Wasomi wapongeza Rais Samia anavyochungulia fursa kwa Mataifa tajiri

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wachambuzi wa masuala ya uchumi na diplomasia wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuhudhuria mkutano wa mataifa matano tajiri (BRICS), wakisema kitendo hicho kinaimarisha uhusi-ano wa kimataifa na kama
Tanzania ikijiunga itakuwa na uchumi imara.

Mkutano huo wa siku mbili ulihitimishwa jana jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini ambako ilishuhudiwa nchi sita zikikaribishwa kwenye umoja huo.

Mkufunzi wa Chuo cha Diplomasia, Goodluck Ng'ingo alisema Rais Samia kuhudhuria mkutano huo kumekuwa na maana kubwa katika nyanja muhimu hasa ya kiuchumi.

"Kama tutaingia kwenye umoja huo tunaweza kupata mikopo kwa masharti nafuu, lakini pia tutafiti sana kwa sa-babu nchi nyingi wanachama huko hazina malighafi na sisi tunayo kwa hiyo ni nafasi nzuri ya kufanya biashara na kujimarisha kiuchumi....tukiingia ni jambo zuri," alisema Ng'ingo.

Naye Profesa Samuel Wangwe alisema anaomba kuwe na mahusiano yaliyokomaa kati ya Tanzania na umoja huo kwani ni jambo lenye manufaa kwa nchi.

"Nchi za BRICS uchumi wake ni mkubwa na ni watu ambao tunafanya nao biashara ni mwanzo mzuri kwetu," alisema Profesa Wangwe ambaye ni mbobezi katika uchumi.

Profesa Abel Kinyondo alisema Rais Samia anaendeleza sera ya Tanzania kutofungamana na upande wowote ndio maana yupo kwenye kutafuta urafiki wenye manufaa kwa yeyote.

"Nchi za BRICS zinakuja juu kiuchumi. Mfano leo (jana) imetangazwa kuna nchi zimekaribishwa kuingia, unaona jinsi gani watu wanavyochangamkia kujiunga. Kuna Saudia, UAE na huko ndipo tunapochukua mafuta..
"Rais amenda kunusanusa kisha anarudi kutulia na kutafakari na kufanya maamuzi... tukijiunga nchi yetu itafanikiwa kwa sababu tayari tunashirikiana nao baadhi kama China," alifafanua Profesa Kinyondo.

Licha ya Rais Samia kuhudhuria mkutano huo, pia alifanya mazungumzo na Rais wa China, Xi Jinping.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa aliwatangazia wanachama wa umoja huo jana kuwa wamezikaribisha nchi sita kujiunga nao Januari mwakani. Nchi hizo ni Argentina, Misri, Iran, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

"Tumekubaliana katika awamu ya kwanza kuwakaribisha hao, nyingine zitafuata, uanachama wao utaanza rasmi Januari Mosi mwaka 2024," alisema Rais Ramaphosa.

Aliongeza kuwa umoja huo uko tayari kusaidia wanachama wake kuwa na uchumi endelevu hivyo wanaagiza viongozi wao kushirikisha mawaziri wa fedha kuzingatia hilo na kuleta mrejesho katika mkutano ujao.

Mkutano huo wa 15 ulihudhuriwa na wakuu wengine wa serikali na mataifa ibalimbali wapatao 50. Viongozi wa nchi zinazounda umoja huo walitoa hotuba zilizolenga mwelekeo wa kundi hilo la kiuchumi na hatima yake katika dunia ya sasa
 
Tutatoboa zaidi tukiamua kujiunga na Umoja wa Falme za Kiarabu. Huko BRICS tuwaachie Urusi na washirika akina Niger na Burkina Faso.
 
Kuchungulia fursa ni sawa kabisa!
Lakini je, wasomi wetu wana uzalendo na akili za kutetea maslahi ya nchi ukifika wakati wa kuingia mikataba?
 
Tutatoboa zaidi tukiamua kujiunga na Umoja wa Falme za Kiarabu. Huko BRICS tuwaachie Urusi na washirika akina Niger na Burkina Faso.
Of course Mali,DRC na CAR wanalindwa na Russia kwa sasa.

Tukiwa makini kuna fursa hapa kupata mafuta, gesi kutoka Urusi, Saudi Arabia UAE kwa bei nzuri, Soko huko India na South Africa.

Bidhaa na uwekezaji wenye tija kutoka China.

Muhimu umakini. To be serious about serious things. Vitu vinavyotugusa wote,, mustakabali wa Taifa.
 
Kuchungulia fursa ni sawa kabisa!
Lakini je, wasomi wetu wana uzalendo na akili za kutetea maslahi ya nchi ukifika wakati wa kuingia mikataba?
Hapo sasa? Sio tu wasomi, serikali yetu inaweza kuwa ya kizalendo, makini kuhusu maslahi ya Taifa zaidi ya kufikiri maslahi binafsi na ya familia zao?
 
Hapo sasa? Sio tu wasomi, serikali yetu inaweza kuwa ya kizalendo, makini kuhusu maslahi ya Taifa zaidi ya kufikiri maslahi binafsi na ya familia zao?
Unazungumzia serikali! Ipi? Hii iliyotokana na ccm?
Wawe makini alafu watakula wapi??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom