Wassira: CHADEMA kufa ni Ngumu

Kuna watu wengine wakiongea unaogopa hata kusikiliza, sawa na sur.............yake
 
Amekwisha huyo, hata wanaomsikiliza lazima wanakasoro kama zake
 

Kumbe sasa akili zimeanza kuwaingia vichwani. Nadhani hii kauli imekuja baada ya kichapo cha 4-0 jijini Arusha ambako yeye (wasira) ni mlezi wa ccm mkoa wa Arusha na alipiga kambi huko lakini wameambulia aibu ya mwaka. Na atambue kwamba Chadema haitakufa pamoja na mipango yote miovu wanayoipangia hadi 2015 inachukua nchi na wao wanabaki kuwa watazamaji.
 

Mmmh mkuu umeongea points tupu ila maccm yamevaa miwani ya mbao, pia tendwa anatumika kama remote control. Sasa ni kweli wajaribu kuifuta chadema waone kazi..nchi haitatawalika kama alivyosema dr slaa...japo maccm yanajifanya hayaelewi dr.slaa alimaabisha nini kusema nchi haitatawalika..nikutokana na upuuuzi wao mfano wanavyotishia kuifuta chadema hebu wajaribu waone tutakachowafanya..ohooo chezea nguvu ya umma wewe!
 
Sifa za Wasira ni adhimu miongoni mwa Wagombea urais kupitia CCM na hata Dr.Slaa anajua kibarua kitakuwa kigumu kwa upande wa CHADEMA.
Wewe ni nani kuliko Lowasa anaeogopa?
We ni nani kuliko Dr.Slaa anayehofia ?

weka mezani hizo unazoita 'sifa za wassira' ili tuzipime na kuona kweli zina mashiko tukilinganisha na potential candidates wengine ndani na nje ya ccm
 
ccm itakufa kwa kujaribu kukiua chadema, take it from me

Uko sahihi kabisa. Niliwahi kusema na nitaendelea kusema...tafsiri ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa kwa ccm ni 'kudhibiti' au 'kuua' vyama vya upinzani kwa nguvu zake zote. Mzee Mkapa alifanikiwa sana katika hili na kilichofuata ni ccm kubweteka na kuendelea kuamini kuwa njia hiyo ndiyo njia pekee ya kuifanya ccm iendelee kushika hatamu za uongozi. Tulitegemea ziara ya sekretariati ya CCM kule China itakuwa imepata fursa ya kijifunza mbinu mpya, lakini mwenendo wa kampeni za hivi karibuni za ARS na kwingineko ulikofanyika uchaguzi wa madiwani hazijaonyesha mabadiliko yoyote. Ni mbinu zile zile ambazo wananchi wameshazichoka!

Matokeo yake sasa hakuna juhudi za makusudi zinafanywa na ccm kueneza itikadi na sera zake na kuingiza wanachama wapya hasa vijana.Ukifuatilia mkutano wa ndani au wa nje wowote wa ccm, press conference, press release n.k. utashangaa kuona vyama vya upinzani hususani CDM kimetajwa mara nyingi na viongozi wa ccm kuliko CCM yenyewe. Na pale ambapo wamejaribu kufanya, wameishia ama kuvisema vyama vya upinzani na sio kueleza sera za ccm na namna ambavyo zinasaidia kutatua kero za wananchi. Waliviita kuwa ni 'vyama vya msimu' uchaguzi ukiisha vitatoweka, sasa ni karibu miaka 3 tangu uchaguzi mkuu ufanyike, lakini bado viko ulingoni na vinawanyanyasa kweli kweli.
 
labda waanzishe ccj inaweza kushindana na cdm lakin chama cha chukua chako mapema itakua ngumu
 

Kimsingi ccm hawajaweza kujifunza kitu kimoja kwamba '' huwezi kutumia mabavu siku zote ukahimili moto wa mabadiliko uliopo kwenye mioyo ya watu''

Unaweza kutawala watu kwa ufanisi kama mioyo yao inakubaliana kwa asilimia kubwa na mfumo wako. Mapinduzi ya nchi huanzishwa na uchovu wa mabavu ulioendeshwa kwa muda mrefu. Psychology ya watu ni kwamba huwa wana limits za kuhimili upuuzi, na kama ukitake it for granted kwamba hiyo tabia ni endelevu, utajishtukia siku moto unawaka na huwezi kuuzima maana ulikuwa unachochewa chini kwa chini kwa muda mrefu.

CCm kuweni makini, kama watu wamewapa ustaarabu kwa muda wote huo mliowatawala jaribuni kuwaheshimu otherwise msije kujutia yaliyowakuta kina Charles Tyler.
 

Hivi wakikifuta hakiwezi kuanzishwa kingine? Watatumia ule mtindo wa NBC ilipokabidhiwa kwa wanunuzi from S. Africa. Ofisi zote pamoja na uongozi wa CHADEMA itakayofutwa utaamia chama hicho kipya....Tena nashauri kiitwe CHADEMA 2.0
 

The Invincible,Robot na Mods wote ushauri wangu uliwafikia au mnafurahia hali hii.
Pata picha angewekwa Slaa kafananishwa na Nguruwe, hapa jukwaani Thread hiyo ingekuwa Hai?
Vp kuhusu Ban, angepona mtu huyo?
JF is a CDM wing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…