Wasomi wapinga kiinua mgongo cha wabunge

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Sadick Mtulya

SIKU chache baada ya Bunge kupitisha muswada wa sheria ya gharama za uchaguzi wa mwaka 2009, wasomi nchini wamesema wabunge wawe wakilipwa kiinua mgongo baada ya uchaguzi kumalizika ili mazingira ya ushindani katika chaguzi yawe sawa.

Katika utaratibu wa sasa na ambao umekuwa ukitumika wabunge kulipwa kiinua mgongo baada ya Bunge kuvunjwa huku ikiwa imebakia miezi michache kabla ya uchaguzi kufanyika.

Bunge lilipitisha muswada huo Jumatano iliyopita, baada ya kufanyiwa marekebisho kwenye baadhi ya vipengele. 


Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, Profesa Mwesiga Baregu, Dk Benson Bana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bashiru Ally walisema kitendo cha Bunge kuridhia muswada huo lina lengo la kuweka sawa mazingira ya ushindani katika uchaguzi, hivyo ni wakati muafaka kwa wabunge kulipwa kiinua mgongo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec) kutoa matokeo.

Ally, ambaye ni Mhadhiri Msaidizi UDSM alisema: "Ili ulingo wa ushindani uwe sawa katika uchaguzi, wabunge wapewe kiinua mgongo chao baada ya NEC kutangaza matokeo".

Mhadhiri huyo, ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa alifafanua kwamba, kitendo cha wabunge kupewa kiinua mgongo kabla ya kufanyika uchaguzi kitawachochea kuzitumia fedha vibaya katika kampeni.

"Utawalinganishaje katika uchaguzi, huyu ambaye ametoka kupata fedha(Mbunge) na yule ambaye anataka kuwa mbunge," alisisitiza Ally.

Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa UDSM, Dk Benson Bana alisema pamoja na mambo mengine, muswada huo umelenga kudhibiti mianya ya rushwa na matumizi holela ya fedha wakati wa uchaguzi, hivyo wabunge wapewe kiinua mgongo baada ya uchaguzi kumalizika.

"Pamoja na muswada huo kupitishwa, serikali ijipange kuunda chombo maalumu kwa ajili ya kuratibu sheria hii. Pia fedha za kiinua mgongo wanazolipwa wabunge baada ya kumaliza muda wao wa miaka mitano, walipwe baada ya uchaguzi kumalizika," alisema Dk Bana.

Alisema kuwepo kwa chombo hicho kutasaidia kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika muswada huo.

"Siku zote tumekuwa tukipitisha sheria nyingi, lakini tatizo linakuwa ni utekelezwaji wa sheria hizo," alifahamisha Dk Bana.

Naye Profesa Baregu alisema, ili kusawazisha uwanja wa ushindani katika medani ya siasa hasa katika chaguzi, wabunge wapewe kiinua mgongo baada ya wabunge wapya kuapishwa bungeni.

"Itakuwa ni busara kama wabunge wakilipwa kiinua mgongo chao mara baada ya wabunge wapya kuapishwa bungeni. Hii itasaidia kuleta uwiano sawa wa ushindani katika chaguzi," alisema Profesa Baregu.

Miongoni mwa vipengele vilivyorekebishwa katika muswada huo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ni kinachohusu eneo la Msajili wa Vyama vya Siasa kuingia na kukagua nyaraka za vyama bila kutoa taarifa na eneo la ukomo wa fedha za matumizi ya uchaguzi.

Pamoja na muswada huo kupata upinzani mkali kutoka kwa wabunge kabla ya kuwasilishwa bungeni, hatimaye ulipitishwa siku moja kabla ya mkutano wa 18 wa Bunge kufungwa Ijumaa iliyopita.

Wakati wa kujadili muswada huo baadhi ya wabunge wakiwemo wa kamati hiyo na kambi ya upinzani walipinga baadhi ya vipengele na hasa kuhusu kuwakirimu wapambe na kiliporekebishwa waliunga mkono na kuupitisha.

Katika kujadili kipengele hicho, yalitokea mabishano makali kati ya Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge na Jaji Werema ambaye baadaye aliridhia yafanyike mabadiliko ndipo wakaafikiana na baadaye muswada ukapita.

Awali baadhi ya wabunge walisema muswada huo usitumike sasa badala yake upitishwe katika Bunge jipya litakaloanza baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa vile muda uliobaki ni mfupi kuitafsiri. Walisema sheria hiyo inahitaji muda wa kutosha kuitafsiri na kwamba, kama utapitishwa sasa wabunge wengi watafungwa kwa kufanya makosa kwasababu ya kutouelewa vizuri.



My take:
Hii imetulia!!!, ila kwa wale ambao hawagombei wanaweza kupewa fweza zao mapema.
 
Hodi hodi uwanjani,unajua lazima tuweke mazingira sawa ya kiushindani lakini katika hili usawa hakuna maana kiinua mgongo gani ambacho kwanza kinatolewa haraka kiasi hicho hapa Tanzania,wadau naomba mnisaidie watanzania wangapi wanamaliza utumishi wao katika umma lakini kama wana gratuity yao kuipata inakuwa ni mbinde sasa hii maana yake ni maandalizi ili itumike kwenye uchaguzi mkuu ,na sisi tupo macho katika hili maana haki haipo baina ya wagombea wapya na wale waliokuwa mjengoni,wadau nawasilisha hoja
 
haki haipo hata kidogo na hiyo miswada ni kwa minajili yao tu,mwaka huu we acha tu hakuna ushabiki ni sera tu.
 
hoja ni nzuri maana ina maana kuwa watu wenye pesa ndio wenye uwezo wa kuchaguliwa. So long term soln? watu wote waelimishwe watu wengi hawana elimu wako vijijini ukimpa tshirt na 10,000 basi kazi imeisha, so hatutaendelea kwa namna hii. tuchague viongozi wenye uchungu na wananchi na nchi yetu. swali utawajuaje? kwa sera? kila mtu ana sera nzuri so unapima and then baada ya miaka 5 assessment kama hakufanya kitu asipewe kura. Tena sio yule mtu anayekaa ukikaribia uchaguzi ndio anaenda jimboni, that is not a kind of leadership. amesikiliza saa ngapi matatizo ya wananchi? sio mambo yote yanahitaji fedha ndio watu waendelee. jamani tanzania? ooh sijui nani atatukomboa?
 
hoja ni nzuri maana ina maana kuwa watu wenye pesa ndio wenye uwezo wa kuchaguliwa. So long term soln? watu wote waelimishwe watu wengi hawana elimu wako vijijini ukimpa tshirt na 10,000 basi kazi imeisha, so hatutaendelea kwa namna hii. tuchague viongozi wenye uchungu na wananchi na nchi yetu. swali utawajuaje? kwa sera? kila mtu ana sera nzuri so unapima and then baada ya miaka 5 assessment kama hakufanya kitu asipewe kura. Tena sio yule mtu anayekaa ukikaribia uchaguzi ndio anaenda jimboni, that is not a kind of leadership. amesikiliza saa ngapi matatizo ya wananchi? sio mambo yote yanahitaji fedha ndio watu waendelee. jamani tanzania? ooh sijui nani atatukomboa?
nakuunga mkono kabisa,hizi t shirt na 10,000 wanazo toa kununua kura ndio zinawafanya wasitumikie wananchi kwani wanajua kwamba wamenunua kura na hawakuchaguliwa kwa utendaji wa kazi.

wabunge wengi hawafanyi kazi iliowapeleka kwa vile wanajua jinsi ya kununua ushindi.kazi kubwa ndio hio kuwaelemisha ndugu zetu vijijini.
 
sipendi kweli haya mambo ya "wasomi hiki"; "wasomi kile".. kama usomi ungekuwa chachu ya mabadiliko tungekwishabadilika. Kutuambia kitu ambacho kiko wazi hakiitaji usomi.
 
Vipi watu wengine wanaolipwa mafao yao kisha wanayahamishiana majimboni? Nafahamu kuna watu katika mashirika wanalipwa pension mamilioni mengi zaidi kuliko hao wabunge, na wanazihamishia huko majimboni hawa nao vipi? Kuzuia mafao sidhani kama hiyo ndiko kusawazisha uwanja!!
 
Hili liinchi bana....yaani kila mtu ni msanii, mbabaishaji, na mzugaji tu. Linakera sana hili liinchi....jitu unaliona tajiri unadhani lina akili na limetumia akili zake kupata mali kumbe wapi, ni jizi tu.
 
Hili liinchi bana....yaani kila mtu ni msanii, mbabaishaji, na mzugaji tu. Linakera sana hili liinchi....jitu unaliona tajiri unadhani lina akili na limetumia akili zake kupata mali kumbe wapi, ni jizi tu.

hili au lile? Kwani wewe upo TZ saa hizi? Shikamoo boss :)
 
haki haipo hata kidogo na hiyo miswada ni kwa minajili yao tu,mwaka huu we acha tu hakuna ushabiki ni sera tu.

Nani alisema kuwa mwaka huu hakuna ushabiki? Ngoja TOT itakapoanza kumwaga mipasho nchi nzima ikifuatiwa na fulana, kofia, khanga na pilau za bure ndipo utakapojua kuwa ushabiki bado ndio utakaoamua, siyo sera kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom