haishangazi
Wasira ni mtu makini sana, ametoa ufafanuzi mzuri sana jana kwenye kipindi cha dakika 45, imeonekana sasa Serikali kupitia Mhe. Wassira imetoa hoja mbadala dhidi ya Muungano wa Vyama vya Siasa vinavyopinga muswada huu kusainiwa na Rais, nilidhani kama vijana makini na tunaojiita Wazalendo kumuunga mkono Wassira kwa hoja hii ili tudumishe umoja na mshikamano tuliozoea hapa Tanznia.
Kama hata ushauri mzuri, na Ufafanuzi wa Kiungwana ni Makosa kwenu nyie Vijana, sasa lengo ni kutafuta Maridhiano au lengo ni kuigeuza Tanznia kuwa Kisiwa cha kumwaga damu kama yanayoendelea Kenya?
Upinzani sio fujo na vita, Wassira kaonyesha njia fuateni na muache matusi na kebehi.
Wiki tatu zijazo ni cdm then zingine cuf
Mkuu akuna anayeyapinga mawazo yako. Ila huoni igekuwa vizuri tusikilize na upande wa pili ufafanuzi wao ili wananchi tuweze kuwa majaji bora na tutowe hukumu stahili?
Wasira ni kiboko yenu ukiona chadema wanalia ujue amewaumiza
Wassira anatesa sana mioyo yenu, nadhani kwa hoja ya jana ule muungano sasa jahazi limetoboka.Haishangazi
CDM hawana uwezo wa kujenga hoja. wao wanachokiweza ni maandamano tu
Pole sana ndugu yangu.
Naona hawa watendaji wa Serikali wameshindwa kutatua tatizo lililotokea Bungeni, walishindwa wao kuzungumzia mswada uliokuwa mbele yao wakaanza kutukana wenzao.
Mswada ukapitishwa kwa idadi inayokiuka kanuni za Bunge yaani theruthi mbili, baada ya kusutwa na wananchi wanatumia kipindi kujisafisha.
Pia na Mtangazaji / Watangazaji wanashindwa kuwa na maswali yahusuyo changamoto za nchi wanajikuta wakiruhusu mambo yasiyo na mashiko.
Wassira alikuwa TBC Jumamosi Live, Jumatatu ITV Live suala hilohilo.
Tunataka maisha bora kwa kila Mtanzania siyo kutuletea longolongo kwenye vipindi vya LUNINGA/
kwani kuna anayewazuia kwenda? Viongozi wengi wa CHADEMA wanaogopa sana maswali ya waandishi wa habari na watangazaji. wamezoea press conference ambazo hazina maswali
mimi huwa hata siangalii hilo likipindi linachefua
Mkuu akuna anayeyapinga mawazo yako. Ila huoni igekuwa vizuri tusikilize na upande wa pili ufafanuzi wao ili wananchi tuweze kuwa majaji bora na tutowe hukumu stahili?
Ni kweli mkuu.
Ila kinachonitatiza ni kwanini ITV ikubali kutumiwa na hawa watu hatari kwa afya ya Taifa letu?
kwani kuna anayewazuia kwenda? Viongozi wengi wa CHADEMA wanaogopa sana maswali ya waandishi wa habari na watangazaji. wamezoea press conference ambazo hazina maswali