Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Mapacha ni neema katika familia kwa mujibu wa tamaduni za kisukuma.

Na Sukuma maana yake ni kaskazini mwa tabora (nhobola)
Na tabora inaitwa dakama.

Kuhusu usukuma na unyamwezi umeletwa tu na wageni ili kutugawa maana sisi tunanguvu sana.
 
Kuna kitu kinaitwa BHUKANGO,....!!onene ekaya habhotemi bhong`wa Limihagati
 
Kwa Wasukuma wa jamii ya Wanyantuzu hizi mila hazipo, ila kwa Wasukuma ambao wanyantuzu huwaitwa Banang'weli huo utamaduni wanao, tena kwao neno mabasa haimanishi tu mapacha kwa maana ya kujifungua watoto wawili kwa mimba moja, wao humanisha kama mkosi. Hii ni kwa sababu wao wana mabasa ya aina mbili, Mama akijifungua watoto wawili huita mabasa na hufanya tambiko, mtoto akitanguliza miguu pia huita mabasa tena wanasema ni mabasa matale na wanafanya tambiko.
 
Kugeukia Ukristo na Uislamu ndiyo KUSTAARABIKA? Waafrika yaani dah! Ikiwezekana kwa kweli wazungu warudi tu watutawale tena kwa sababu hakuna namna.
Huwezi kuwa unaabudu miti au mizimu ukasema umestaarabika. Huo ndoo ukweli hata kama ni mchungu
 
Usidanganye watu wewe, vitu Vingi umetumia nadharia

Kwa mfano
1.ngoma wanayochezewa Mapacha inaitwa "MABASANA"

2.Katika utamaduni Wa kisukuma Hakuna jina SAKA ila aliyefiwa na pacha wake tunamwita "MASAGA"au"SAGA" kwa kifupi.

3."KALULU"ni vigelegele hasa vya Furaha wapigavyo kina mama kwenye matukio Mhimu Kama vile arusi, posa

4.BHOYO ni mjumuiko Wa ubalozi au mtaa ambapo msiba umetokea.


NAKARIBISHA. MASWALI!!!!!!
 
Nimekuuliza ulishasikia wasukuma wanasalimiana "enkamba" au "iseya"? Unakuta hata siyo msukuma, kumbe ni ujuaji wa JF tu.
Ujuaji wa JF kivipi?, wewe ndio unajiona ndio msukuma samahani Mnyantuzu wa mwisho kabisa hakuna zaidi yako?

Sijawahi sikia hizo salam, nini tofauti ya Wasukuma na Wanyantuzu? Na nini ufanano wao?
 
Hivi una miaka mingapi wewe? Kuna Wakamba huwa wanasalimiana "enkamba" na kuna Waiseya huwa wanasalimiana "iseya" kama kutambulisha tabaka walipotoka. Hukuwahi kusikia hizi salamu?
Hiyo kusalimiana naamini unajua inaitwa Lwèmbo na ukifuatilia hizi lwèmbo zinatumia majina ya wanawake, Majina haya ni wake wa watemi wa utemi fulani, mfano kama mke wa mtemi wa Ntuzu alikuwa anaitwa Minza basi watu wote waliotoka utemi wa Ntuzu watakuwa babinza na watakuwa wanasalimia éminza.
 
Sahihisho :mtoto aliyezaliwa katanguliza miguu hatuiti mabasa ila huitwa "Kashinje "


Karibu Kwa maswali
 
Wasukuma wanamatabaka mengi mno. Tukiorodhesha hapa yanafika mia.
Na hayo yametokana na kuwa kuna Makabila ambayo hayakuwa Wasukuma ila wameingia ndani ya Usukuma kwa kuitumia lugha ya kisukuma na kuchukua baadhi ya mila za Kisukuma
 
Na hayo yametokana na kuwa kuna Makabila ambayo hayakuwa Wasukuma ila wameingia ndani ya Usukuma kwa kuitumia lugha ya kisukuma na kuchukua baadhi ya mila za Kisukuma
Wanyantuzu cyo wasukuma halisi ni mchanganyiko wa wasukuma na wanyiramba.
 
Ndugu upo sahihi kabisa. Kuna watu wanajifanya wanajua sana issue za kisukuma kwa kutumia nadharia bila kufanya uchunguzi
 
wasukuma tambiko kila kabila wanalo. kwa mapacha lazima wafanye tambiko na huku nkwetu shinyanga hata mtu akijifungua mtto katanguliza matako tunafanya tambiko ndio mila zetu msidaganye watu
 
Huwezi kuwa unaabudu miti au mizimu ukasema umestaarabika. Huo ndoo ukweli hata kama ni mchungu
Unajua kuwa mpaka leo kuna Wajapan na watu wengi tu waliostaarabika (per your standard) wanaabudu miti na mizimu?. Na wakitoka hapo wanakwenda kukutengenezea Sony Music System na Toyota Land Cruiser. Kwako wewe ustaarabu ni nini?
 
Sahihisho :mtoto aliyezaliwa katanguliza miguu hatuiti mabasa ila huitwa "Kashinje "


Karibu Kwa maswali
Sio jina lake, ile hali ya kutanguliza miguu ndo mabasa yenyewe. Narudia tena sikumaanisha kwamba jina lake ni mabasa ila mabasa ni kile kitendo cha kutanguliza miguu.
 
Ndugu upo sahihi kabisa. Kuna watu wanajifanya wanajua sana issue za kisukuma kwa kutumia nadharia bila kufanya uchunguzi
Yaan mtu anaibuka na nadharia zake ili aonekane bingwa kumbe hamna kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…