Sigara Kali
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 3,623
- 8,428
Ukizunguka mitaa mbalimbali hapa jijini Mwanza hasa mida ya jioni kuanzia mjini kati, Igoma, Buswelu, National na mitaa mingine mingi basi utakutana na moshi mwingi unaofuka kwenye majiko watu wakiwa busy kuchoma mishikaki ya moyo, maini, korodani, maziwa na maviungo mengine ya ng'ombe.
Kanda ya ziwa hasa Mwanza hakuna kiungo cha ng'ombe kinachotupwa, labda pembe na kwato tu. Huku kuna kitu kinaitwa kichuri, ni mchanganyiko wa mavi ya ng'ombe na nyongo. Wenyeji wanakula nyama choma ugali mwekundu wanashushia na kichuri yaani mavi na nyongo.
Ukitaka mishikaki ya kila kitu basi huku inapatikana, korodani, maini, moyo, utumbo, maziwa na madude mengine.
Kuishi Mwanza raha sana.