa Wasukuma ni sawa na kusema vigodoro ni utamaduni wa Watanzania.
 
Babu yangu ni Pacha,Baba yangu amefuata mapacha na mimi tumezaliwa mapacha na mdogo wangu wa kike,mashangazi zangu na dada zangu wengi tu wana mapacha,hii sherehe nishafanyiwaga,tena ziko mbili...ile mkiwa vitoto vidogo mama yenu hawezi akaenda ugenini akalala nanyi huko,mpaka mfanyiwe tambiko kidogo,zinachinjwa kondoo kulingana na jinsia yenu (kama ni wa kiume,kondoo atakua wa dume,km sivyo basi kondoo watakua jike na dume) watu wanakula.Kuna ngozi kutoka kwa wale kondoo mnavalishwa kama pete (watoto na mama yenu).Tambiko hilo likiisha basi mnaruhusa ya kulala ugenini.
Pia mtu akijifungua mapacha, kiongozi wa jadi wa kanda (Lugoye) atapiga Kalulu ili kujulishwa wanazengo wote (hii kalulu inaashiriaga majanga au mkosi,mfano ikinyesha mvua ya mawe,mtu kuzaa mtoto mfu au mtu kufa akiwa anazaa huwa wanapiga kalulu pia) hii "kalulu" huwa inapigwa afu mpiga anatamka neno "Boyo" then anataja jina la familia.
Kuzaa mapacha ilikua kama mkosi flani hivi kama alivyosema mwandishi,watoto wa mapacha tulikua tunafichwa sana tulikua tunajulikana kama "Basebu" ikiwa na maana wa "moto" ikimaanisha mapacha wanaweza kufa muda wowote na huwa wanafanyiwa matambiko sana.Kama ulisoma kitabu cha Things Fall Apart,kwenye kabila la akina Okonkwo mapacha walikua wanaitwa "Osu" na walikua dalili ya mkosi katika jamii na walikua wanatupwa porini.
Zamani usukumani mwanamke anayezaa mapacha alikua anaachwa....Natokea Bariadi,wilaya mpya ya Itilima....kwenye ukoo wetu akina saka (mtoto pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa wakati wa kuzaliwa au kufa baada ya muda mchache ni wengi sana.
Majina haya kwetu ni common
1.Kulwa-Pacha wa kwanza kutoka (mkubwa)
2.Doto - pacha wa pili kutoka (mdogo)
3.Kija- mtoto wa kwanza(kiume) kufuata mapacha
4.Hoja-Mtoto wa pili(kiume) kufuata mapacha
*Saka ni mtoto mapacha ambaye mwenzake hayupo (ashakufa) Maana ya neno SAKA ni "BAKI" Kwa hiyo SAKA ni pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa.
Kwa hiyo Nyani Ngabu wewe ni msukuma fake umeongea uongo,mimi ni mshosha ng'ombe halisi,Msukuma grade A,Mnyantuzu pure kabisa na natoka familia ya mapacha kutoka babu yangu hadi mimi.


Mkuu ulichosema sio mila ya Wanyantuzu wa bariadi bali ni wanyamweli kutoka kahama. Alivyosema Ngabu ndio sahihi hii mila haipo Bariadi. Tumekulia huko temelelewa hivyo. Mwandishi upo sahihi kwa wasukuma wa Kahama na Kwimba lakini sio Bariadi. Nimekuja kishuhudia hii mila mara baada ya dada yangu kuolewa na wasukuma wa kutoka Kahama ndio nikasikia kwa mara ya kwanza lakini sio wasukuma grade A (wanyantunzu).
 
Soma aya ya pili hapo juu! Nimeshakujibu.

Ndiyo tumia hii JF kuwauliza wenyewe BBC eti wana kisa gani na watu wa huko?
So low. Mna nini cha kuwafanya muandamwe? Kweli ushamba haujakuisha mista mapolojekti...BBC, dhidi ya wasukuma kwani nyie ndio nani hapa duniani?
 
Ntaenda kaka hapo Bujora, lakini hakuna Msukuma wa maeneo mengine anaekubali kuwa mnyantuzu kuwa ni Msukuma, bali huwa wanawaita Wanyantuzu tu kwa nini?
Ila mnyatumzu sio msukuma ana force kuwa msukuma kwanza jamaa wanatabia za kichaga hawa wakorofi pesa mbele afu katili sana kwa wanawake
 
Ni lazima ufanyiwe matambiko,,, na hasa yapo shinyanga na nzega tabora,, wao huita ukango,,, hata modern society naona mnawapeleka mapacha kanisani na kama mmoja hamuwapeleki... Hizo ngoma zipo na kwa kwa mwanza hazipo
 
Wasukuma bado mnafuga fisi ?
Ila hongereni mauaji ya albino yamepungua.
 
Siku hizi BBC haina tofauti na magazeti ya udaku ama blog za udaku zinazoweka picha za utupu na kumtaka mtu afungue link husika ili kuona picha za utupu zaid na udaku mwingine.
Sijui akaunti ya BBC fb, na instagram zimehakiwa au ndo ukanjanja wao tu siku hizi.
 
Back
Top Bottom