Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

wanazuoni jumuiya yenu inaitwaje , je imesajiliwa? mmesomea fani gani mpaka muone kila kitu hovyo kwenye ripoti ya PAC Maana hapakutakiwa habari ya miamba pale panataka sheria domestic na internationa masuala ya uhasibu wa kimataifa banking auditing finance wabunge na kamati walikuwa na taaluma hizi na access ya wataalam nje ya bunge au nyie ndo wasomi wa kwanza ? kaa kwenye radio msikilize mtukufu raisi anahitimisha mambo
 
Nakubaliana moja kwa moja na wasomi hawa. PAC haikutenda sahihi, CAG hakusema kuwa fedha ya escrow ni mali ya umma.
 
Bora nimeshapita umri wa kuitwa kijana. Kama ujana ndiyo huu, bora kubaki sie wazee tu...!

Natamani ningewaona na kuwaomba kuyajibu hayo maswali waliyouliza kwa kutoa usahihi wake...Mfano, kama siyo 306b, zilichukuliwa ngapi?

Shame on youths of this calibre!
 
wanazuoni jumuiya yenu inaitwaje , je imesajiliwa? mmesomea fani gani mpaka muone kila kitu hovyo kwenye ripoti ya PAC Maana hapakutakiwa habari ya miamba pale panataka sheria domestic na internationa masuala ya uhasibu wa kimataifa banking auditing finance wabunge na kamati walikuwa na taaluma hizi na access ya wataalam nje ya bunge au nyie ndo wasomi wa kwanza ? kaa kwenye radio msikilize mtukufu raisi anahitimisha mambo

Lakini mkuu huyo CAG aliyesoma hizo mambo za uhasibu mbona hakusema kuwa fedha za escrow ni mali ya umma, alichokisema ni kuwa sehemu ya fedha zinaweza kuwa za TANESCO au za IPTL. Hii conclusion waliyokuja nayo PAC wameitoa wapi wao?
 
hii ni nchi ya demokrasia watu wote wana haki ya kuongea kile wanachohisi ni sahihi kwao, na hii ni tatizo la demokrasia sio wao
Mkuu Rebeccamrema, kuna muda wa kuongea kila jambo. Tusipozingatia muda na taratibu hiyo inakuwa ni domokrasia na si demokrasia. Mkuu wa nchi ni Mtu wa mwisho kuingia uwanjani na wa kwanza kutoka. Hivyo ndivyo ilivyo. Na kwenye hili swala la ESCROW yeye ndoo alikuwa wa mwisho kutoa kauli rasmi ambayo tunasubiria utekelezaji wake. (Zimevuja kuwa waliokuwa wamewatuma hawa makinda wamepoteza. Mabadiliko tayari).
 
Naam, hayo maoni ya wasomi yanalingana sana na maoni yangu siku zote humu JF.

Wiki inaanza kesho mkuu tutaona msimamo wako kama unaendana na mkuu wa nchi au laa maana siasa za makundi zinawatesa sana wanaJF. Watuhumiwa lazima waende na maji na hasa Muhongo na Tibaijuka.
 
MWISHO
Ni mwendawazimu pekee ambaye, ama mtu mwenye wivu, chuki au maslahi binafsi kama ilivyo kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa PAC ndiye atakayeweza kudharau kazi nzuri nay a kizalendo inayofanywa na serikali hasa kupitia wizara ya nishati na madini na waziri wake.

Hakika Kwa MATUSI haya MMEVIMBIWA na KUJISAHAHU kwa hizo SCHOLARSHIP mlizopata kutokana na KODI YANGU.​
 
hii issue kwa lugha nyepesi ni beyond our reach its more interational than domestic
 
Lakini mkuu huyo CAG aliyesoma hizo mambo za uhasibu mbona hakusema kuwa fedha za escrow ni mali ya umma, alichokisema ni kuwa sehemu ya fedha zinaweza kuwa za TANESCO au za IPTL. Hii conclusion waliyokuja nayo PAC wameitoa wapi wao?

Kwa nini ZINAWEZA, Wakati kuna KODI ya VAT?
Hivi unajua VAT ni nini?
 
Da yaani hawajamaa wamenichefua kiukweli

Mimi ningewaona wa maana wangeweka majina yao tujue kama ni watoto wa masikini wenzetu au watoto wa ukoo wa panya. Nitakuwa wa mwisho kuamini kama hili ni andiko la wanaojiita wasomi
 
Rais Kikwete anapaswa kulitazama suala la IPTL ni matokeo ya msukumo wa wanasiasa, ushindani wa kibiashara, matatizo ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani, msukumo kutoka benki za nje, uelewa wa mdogo kwa baadhi ya wananchi kunakotokana na kukosa taarifa za sakata hilo.
 
JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA.
....................

Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki wazalendo na watetezi wa kweli wa Rasilimali.

Imesomwa na

Shaibu Sufiani

Kaimu Mratibu Umoja wa wanazuoni vijana Tanzania

Walikuwa wapi wakati report hii inasomwa Bungeni?

Hawa mapumbavu wanaodhalilisha elimu ya nchi hii ni wa wapi? Na huyo mfamaji anaetapatapa ni Nani? Nna hasira!!!!!

Si mmeshasema mmesomea masuala hayo nje na muasisi wa huo mpango anahusishwa!!??

Eti wasomi! !!!

duuu kwani wahitimu wa secondary nao wanazuoni?

Nawaombeni musishangae maoni ya aina hii kwa sababu ni wakati ambao nadhani waTZ tumebanwa sana na maisha kiasi kwamba sasa kila mtu anatafuta msaada wa kujinasua na ugumu wa maisha.

Tatizo kubwa kwangu ni ubora wa waandikaji. Kama kweli hawa wana digrii au wanasoma ili kupata digrii, hakika sasa nasema elimu yetu iko taabani. Hatuwezi kuwa na uandikaji wa chini kiasi hiki ktk kiwango cha chuo kikuu. Kwa maana nyingine hata uwezo wa kufikiri uko chini kiasi hiki!

Kama ni hivi, watu kama tezi dume watatawala tena miaka ijayo.
 
Lakini mkuu huyo CAG aliyesoma hizo mambo za uhasibu mbona hakusema kuwa fedha za escrow ni mali ya umma, alichokisema ni kuwa sehemu ya fedha zinaweza kuwa za TANESCO au za IPTL. Hii conclusion waliyokuja nayo PAC wameitoa wapi wao?

Kwa nini ZINAWEZA, Wakati kuna KODI ya VAT?
Hivi unajua VAT ni nini?

Hiyo si kauli yangu mimi ni kauli ya CAG! CAG anasema zinaweza kuwa za umma ukitazama kwa mtazamo wa kuwepo kwa kodi, lakini pia zinaweza kuwa za TANESCO au za IPTL.
 
Kuna Kundi la wafanyabiashara ambao walifanya kila juhudi ikiwa ni pamoja na kumwaga mamilioni ya fedha wakati wa vikao vya Bunge, kwa kuwatumia baadhi ya wabunge waliopo CCM na wengi kutoka vyama vya upinzani kuhakikisha Waziri na Katibu Mkuu wanaondolewa. Kwa sasa baadhi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara vimekuwa vikitumika kumshinikiza Rais Kikwete kuwaondoa.
Kwa upande mwingine Rais Kikwete anapaswa kuangalia maslahi ya nchi za magharibi zinazotaka kuhodhi mitambo ya IPTL kwa njia ya mlango wa nyuma.
 
Nakubaliana moja kwa moja na wasomi hawa. PAC haikutenda sahihi, CAG hakusema kuwa fedha ya escrow ni mali ya umma.

kabisa mkuu nami pia nakubaliana na mawazo yako kuwa PAC ilitumika vibaya
 
Nawaombeni musishangae maoni ya aina hii kwa sababu ni wakati ambao nadhani waTZ tumebanwa sana na maisha kiasi kwamba sasa kila mtu anatafuta msaada wa kujinasua na ugumu wa maisha.

Tatizo kubwa kwangu ni ubora wa waandikaji. Kama kweli hawa wana digrii au wanasoma ili kupata digrii, hakika sasa nasema elimu yetu iko taabani. Hatuwezi kuwa na uandikaji wa chini kiasi hiki ktk kiwango cha chuo kikuu. Kwa maana nyingine hata uwezo wa kufikiri uko chini kiasi hiki!

Kama ni hivi, watu kama tezi dume watatawala tena miaka ijayo.

umetia aibu hivi tope uloandika hapo juu sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu anaweza andika
 
Rais Kikwete anapaswa kulitazama suala la IPTL ni matokeo ya msukumo wa wanasiasa, ushindani wa kibiashara, matatizo ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani, msukumo kutoka benki za nje, uelewa wa mdogo kwa baadhi ya wananchi kunakotokana na kukosa taarifa za sakata hilo.

Come out more clearly. We need highest level of reasoning for a balanced discussion.
Ok say more than that, please!

Yooote uliyoandika yanaweza kuwa ni sababu ya pesa hizo kuondoka kwenye akaunti? Inaweza kuwa ni sababu ya watu kugawiwa mil. 4.6, 4.6, 4.6, etc. ???

Lazima tukubali kuna ujinga ulifanyika ktk serikali hii bila kujali sababu.
 
Wanazuoni gani nyie mnajua mamburula ni kuna asumta tu wengine bado wapo vyuoni nahivi wamepewa milioni tatutatu na laptop lazima wafanyekazi kwa kuwatetea wezi wenzao SHEM to them wengine wanatafuta Kik kwa kuwapinga watu maarufu wapuuzi kweli
 
Mimi ningewaona wa maana wangeweka majina yao tujue kama ni watoto wa masikini wenzetu au watoto wa ukoo wa panya. Nitakuwa wa mwisho kuamini kama hili ni andiko la wanaojiita wasomi

hawakutoa tamko ili uamini wao wametoa maoni yao kwa mheshimiwa rais ili kufikisha mawazo yao kuwa mheshimiwa rais aongeze za kwake na sio kuchukua maamuzi kuwaridhisha watu wanaotumikia wafanyabiashara walionyang'anywa vitalu walivyopanga kuuza kwa wazungu,hata huyu aliyetuma tamko jf ana matatizo,hili tamko apelekewe JK
 
Wiki inaanza kesho mkuu tutaona msimamo wako kama unaendana na mkuu wa nchi au laa maana siasa za makundi zinawatesa sana wanaJF. Watuhumiwa lazima waende na maji na hasa Muhongo na Tibaijuka.

sawa mama tutaona hayo unayosema
 
Back
Top Bottom