Wassira: CHADEMA kufa ni Ngumu

Mkuu siasa ni uungwana hasw ahizi zenye mlengo wa Kidemokrasia...

Kumbuka mtaji mkubwa wa Vyama vya Siasa ni watu na hao ndio huonesha dira nzima ya uelekeo wa chama fulani...

Kuihujumu Chadema na kutaka kuipoteza kwenye ramani ya siasa hiyo haimaanishi kuwa watu pia watatokomezwa...

Siku zote huwa naandika hapa jamvini, njia pekee CCM aliyobakia nayo ili kuvitokomeza vyama vya upinzani ni kuhakikisha wanaikwamua hii nchi kutoka kwenye ufukara na kutekeleza sera zao ipasavyo...

Historia ya siasa inaonesha wazi kabisa, jinsi CCM wanavyohangaika kuviua vyama vya upinzani ndivyo ambavyo vyama hivyo vinazidi kuchipua na kupendwa na wengi...

Walianza NCCR enzi za Mrema wakaichachafya CCM kwa kiasi, baadaye wakaja CUF hamasa ikaongezeka zaidi na tukaanza kuona hadi idadi ya wabunge inaongezeka...sasa imekuja Chadema na imekuwa tishio zaidi ya hao waliotangulia...ni matarajio yangu kuwa hata hawa Chadema wakidumazwa basi watakaofuata watakua hatari zaidi ya wote waliopita.

 
mkuu dosama, nasita kuyaamini maneno haya hata kama umeweka chanzo, kwa maana ni maneno ambayo siamini kama yanaweza kutamkwa na binadamu mwenye kuliona jua likichomoza asubuhi na kuzama jioni!
Kama kweli kayatamka basi kuanzia leo nanullify kila kitu nilichowahi kukisikia kutoka kwake na sitakaa nimsikilize tena!
 
Atatangulia yeye maana CHADEMA ni mpango wa Mungu.Matamanio ya Ibilisi hayawezi kutimia
 
Kumbe? Yale yale ya Godfrey Zambi, ya kugawa mkoa wwa Mbeya ili awe na influence mkoa mpya, baada ya kukataliwa hapo awali.

Ni wiki hii tu, tanroad wapepandisha hadhi barabara inayoelekea huko kwenye ngome yake. Balili hadi Nyamatoke. hii ni baada ya kuahidi maji kwa miongo kadhaa na kuhadaa wakazi wa bunda!
 
Huyu Mzee Tunasali naye Kanisani Magomeni Mwembechai lakini hana busara hata neno la Mungu sidhani kama linaingia akilini mwake vizuri.
 
Nadhani ndiye mwenye umri mkubwa kuliko wote aliebaki, wenzake waliamua kupumzika. aking'ang'ania atatoka kwa aibu itakayompelekea kufa kwa shinikizo la damu.
 
Kwani amesahau kauri yake sk alijifanya shehe yahaya. Chezsa mabadiliko usipoyakubali yanakubadilisha tu
 

dawa pekee ya kuiuwa cdm ni ccm kujirekebisha\kuendesha nchi kwa uwazi na kuacha siasa za kulindana, hakuna njia mbadala
 
Wanaanza kukiri pole pole ili baadae waombe kuhamia CDM.
 
Viongozi wote wa ccm walipoteza hekima siku nyingi sana
 
Tunakushukuru Mzee Wassira kwa kuwa Muungwana kwa kueleza ukweli ila tu msiote hizo ndoto zenu za kukifuta Chadema itakugharamuni mjute maisha
 
Hivi demokrasia ni kuviua vyama vya upinzani au kutangaza sera madhubuti....
Kiongozi usije ukafikiria hawa viongozi wa CCM na wanachama wao wana mawazo yoyote mbadala ya kisera au hata wanafkiria kutunga sera mbadala. Wao wanachofikiria ni kutafuta mbinu chafu kukiua chadema, wanadhan wakishaiua chadema wananchi ndio wataipenda CCM. CCM inadhan tatizo lake kubwa ni uwepo wa CDM, Hawajui kuwa hata CDM ikifa leo hii bado CCM haikubaliki.

CCM hawajajua kuwa kinachoiua CCM ni CCM yenyewe. Na kwakuwa hadi sasa CCM bado hawajajua kuwa tatizo la CCM ni CCM yenyewe, basi kupona kwake ni ngumu sana. Kama wangejua tatizo ni nini at least tungeweza kusema one day wanaweza wakaja kulitatua hilo tatizo na kurudi ulingoni. Ila kwa utaratibu huu wa kihuni wanaoutumia sasa hiv ili kujijengea mvuto kwa wananchi, ndio wanajimaliza kabisaaaaa!
 

Kwingine kote umepatia, lakini hapo penye RED umekosea. Walimuua Mwangosi. Hawakushindwa bali walifanikiwa.
 

Hivi huyu mzee kwa umri wake kwa nini hatulii na kutumia busara kama wazee wengine?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Jaman msimshambulie mzee wa Ikulu(Waaa cra)kaongea ukweli,kumbe kauri za Tendwa ni kushawishiwa na akina Joka kuu(jk) na kundi lake na sio yeye,kukenua mwanya tu ka panzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…