Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Muhongo kwa sababau tu tangu kuingia kwake ofisini ameziba mianya ya uchotwaji mkubwa wa pesa za watanzania kupitia sekta ya madini, na sasa mabepari wameungana na wabunge wenye husda kupambana dhidi ya kweli na haki anayosimamia Muhongo.

Kumpoteza Muhongo kwa sababu tu yeye na Katibu mkuu wake Eliakim Maswi, hawana mawasiliano mazuri na Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe (Hii inatokana na kitendo chao kudhibiti udalali wa Rasilimali).

Kama ameziba mianya ya uchotwaji mkubwa wa pesa za watanzania mbna hakuna unafuu wowote, hata nukta ya bei ya umeme haijashuka, zaid ya kutubadilishia mamita ya umeme yanayotafuna umeme balaaa
 
Inanisikitisha Sana watu wanapokuja na taarifa ambazo zinaandikwa kishabiki na kuwalinda watu. Nasikitika Sana mtu anapofanya personal attack badala ya kufanya mambo kwa kuegemea facts. Kwanza kwa taarifa hii maana yake wamelitukana bunge la jamhuri ya Muungano Wa Tanzania. Unapowatukana PAC maana yake umetukana bunge.
t

WATANZANIA, TUSIPENDE KUWAONA WENYE MTAZAMO NA SISI KUWA NI WASIOJUA.SWALA LIKITAZAMWA KWA UMAKINI NA YEYOTE MWENYE UTIMAMU WA AKILI NA ALIYE HURU KIFIKRA, UTAGUNDUA PASI SHAKA KWAMBA PAC ILIWAKAMIA WATU FLANI FLANI VINGNEVYO TUNGEONA WAZIRI WA FEDHA,VIWANDA,GAVANA NA CEO WA TANESCO WAKIGHUSWA.PAC INATAKIWA ICHUNGUZWE PIA.BUNGE LETU LIMEJAA WATU WENGI WASIOJITAMBUA NA WENYE UELEWA MDOGO, HATUWEZI KUWAACHA WATUAMLIE MAMBO YA MSINGI.
 
JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA.
MAONI NA MTAZAMO WA JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA KUHUSIANA NA MAADHIMIO YA BUNGE KUHUSU RIPOTI YA CAG YA NOV 26-28.2014


Tunaanzisha sasa hati ya maombi maalum kwa Raais (Petition Form) itakayosainiwa na mamilioni ya watanzania wanaoitakia mema nchi yetu kumuomba Rias apuuze maazimio haya ya mabepari, wahujumu uchumi na wasaka tonge walioungana na wasaka Urais.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki wazalendo na watetezi wa kweli wa Rasilimali.

Imesomwa na

Shaibu Sufiani

Kaimu Mratibu Umoja wa wanazuoni vijana Tanzania


View attachment 210855 View attachment 210856




Eti wanazuoni-Wanazuoni wa Lumumba yes!
Nchi hii kila mtu anajipa cheo na hadhi kadri ajisikiapo.Lakini kinachosikitisha ni uwepo wa genge la vijana kujiingiza kwenye kazi hizi za ukuwadi kwa ufadhili wa Wezi wa mali za Umma.
 
Hao ni wasomi gani tena? Mana siku hizi kila mtu anajiita msomi. Mtu akisafiri kwa mguu toka chuo mpaka mwenge zaidi ya mara tatu nne anapewa Uprofesa wa kutembea. Akilala njaa siku mbili tatu kwasababu amemaliza boom anapewa Uprofesa wa kulala njaa. Tabu ni pale wanapotaka tuwaite ni wasomi na maprofesa wakati hakuna lolote kichwani.

Adui kweli muombee njaa
 
wanachuo uchwara wakoje mkuu


dhihirisha uchwara wao kwa kupangua hoja zao.msilazimishe watu wawaze na kufikri kama ninyi.ni kwa kiwango tunaweza kuliamini bunge ambalo lilishndwa kuona umuhimu wa katiba kwa mstakabali wa taifa, leo muwaamini kwamba wana uchungu na taifa lenu??nyambafu zenu,wanafiki nyie na wabunge wenu.msiwe mazuzu,wabunge ni wanafiki,wara rushwa na uwezo mdogogo kiakili.wametumika na wahujumu uchumi wakubwa, mnawasifia??
 
nadhani hata kuchaguliwa kusomea kozi za mafuta ni favour walipewa na huyo wanayemtetea,watoe majina yao na kozi wanazosoma ili tuangalie kama walikidhi vigezo vya kupewa hizo scholarship.wanawakilisha wasomi wangapi?wana uhusiano gani na maesrow?

wewe una wivu na hyo ni kawaida yetu waswahili.hatungeweza kusomeshwa wote na isitoshe wengne tumefail hata qt.tufanye mengne na wivu hautusaidii.
 
Basi nyie wasomi naombeni muishauri serikali kuhusu tazizo la ajira, maji, elimu, umeme nk maana escrow hamuiwez.......
 
hao misukuke issue ya katiba pendekezi hawakuona mapungufu wanaona mapungufu kwenye hii issue inayomgusa mtu au watu wawili kuliko katiba inayowagusa watanzania wote kwa miongo kadhaa ijayo? Hii elimu ta siku hii balaa sana.


ninyi ndo mjihoji,bunge lililochakachua katiba ndo mnaliunga mkono kwa ufisadi waliofanya.kweli watanzani tuna kazi.nashindwa kuelewa, c c m wabovu na nchi imewashnd,wapinzani nao kwa mawazo kama haya naona kama wanakurupuka na hawako makini kimikakati,bora urudi utawala wa wajerumani tu.
 
hao ni kweli wanazuoni walioamua kuongea neno ili kuokoa taifa lao lililo kwenye mkwamo unaosababishwa na watu wenye uchu wa rasilimali za nchi hii kama yule mpenda dogodogo

nimependa comment yako.una fikra huru na akili yako iko active.
 
Mimi pia ni kijana niliyehitimu, ila nyie na wachumia tumbo.
Unasema ile hela si ya umma?
Kuna kodi yetu pale, hiyo nayo sio hela ya umma ok naomba kuuliza ile hela ili zalishwa wapi?, na kama si ya umma je, nini chanzo cha hiyo hela hapo? Na kama chanzo unakijua je muafaka ulipatikana kwaujibu ya capacity charge?
Na kama ulipatikana, je IPTL ilishinda ama ni Tanesco walishinda?
Calculation bado hazijafanyika kuhusu capacity charge what if Tanesco wakishinda, je wao hela watapata wapi? , na hiyo hela ya tanesco utaiita ni ya nchi za nje?

Waache ujinga, hata tanesco wangechukua nao wangekuwa kwenye makosa kwa kuwa bado muafaka haujapatikana. Wewe unayejiita msomi labda msomi wa sasa maanake ni kutumikia wakubwa lakini sio sisi wenye machungu ya kutafuta ajira.
 
logically kama cag angekuwa ndio final kamati isingeundwa, kama serikali inatoa pesa ya kuendesha bunge na waliridhia kuundwa hiyo kamati na ikawasilisha maana yake serikali inakubali uwepo wa kamati na uwezo wa wahusika!!!!

Ndio maana inaonekana kioja cha mwaka kukubali mchakato halafu majibu yanayotokana na mchakato ulioukubali uanze kukutatanisha!!!

kwa mtazamo wako,kamati ingechukua maamuzi na kuwaadhibu wahusika.kinyume na hapo mtoa maamuzi ana nafasi ya kuona linalofaa na lisilofaa ndo akawa top.
 
Kweli ninyi niwasomi maana mnajenga hoja za akina Pwagu na Pwaguzi nini msichoamini kuwa ile no fedha ya Umma. Tanesco wameingiza fedha kwenye akaunti hiyo mpaka suluhu ipatikane baina ya wawili hao sasa nani aliyetoaji jibu la capacity chaji mpaka mseme ni mali ya IPTL na pia kama ya IPTL kwanini itapanywe kiholela kwa kila mtu. Hivi ninyi wasomi mliwahi kusikia wapi dunia msaada wa kijamii kama kwenye shule na kanisani ukiingizwa kwa kupitia akaunti za watu binafsi kama ya Anna Tibaijuka, Andrew Chenge na wengineo
 
Taifa lina hasara kweli kweli kama huo ni Mchango wa wanazuoni. Sioni haja ya mimi kuwa mwanazuoni. Vinginevyo waibuke wanazuoni halisi wakanushe/wakosoe bandiko hilo.
 
Kuna haja ya majina ya wotewaliofadhiliwa na serikali kwenda kusomea sector gas nje ya nchi wadau tusaidieni isije kuwa yaleyale ya uhamiaji.
 
Duuh Eti wanazuoni?Labda wana chooni.
Wakati maelfu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu wamekosa mikopo,hilo hamjaliona na kulisemea?
Leo hii mmekuja na unafiki wa kutetea suala la Escrow,siamini kama walioandika taarifa hii ni wanazuoni. Kwanza suala la Escrow halihitaji hata uwe mwanazuoni.
***Nchi hii inahitaji watu wenye nia njema***
 
Sishangai, hawa ndiyo 'wasomi' wa kibongobongo wanaotumia kwato na matumbo kufikiri. Wanafikiri, kuona na hata kuelewa tofauti na binadamu wote! Ni wasomi wa kisisiemusisiemu eti!
Ubongo wa umenunuliwa kwa rupia, vichwani kujazwa tope na kwa fahari wanatetea baba zao.
Walaaniwe sasa had I vizazi 100 vijavyo!
 
Sishangai, hawa ndiyo 'wasomi' wa kibongobongo wanaotumia kwato na matumbo kufikiri. Wanafikiri, kuona na hata kuelewa tofauti na binadamu wote! Ni wasomi wa kisisiemusisiemu eti!
Ubongo wa umenunuliwa kwa rupia, vichwani kujazwa tope na kwa fahari wanatetea baba zao.
Walaaniwe sasa had I vizazi 100 vijavyo!

kwani wasomi wa kichademachadema wanapaka kinyesi kichwani au?
 
Back
Top Bottom