Wasomi wahoji ububu wa UKAWA bungeni

Wasomi wahoji ububu wa UKAWA bungeni

UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bungeni.

Hadhari hiyo imetolewa na wasomi na viongozi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, walipokuwa wakitoa maoni kuhusu uamuzi wa kambi hiyo kususa hotuba hiyo.

Dk Bana

Mhadhiri wa fani ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ndiye aliyesema kuwa kama uamuzi huo wa kuwa bubu bungeni hautabadilishwa, kambi hiyo itaonekana inalinda posho na kwamba haipo kwa ajili ya kutetea wananchi.

“Kazi yao ni kuwakilisha wananchi na makundi yote bungeni, sasa kitendo cha kuota ububu na kushindwa kueleza kero za wananchi, ni kutotendea haki wananchi maana ni vema wakae bungeni na kutoa hoja zao la sivyo, itafika wakati watatuomba radhi wananchi,” alisisitiza.

Akizungumzia hoja ya kwanza ya Mwenyekiti wa kambi hiyo, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kulalamikia muundo wa Serikali kutowekwa gazetini, Dk Bana alihoji kama Mbowe hajui kuwa muundo wa Serikali hautolewi kwa kila mtu.

Kuhusu suala la fedha zilizokatwa katika Mfuko wa Bunge na kuelekezwa katika utengenezaji wa madawati, Dk Bana aliwashangaa wawakilishi hao wa wananchi wanaopingana na uamuzi wa kumuinua mwananchi wa kawaida.

Alisema wananchi wote walipendezwa na hatua hiyo ya Serikali ya kuchukua fedha zilizotoka bungeni baada ya kubana matumizi na kupeleka katika kununua madawati.

“Hatua hii ni kielelezo kuwa Bunge lilikuwa likipangiwa fedha nyingi kuliko matumizi yake hivyo kusababisha kuwepo matumizi ya hovyo, sasa viongozi wa Bunge kuliona hilo na kurejeshwa kwenye jamii ni jambo jema,” alisema.

Alionya kuwa mikakati ya kambi ya upinzani, ni kutetea wananchi lakini kwenye hilo wananchi wenyewe kila kona wanawashangaa kwani inaonesha kutetea maslahi ya wabunge.

Bashiru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema wananchi wanaangalia vitendo vya wabunge wao ndani ya Bunge na watawahukumu kwani michango yao ndani ya Bunge ni muhimu na njia ya kutatua tatizo si kususa, bali kufuata taratibu za kisheria.

Alisema uamuzi wa kutozungumza, unaondoa maana ya vyama vya upinzani ndani ya Bunge kwa kuwa watashindwa kujadili masuala yenye manufaa ya wananchi, kwani mawazo ya kiongozi wa upinzani bungeni ni muhimu na yanawekwa kwenye kumbukumbu.

“Kuwekwa kwenye kumbukumbu mawazo hayo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo, sasa kitendo cha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kutumia vibaya nafasi anayopewa, ni udhaifu wa kimkakati,” alisisitiza Bashiru.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema wanavyofanya wapinzani ni jambo lisilopendeza katika kuleta umoja wa kitaifa, kwani wao ni wawakilishi wa wananchi ndani ya Bunge na kususa siyo jambo la kiungwana.
Hivi huyo bana ndiyo msomi pekee wa ccm au ndiye anakubaliana na matatkwa ya ccm ya kuburuzwa buruzwa?maana kila jambo baana kila tukio baana,tumechoka sasa
 
Wananchi wanawashangaa sana....hapo ndio wanapoenda kijizika 2020...
Huo ugoro wenu hamukuanza leo kurohoja tangu umeanza kujizolea viti vya ubunge ndio wimbo wenu kila siku hivyo na upunzani kila mwaka wa uchaguzi unazidisha viti bungeni
 
Mtu akikuambia jambo la kijinga na ukamwamini atakudharau- by JK Nyerere.
CCM imewaona wajinga sana baada ya kuwalisha uongo nanyi kama mazuzu mkaamini. UKAWA hawajapinga kununua dawati au dawa, wao wanazungumzia taratibu kufuatwa kama sheria inavyosema tatizo likowapi?
Mbona mnaruhusu CCM iwadharau hivyo kwa kusadiki ujinga?
Tafuta hata wa bunge wa CCM wenye kujielewa watakufahamisha kuwa kuna makosa ila kwa vile hawaruhusiwi na chama chao kukosoa wanaumia moyoni tuu na kujiona watumwa
Mkuu huyo unaye mwambia ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
 
Wewe ndo jinga kubwa, hujui kucheza na siasa!
Ona sasa mlivyopuuzwa! Yaani mnadhani mnaweza kuubadili mtizamo wa umma kwa hoja hiyo ya kijinga!?

Kwa Mara nyingine tena, UKAWA mmejiingiza kwenye ujinga wa kiwango cha PhD! Mpigieni magoti Dr Slaa ndo alikuwa na akili za kutosha
Wewe ndiye tumbaku bovu kabisa,naona unacheza ngoma ya vibwengo usiku wa manane
 
Kwa mwenendo huu tutakuwa na CCM imara sana na upinzani dhaifu sana! Wanajua fika kuwa kwa sasa CCM imeteka agenda zote na wao kubakia wakitapatapa!

Uchaguzi wa 2020 utakuwa nzuri sana kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani.
Masikini ya mungu,hii njaa ni hatari sana kwa vijana wa lumumba
 
Mkuu we bure kabisa ukawa ndiyo mnazidi kujimaliza hiyo ni hoja ya kijinga sana huwezi kumshawishi mtu mwenye akili akakuelewa.
Hivi na wewe unajihesabia kuwa kwenye kundi la watu wenye akili
 
Shida kubwa pia ambayo ukawa inawapa shida ni aina ya viongozi wakuu wa chama siyo aina ya viongozi wenye upeo mpana wa kufikiri na kuibua agenda za msaada kwa jamii katika ujenzi wa jamii mpya.
Majizi wakubwa nyinyi
 
Hivi huyo bana ndiyo msomi pekee wa ccm au ndiye anakubaliana na matatkwa ya ccm ya kuburuzwa buruzwa?maana kila jambo baana kila tukio baana,tumechoka sasa
Unaitwa kwenye uzi wa CAG kuisafisha NSSF.
 
Mtaimba sana ngonjera zenu lkn kilicho andikwa kwa wino kinaonkana na kila mwenye uelewa wa kusoma
Punguza jazba, wewe ndiye uliyekuwa unatuambia tusubiri ripoti ya CAG, tayari imekuishatoka......je kuna ufisadi wowote kauzungumzia kuhusu NSSF?
 
Punguza jazba, wewe ndiye uliyekuwa unatuambia tusubiri ripoti ya CAG, tayari imekuishatoka......je kuna ufisadi wowote kauzungumzia kuhusu NSSF?
Njaa itawauwa mwaka huu mmeamua kujiondoa ufahamu sababu ya njaa na uchumia tumbo,act ruzuku haitoshi mbunge mmoja! Sasa mmeamua kuitumikia ccm ili mradi mkono uende kinywani
 
Njaa itawua mwaka huu mmeamua kujiondoa ufahamu sababu ya njaa na uchumia tumbo,act ruzuku haitoshi mbunge mmoja!
Stick to the topic.....tulia ujibu hoja kimantiki, je CAG amezungumzia ufisadi NSSF?
 
Usiruke ruke kama maharagwe yachemkayo.......usipo pelekwa mahakamani hauwezi kuitwa fisadi hata kama umeliibia taifa?
Nani ana thibitisha makosa ikiwemo wizi,ufisadi?
 
Hivi niwaulize wadau. Mnawaonaje kwamba Ukawa hawaongei? Kupitia Media gani? Ungo? Bunge lipo gizani nyie mnawaonaje?
 
Back
Top Bottom