Dibo10
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,298
- 1,563
Wiki iliyopita nikiwa safarini nilibahatika kukaa na mzee mmoja,alionekana kukosa uchangamfu huku mawazo yakiwa wazi yameshamiri ktk paji la uso wake, Baada ya kufahamiana na kuzungumza mawili matatu,taratibu tukaanza kushirikishana ktk mambo mbalimbali na mwishoni kabisa aliamua kuutema mwiba uliomkaba kooni. Kilichokuwa kinamsonomesha mzee wa watu ni uchache wa fao lake la kustaafu.Alianiambia hivi ndugu milioni chini ya 50 za mafao atazifanyia nini baada ya kulitumikia Taifa kwa zaidi ya miongo mitatu.
Picha ya yule mzee bado ipo kichwani mwangu, kwa wenzetu wakati wa kustaafu ni wakati wa kula matunda lakini hapa kwetu imekuwa kinyume. Baada ya Kuunganishwa kwa mifuko na kutungwa sheria mpya ya kusimamia tasnia ya hifadhi ya jamii, kanuni za ukokotozi nazo zilifanyiwa mabadiliko makubwa sana.Cha ajabu vyama vya wafanyakazi kazi vimekaa kimya kuhusu jambo hili nyeti sana.
Mamlaka ya kusimamia mifuko ya hifadhi ambayo naskia imebaki kuwa idara iko wapi ktk kuhakikisha mifuko inafanya kazi kwa ufanisi na kuwaongezea wanachama wake mafao badala ya kuyapunguza.?
Tatizo la hii mifuko ni kufanya uwekezaji usio na tija. Wao wanachojua ni kujenga majengo marefu, wengine wamewekeza mpka kwenye madaraja. Wala hauhitaji kuwa mtalaam wa fedha kujua huu ni uwekezaji usio na tija kwa wenye fedha zao ( Wastaafu). Wenyewe wanasema ujenzi wa majengo unaongezea thamani mfuko. Thamani ipi wakati wenye fedha zao wanalalamika mafao kiduchu huku wafanyakazi wa mfuko hasa top management wakiwa wanaogelea ktk ukwasi wa kutisha. Madg ktk mifuko na madf ni watu wasioshikika kila mradi lazima wawe na percent zao na huu ni utaratibu wa kawaida kabisa.
Ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua ya kudhibiti namna mifuko hii inavyofanya uwekezaji wake. Kwa baadhi ya nchi majirani kuna taasis maalum za uwekezaji zinaundwa zikiwa zimesheheni wabobezi wa uwekezaji ,wao ndio wanapewa dhamana za kuwekeza pesa za mifuko ya hifadhi. Leo mfano hai DG wa nssf ni mtu wa law, mtu kama huyu akikosa washauri wazuri chini yake usitarajie mawazo mbadala ya uwekezaji zaidi ya majengo.
Sasa ni wakati wa serikali kupora mamlaka ya uwekezaji kutoka kwa kwa hii mifuko na ziundwe taasis za kufanya kazi kwa niaba ya mifuko vinginevyo kila siku zitakuwa zinatafutwa sababu za kupunguza mafao badala ya kongeza.
Na mwisho serikali ichochee uanzishwaji wa mifuko binafsi ya hifadhi ya jamii. Nina hakika hii itaongeza ushindani na ufanisi ktk utoaji huduma.