Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Ili kukata mzizi wa fitina tume huru iundwe,wakiwemo kina mbowe,mkono,mengi,simbachawene,wasira,mwiguru,etc,wafuatilie hesabu yote A to Z,iwekwe wazi maana kina zito wanadai pesa ya umma bilioni 321 au 306 imeibiwa ,wakati kwenye account ya escrow zilikuwemo bilion 182.
sasa hizo zingine waliiba toka wapi?

ni kweli mkuu kinachotakiwa ni rais aunde tume huru ili kujiridhisha kati ya maelezo ya CAG na ripoti ya PAC, ili kutoa maamuzi yalivyo sahihi
 
Lakini wewe MTK si umeenda shule,hebu weka ushabiki kando ,uanze kupangua point za hao vijana.
tuambie inakuaje kina zito wadai zimechotwa bilion 321 wakati zilikuwemo bilion 182?

mkuu ELUNGATA WAKINA ZITTO WAMEAMUA KWA MAKUSUDI KUPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA ILI KUVURUGA AMANI YA NCHI KWA KUSERVE MATAKWA YA WAFANYABIASHARA WENYE TAMAA
 
uwiiiii!! Uwiiiii!! Uwiiii!!!!! Jamani tumekwisha kama wasomi wetu ndiyo hawa, hatuna wasomi hapa nchini!

Niwaulize swali dogo sanaaa!! La darasa la chekechea au vidudu kwa lugha nyingine, hivi wameona kasoro hiyo tu ya kamati ya bunge (pac) - wakati maoni yetu yakichakachuliwa ndani ya bunge la katiba walikuwa hawajahitimu usomi wao????? Mamamaaaaaa!! Aiseee nikubaliane na wale waliosema njaa kweli mbaya, leo mnakubali kudhalilisha usomi wenu kwa thamani ndogo ya fedha!!! Waombeni radhi watanzania! Na ikibidi jiwekeni wazi majina yenu tuwajue!!!

Kama mmekerwa na jinsi bunge lilivyojadili suala la akaunti ya tegeta escrow, basi hata mambo mengine ya msingi mgeyajadili na kuishauri serikali yetu, mfano ni tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini, wapo wazee mpaka leo wamenga'ang'ania madaraka ya nchi hii hawataki kuachia ngazi, hilo ninyi mnaliona sawa, deni kubwa la taifa, ambalo linatisha hatujawasikia mkipiga kelele kuhoji fedha zilizokopwa zilitumika katika miradi ipi ya maendeleo hapa nchini!!!

Jamaniii watanzania kumbe hatuna wasomi, inatishaaa na kuogofya saaaaaaana!!!!

yaani hata hueleweki mara hatuna wasomi wala wasomi wamekubali kutumika tuache ushabiki wa chama na kuona mambo katika rangi yake halisi
 
sishangai, hawa ndiyo 'wasomi' wa kibongobongo wanaotumia kwato na matumbo kufikiri. Wanafikiri, kuona na hata kuelewa tofauti na binadamu wote! Ni wasomi wa kisisiemusisiemu eti!
Ubongo wa umenunuliwa kwa rupia, vichwani kujazwa tope na kwa fahari wanatetea baba zao.
Walaaniwe sasa had i vizazi 100 vijavyo!

laana hiyo isiwapate kamwe zaidi ulaaniwe wewe na wazazi wako milele na milele amina
 
ni kweli mkuu kinachotakiwa ni rais aunde tume huru ili kujiridhisha kati ya maelezo ya CAG na ripoti ya PAC, ili kutoa maamuzi yalivyo sahihi

Ni maelezo ya PAC, TRA, PCCB na CAG. Naamini hao wengine walihojiwa na PAC tena kwa viapo.
Hao wasomi mkakati hawana jipya!
 
ndugu hawa vijana ni mbwa flani vile.

Wanaidhalilisha hadhi ya vyuo vyetu, uelewa wa vijana wa tanzania na kizazi hiki.

Hawa walistahili kupigwa hadharani. Taifa linateeketea halafu kenge wa div - 5 na brn wanasifia upumbavu!!!!!!

yaani appearance yako unafanana na huo ----- uliopost dada yangu
 
ni maelezo ya pac, tra, pccb na cag. Naamini hao wengine walihojiwa na pac tena kwa viapo.
Hao wasomi mkakati hawana jipya!

hakuna maelezo yao hao soma ripoti ya cag uone mawazo ya ofisi yake sio maneno waliyookoteza wanakokujua eti kwenye vitabu na majarida, soma ripoti ya cag uone viongozi wetu walivyowajibika katika hilo sio maneno waliyolishwa na mafisadi wa vitalu vya madini wanaojiita wajasiliamali
 
Sishangai, hawa ndiyo 'wasomi' wa kibongobongo wanaotumia kwato na matumbo kufikiri. Wanafikiri, kuona na hata kuelewa tofauti na binadamu wote! Ni wasomi wa kisisiemusisiemu eti!
Ubongo wa umenunuliwa kwa rupia, vichwani kujazwa tope na kwa fahari wanatetea baba zao.
Walaaniwe sasa had I vizazi 100 vijavyo!

Hapana mkuu, hawawezi kulaaniwa sababu wametofautiana na mawazo yako. Hatuwezi kushabikia ushabiki wa kisiasa na chuki binafsi za watu, CAG anasema fedha zilizokuwemo kwenye account ni sh bilioni 183, PAC wanasema sh bilioni 306 tumwamini nani sasa? Ripoti ya CAG inasema inawezekana kuna fedha ya umma ya kutolipwa kodi, sinashida na hili mimi kama ni kodi TRA wahakikishe kodi hiyo inalipwa lakini CAG hakusema kuwa fedha za escrow ni mali ya umma kwa kauli iliyonyooka, CAG anasema inaweza kuwa ya TANESCO au ya IPTL.


Ac
 
Kweli njaa mbaya....mi sijawaelewa kwanza maana composition yenu inadhalilisha elimu zenu mmejinunulia aibu kwa bei rahisi sana bora mngesema vijana wa sekondari.
 
yaani appearance yako unafanana na huo ----- uliopost dada yangu


avatar251087_1.gif
unadhani binadamu whenye avata ya aina hii atakuwa nazo kichwani????
 
MASWALI KWA PAC

1. Tunaitaka kamati hii itueleze, ni katika ukurasa wa ngapi, aya ya ngapi, nukta ya ngapi iliyopo kwenye ripoti ya CAG inayosema kwamba ESCROW ni MALI YA UMMA?.

2. Tunaitaka PAC itueleze, ni katika ukurusa wa ngaopi, aya ya ngapi, nukta ya ngapi iliyopo kwenye ripoti ya CAG inayosema kwamba MUHONGO na wenzake wamefanya makosa hivyo wawajibishwe.

3. Tunaitaka PAC ituonyeshe, ni wapi katika ripoti ya CAG imesema fedha ambazo IPTL imezichukua kutoka kwenye ESCROW ni BIL ama 321 au 306 kama wanavyodai.

4. Tunaitaka PAC itueleze, kama kulikuwa na mchezo mchafu, na wakauthibitisha, iweje wizara ya fedha isihusike?, kwanini Gavana wa BOT na timu yake na Waziri wa fedha na Timu yake nao wasihusike kwenye hilo kwa kuwa fedha ilikuwa kwao?.

5. Kama kweli kulikuwa na mchezo mchafu, iweje BRELLA, na wizara inayoisimamia ambayo ni Viwanda na Biashara na waziri wake na timu nzima wasiwajibishwe nao kusajili kampuni ambayo wanadai siyo halali?.

6. Kama ni kweli kuna tatizo, iweje TRA wakubali kupokea kodi ya zaidi ya Bil 30 kutoka kwa mbia wa IPTL ambao ni VIP iliyotokana na mauzo ya hisa 30% kwa PAP?. Kwanini TRA isiwajibishwe kwa kupokea fedha haramu na kuziingiza kwenye mapato ya serikali ilihali ikijua ni fedha haramu?.

7. Kama PAC walikuwa wanachambua Ripoti ya CAG, kwanini walimwita tena CAG na kutumia mawazo yake binafsi na ambayo hajayaweka wazi moja kwa moja, na kwanini hawakuwaita watuhumiwa waliowabaini?. Uko wapi utawala wa sharia hapa?.

8. PAC itueleze, tangu lini Bunge limekuwa walalamikaji, waendesha mashtaka, wasikilizaji kesi, majaji, na waandika hukumu?.

MAPENDEKEZO NA MSIMAMO WETU.
Kwa kuwa Bunge wao wamepeleka maombi yao haramu kwa Rais, nasisi tunapeleka mapendekezo yetu kwa Rais na kumsihi afanye yafuatayo.

1. Kwa kuwa Swala zima la ESCROW limegubikwa na siasa, maslahi binafsi, chuki, wivu na kukomeshana, hivyo tunamuomba Rais asitekeleze azimio hata moja mpaka kwanza umma utakapoelewa ukweli halisi wa mbivu na mbichi na kila lililo nyuma ya pazia kuhusiana na sakata hili


2. Tunamuomba Rais Aunde chombo huru, ili swala hili lichunguzwe na kufanyiwa maamuzi huru ikiwemo na Tuhuma za baadhi ya Wabunge kuhongwa, kununuliwa na kuwa mawakala wa Benki ya Standard Charterd.

3. Tunamuomba Rais, aviagize vyombo vyake vya ulinzi na usalama viwachunguze wabunge hawa kwa kukubali kutumiwa, kuhongwa na kununuliwa ili kutuondolea watetezi wetu wa Rasilimali.
 
Naam, hayo maoni ya wasomi yanalingana sana na maoni yangu siku zote humu JF.
 
Kimsingi PAC walifanya kazi yao kwafitina kubwa ya kisiasa na watu ni wazi walikamiana na kutaka kuoneshana ubabe wao. Mapendekezo yao hayajashabihiana na kilichoandikwa kwenye ipoti ya CAG.
 
Back
Top Bottom