Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,587
- 215,179
Wastaafu wengi huumizwa na mafao ambayo yalilengwa kuwasaidia. Kuna mmoja alipata milioni 200, wapambe walimshauri awekeze kwenye uchimbaji mdogo wa dhahabu. Alikaa huko miezi 18. Amerudi nyumbani hana kitu bahati yake mke ni mhangaikaji ana mgahawa.
Wahanga wa matukio haya ni wengi sana. Unamkuta mfanyakazi alikua anapokea laki nne na nusu kwa mwezi ghafla anamiliki milioni 60 benki. Kuna ambao wana malengo. Alikopa huko nyuma na kununua kiwanja na kujenga nyumba ya nyuma ili aachane na kulipa kodi. Alipanga mafao ndiyo ajenge nyumba ya mbele.
Ninachoona mifuko ya jamii iajiri wataalamu wa saikolojia na pia washauri wa uwekezaji. Ile wiki msataafu anayokabidhiwia pesa zake aelewe kuwa ana pesa lakini pesa ni liquid asset na ikishamwagika haizoleki. Apewe pia mawazo katika uwekezaji sahihi kama atapenda.