Wasukuma na ulaji wa korodani za ng'ombe na kichuri

Usikariri. Wote wanaokula ndizi ni Wahaya, makande ni Wapare au mtori ni Wachaga pekee?
Kuna kujifunza kula ila siyo asili yao. Msukuma na kichuri wapi na wapi mkuu. Hapo umedanganya mkuu.
Kichuri lbd ukuryani ila siyo kwa wasukuma. Hao unawaowazungumzia ni washashi na wakurya. Ngosha ale kichuri? Ni sawa na masai ale mlenda au mbute
Karibu usukumani ujionee. Huku hatujui hata kichuri kinaandaliwaje. Kuhusu koroni hata za mbuzi tunakula hapo sibishi.
 
Wakazi wa Mwanza hapa mjini ni full mchanganyiko wa makabila ya kanda ya ziwa tena huezi amini wasukuma hapa mjini hawafiki hata robo ya wakazi wake hivyo hii imetufanya tuingiliane sana katika vyakula. Kichuri kinauzwa na wachoma nyama wa makabila ya huku na kinaliwa pia hata na makabila mengine ya huku. Mfano hapa Nyamagana wasukuma wapo wapo Igoma na Buhongwa sehemu zingine wamejaa waha, wahaya, wajaruo na washashi ambao nyinyi mnawaita wakurya
 
Kuna kujifunza kula ila siyo asili yao. Msukuma na kichuri wapi na wapi mkuu. Hapo umedanganya mkuu.
Kichuri lbd ukuryani ila siyo kwa wasukuma. Hao unawaowazungumzia ni washashi na wakurya. Ngosha ale kichuri? Ni sawa na masai ale mlenda au mbute
Karibu usukumani ujionee. Huku hatujui hata kichuri kinaandaliwaje. Kuhusu koroni hata za mbuzi tunakula hapo sibishi.
Hajaongelea "kujifunza kula" bali "kula", huwezi ukaniambia Msukuma wa Mwanza anayekula ndizi kila siku kuwa anajifunza kula.
 
Hajaongelea "kujifunza kula" bali "kula", huwezi ukaniambia Msukuma wa Mwanza anayekula ndizi kila siku kuwa anajifunza kula.

Mh!
Mkuu msukuma anayekula ndizi kila siku? Huyo hayupo. Atakuwa amekondeana sana. Huyo ni mhaya wala si msukuma. Unawajua wasukuma lkn? Msukuma pure huwa hali chakula cha kujilamba lamba halafu msosi wake ni mgumu. Kwa ndizi sidhan km anashiba.
Njoo huku usukumani mkuu, hao unawazungumzia ni wasukuma fake. Wasukuma tunakula kweli huwa hatubeep. Msukuma na ndizi wapi wapi mkuu. Ugali, wali, mbute, mihogo, makande, n.k na ugali uwe wa kutosha kweli.
Hapo umedanganya mkuu. Ndizi tu lbd useme mchanganyiko na mihogo hapo nitakuelewa ila ndizi pekee ni tusi kwa msukuma.
 
Kichuri sio mavi ya Ng'ombe.

Ile ni zile nyasi ambazo mnyama kama mbuzi au Ng'ombe anakua amekula ziko kwenye utumbo mwembamba zikimeng'enywa kabla hazijahamia utumbo mpana kua mavi.

So ni sawa na ile wanaita work in progress, sio nyasi na sio mavi. So bado inakua ina virutubisho vyote vya yale majani, ndio inatolewa inamiksiwq na nyongo.

Makabila mengi wanakula hiyo kitu sio wa mwanza tu, na sio wasukuma wanakula hiyo, hiyo ni ya jamii ya wakurya wote wa mkoa wa mara.

Kichuli, ile ni kama appetiser, unaweza kula mbuzi nzima, achana na kichuri.
Umeua
 
Aisee korodani za mbuzi au ng'ombe ni tamu sana..wenyewe tunaziita Hashua..jaribu then ulete mrejesho.
 
Kuhusu kichuri na mavi ya ng'ombe umewasingizia wasukuma. Hayo mengine nakuunga mkono.
 
Kichuri kwa asilimia kubwa huwa ni kwa sisi wakurya mkuu sio wasukuma na ukiona msukuma anakula kichuri huyo mwanafunzi.

Ukija huku vijijini kwetu (ukuryani) nyantira, kimusi, nyamongo, bwirege, keisangora etc, etc siku za tohara kutahiriwa bila ganzi ni kama pie yaani 22/7 (principle) ndio hapo utagundua kwa nini wakurya wanapenda sana kichuri.

Wasukuma kichuri hawezi mziki wake kwa mfano sasa hivi ndio useme eti unampa baba Jesca kichuri sio ndio utamharibu kichwa kabisa.
 
Mie msukuma kiukweli kichuri hatukijui kabisa ila nishawahi kukila kikanishinda kabisa kuna rafiki yangu wambura alikileta kutoka nyumbani kwao serengeti wakati tunafungua Shule pale musoma tech.
 
Mimi mtu wa pwani ndio kwanza nayasikia leo. Kuna mishkaki inachomwa barabarani mdogo midogo hivi.naipenda kuna mtu akaniambia zile nyama ni matiti ya ng'ombe.sijui ni kweli Mimi naziona ni tamu
 
Mimi mtu wa pwani ndio kwanza nayasikia leo. Kuna mishkaki inachomwa barabarani mdogo midogo hivi.naipenda kuna mtu akaniambia zile nyama ni matiti ya ng'ombe.sijui ni kweli Mimi naziona ni tamu
Kweli mkuu ni matiti ya ng'ombe ndo mishikaki yetu kanda ya ziwa huku
 
Wakurya ndyo walaji wasukuma hapo umetudanganya Mkuu

Alfu korodani kwani ndyo kichuri?
 
Nashindwa kuumuunga mkono mleta uzi kwa asilimia nyingi!
Enewei Mwanza ni jiji labda sehemu anazotembelea yeye ndio kuna hizo mambo, ila sasa hapo ametaja Buwelu na ndio ninakoishi sijawahi kuona hayo zaidi ya vichwa vya kuku na miguu yake ndio naona wakina mama wanakaanga na kuuza pale Centre!.
anhaa kumbe aisee
 
Back
Top Bottom