Wasukuma hili neno maarufu la NYEGEZI mlilitoa wapi au lilitokana na nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Karibia maana halisi na majina ya maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania tayari nimeshapata ' Kiini ' chake ILA mpaka hii leo naandika huu ' uzi ' sijapata maana halisi ya hili neno la eneo maarufu sana huko Mkoani Mwanza la ' NYEGEZI '.

Najua humu JF tuna Ndugu zetu ' Wasukuma ' wengi sana hivyo si vibaya nanyi ' mkatiririka ' kama siyo ' kuserereka ' kabisa kutuambia hili neno la ' NYEGEZI ' mlilitoa wapi au lilitokana na nini au tukio / jambo gani.

Nitashukuru nikielimishwa kuhusu hili neno ' NYEGEZI '.

Nawasilisha.
 
Jina halisi kwa kisukuma ni N' NEGEJI hilo NYEGEZI lilitokana na kushindwa kutamka kwa wasio wasukuma, kama ilivyo DODOMA badala ya IDODOMYA.
Nitarudi baadae kutoa maana yake.
 
Back
Top Bottom