Wastaafu wawe wanaandaliwa kisaikojia kabla ya kukabidhiwa mafao

Huwa sielewi kabisa hesabu za mafao zinapigwa vipi. Kwa kanuni ambazo mifuko inatutangazia haiwezekani kipato cha laki nne unusu kikazaa milioni 60 hata ungefanya kazi miaka 50!
We unachangia na serikali inakuchangia mzee. Kuna uzi ulidadavua hilo suala humu
 
Kuna wale wazee aka wabishi kuzeeka,wako tayari wafie kwenye vinena aka vipochi manyonya.Nawafahamu wawili mmoja mzee wa bandari kastaafu na mwingine alikuwa UDSM alafu wote walikuwa marafiki walivyopata mafao waliondoka home kabisa na kuhamia kwenye nyumba ndogo baada ya pesa kuisha wakarudi kwa wake zao na korodani zao.


Wastaafu wengi huumizwa na mafao ambayo yalilengwa kuwasaidia. Kuna mmoja alipata milioni 200, wapambe walimshauri awekeze kwenye uchimbaji mdogo wa dhahabu. Alikaa huko miezi 18. Amerudi nyumbani hana kitu bahati yake mke ni mhangaikaji ana mgahawa.

Wahanga wa matukio haya ni wengi sana. Unamkuta mfanyakazi alikua anapokea laki nne na nusu kwa mwezi ghafla anamiliki milioni 60 benki. Kuna ambao wana malengo. Alikopa huko nyuma na kununua kiwanja na kujenga nyumba ya nyuma ili aachane na kulipa kodi. Alipanga mafao ndiyo ajenge nyumba ya mbele.

Ninachoona mifuko ya jamii iajiri wataalamu wa saikolojia na pia washauri wa uwekezaji. Ile wiki msataafu anayokabidhiwia pesa zake aelewe kuwa ana pesa lakini pesa ni liquid asset na ikishamwagika haizoleki. Apewe pia mawazo katika uwekezaji sahihi kama atapenda.
 
Fixed Deposit haina faida kama una hela ya kitoto hizo za below 100M...Wanaoinjoy hio ni wenye 400M plus!
Mkuu heshima kwako. Nifanyie wepesi kwa kikokotoo cha fixed deposit. Tuseme kwa mfano ukaweka million 500 fixed deposit faida yake kwa mwezi na mwaka unapata ngapi?

Natanguliza Shukrani zangu za dhati kabisa
 
We unachangia na serikali inakuchangia mzee. Kuna uzi ulidadavua hilo suala humu
I know that much.

Wewe 5% na serikali 15%, public sector

Wewe 10% na mwajiri 10%, private sector

Jumla 20% of gross income inachangiwa

Kwa hiyo mshahara wa laki 4 unusu inakwenda kwenye mfuko jumla 90,000/=, ambayo ni 20%.

Hata miaka mia ya utumishi hufikishi milioni 200 ya pensheni ya mkupuo.

Sijui huwa mnapiga hesabu gani
 
Uoga wa maisha ndio unawafanya watumishi na wastaafu wengi kupagawa na pesa ndogo za kiinua mgongo.
 
Kuna Mwalimu mwaka jana/juzi aliuziwa fuso likiwa njiani kupeleka cargo Mwanza kufika tu Mwanza jamaa wakasepa na hela akaja dreva akasema anaenda kuosha wamsubirie bar walate document original ndio ntoleee hiyo!
Baadae akaenda polisi kuja kukamatwa hawana hata senti Noma sana!
 
Wastaafu wanawindwa sana kama sio wezi wa mitandao basi mama anaungana na watoto kumshugulikia baba ( kama mstaafu ni baba) ,pia kuna Wanawake hata huku mijini wana namba za simu za wastaafu na wanawaibia hasa!!! Yani dawa ni moja ukistaafu hama ulipopazoea badili lini kabisa
 
Back
Top Bottom