Wasomi wahoji ububu wa UKAWA bungeni

Wasomi wahoji ububu wa UKAWA bungeni

Kwa mwenendo huu tutakuwa na CCM imara sana na upinzani dhaifu sana! Wanajua fika kuwa kwa sasa CCM imeteka agenda zote na wao kubakia wakitapatapa!

Uchaguzi wa 2020 utakuwa nzuri sana kuanzia Rais, Wabunge taja yeyote na Madiwani.
Shida kubwa pia ambayo ukawa inawapa shida ni aina ya viongozi wakuu wa chama siyo aina ya viongozi wenye upeo mpana wa kufikiri na kuibua agenda za msaada kwa jamii katika ujenzi wa jamii mpya.
mtaje yeyote wa CCM aliyewahi kuibua hoja mpya yenye mashiko kwa jamii hapa. Bado hujanawa uso tu hadi leo? Uchaguzi ulishapita jadilini mtafanya nini ili mpewe ridhaa nyingine kirahisi bila kutumia vyombo vya ulinzi na usalama na tume yenu. Au ndio unauwinda ukuu wa wilaya kwa kujitia una maono ya 2020? Kama hukuifikia utaomba maternity leave kwa Mungu uje kuwashindisha CCM?! Punguza abstract thinking dogo! Waambie na wenzako waache kusafiria na kula kupitia mgongo wa ukawa kwani siyo size yenu na wa level ingine ya juu sana kwenu. Hoja zote zenye mashiko zinatoka ukawa, CCM taarabu tu!
 
UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bungeni.

Hadhari hiyo imetolewa na wasomi na viongozi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, walipokuwa wakitoa maoni kuhusu uamuzi wa kambi hiyo kususa hotuba hiyo.

Dk Bana

Mhadhiri wa fani ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ndiye aliyesema kuwa kama uamuzi huo wa kuwa bubu bungeni hautabadilishwa, kambi hiyo itaonekana inalinda posho na kwamba haipo kwa ajili ya kutetea wananchi.

“Kazi yao ni kuwakilisha wananchi na makundi yote bungeni, sasa kitendo cha kuota ububu na kushindwa kueleza kero za wananchi, ni kutotendea haki wananchi maana ni vema wakae bungeni na kutoa hoja zao la sivyo, itafika wakati watatuomba radhi wananchi,” alisisitiza.

Akizungumzia hoja ya kwanza ya Mwenyekiti wa kambi hiyo, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kulalamikia muundo wa Serikali kutowekwa gazetini, Dk Bana alihoji kama Mbowe hajui kuwa muundo wa Serikali hautolewi kwa kila mtu.

Kuhusu suala la fedha zilizokatwa katika Mfuko wa Bunge na kuelekezwa katika utengenezaji wa madawati, Dk Bana aliwashangaa wawakilishi hao wa wananchi wanaopingana na uamuzi wa kumuinua mwananchi wa kawaida.

Alisema wananchi wote walipendezwa na hatua hiyo ya Serikali ya kuchukua fedha zilizotoka bungeni baada ya kubana matumizi na kupeleka katika kununua madawati.

“Hatua hii ni kielelezo kuwa Bunge lilikuwa likipangiwa fedha nyingi kuliko matumizi yake hivyo kusababisha kuwepo matumizi ya hovyo, sasa viongozi wa Bunge kuliona hilo na kurejeshwa kwenye jamii ni jambo jema,” alisema.

Alionya kuwa mikakati ya kambi ya upinzani, ni kutetea wananchi lakini kwenye hilo wananchi wenyewe kila kona wanawashangaa kwani inaonesha kutetea maslahi ya wabunge.

Bashiru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema wananchi wanaangalia vitendo vya wabunge wao ndani ya Bunge na watawahukumu kwani michango yao ndani ya Bunge ni muhimu na njia ya kutatua tatizo si kususa, bali kufuata taratibu za kisheria.

Alisema uamuzi wa kutozungumza, unaondoa maana ya vyama vya upinzani ndani ya Bunge kwa kuwa watashindwa kujadili masuala yenye manufaa ya wananchi, kwani mawazo ya kiongozi wa upinzani bungeni ni muhimu na yanawekwa kwenye kumbukumbu.

“Kuwekwa kwenye kumbukumbu mawazo hayo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo, sasa kitendo cha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kutumia vibaya nafasi anayopewa, ni udhaifu wa kimkakati,” alisisitiza Bashiru.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema wanavyofanya wapinzani ni jambo lisilopendeza katika kuleta umoja wa kitaifa, kwani wao ni wawakilishi wa wananchi ndani ya Bunge na kususa siyo jambo la kiungwana.

Hawa wote ni wasakatonge tu. Hanna usomi wala fikra za kifalsafa.
 
Hawa wanaojiita wasomi,a.k.a wanafik wasiohoj ukiukaji wa katiba na sheria za nchi.Mimi namkubali Dr.Mdachi tu hapo wengine wote usomi wao ni kwa kujipendekeza hususan hao akina bhana.
 
Wahadhiri Bana na Bashiru wanataka zawadi uDC kama yule mwenzao wa Iringa mjini.Elimu inashuka wao wamenyamaza lkn mambo ya bunge wayanatolea matamko aibu kwa wasomi wetu.
 
Ukawa mmevurugwa nyie!!;mbona hela za sherehe za uhuru hawasemi!!;wasanii tu hao!!
 
Dr Bana kutokuwepo mwongozo ni tatizo kubwa zaidi. Unataka watu waendelee kujindanganya na kudanganya wananchi kuwa yote yako sawa? Unaunga mkono serikali inapoendeshwa kiholela? Eti mwongozo ni siri; ya nani kwa faida ya nani?

Kama instrument ya muundo wa serikali ni siri basi nchi hii imekwisha. Bunge litadhibiti vipi serikali wakati wabunge hawana ufahamu kitengo gani cha serikali kipo wapi? Hata sisi tusiyekuwa na elimu ya siasa na utawala tunaliona hili sasa kwa mtaalamu kama Bana inakuwaje? Labda nina uelewa hafifu!!!!!! au...............
 
Yaani ukiwa msomi wa CCM ni lazima ujitoe ufahamu,huyo mganga Bana aliona lini hilo bunge ambalo UKAWA walikuwa bubu???maana sisi huku Mbeya tunafungua TV zote kuanzia TBC,STAR TV,ITV,MLIMANI TV,BARMEDA TV,MBEYA TV,hatulioni hilo bunge.... Au linaonekana Dar tu????
 
Hivi unawezajje kutoa kitu bungeni bila kulishirikisha bunge
Heshima ya bunge kama muhimili unaojitegemea uko wapi??
 
Dokta Bana Kichwa maji kweli, unasema wamegeuka bubu, hapo hapo unajibu hoja zao, hizo hoja zilitolewa ndotoni au makalioni? HOVYO KABISA NA MPUUZI WA MWISHO.

Bashiru na Bana swali langu kwenu, Wananchi wapi hao? Wanawaona kupitia RAMLI? Au Vikao vya Bunge vinafanyikia Uwanja wa Jamuhuri Dodoma hivyo Wananchi wanawaona?
Mnajificha gizani halafu mnasema mnaonekana? Nyie mlitafakari kweli kabla ya maoni haya ya Kipuuzi?

Hakuna excuse yoyote linapokuja suala la Sheria. Sheria ikisema imesema. Unakiuka Sheria lakini unataka waliokiuka Sheria Wakutane na Sheria? Kwa nini watu wanavaa miwani ya mbao na kuishi kwa ushabiki? Kukiuka Sheria katika kuwashughulikia waliokiuka Sheria ni kuwapa nafasi nzuri ya kujitetea na kuishinda serikali mbele ya Sheria maana Sheria inahitaji kufuata Sheria kwa Waovu, hili nalo ni gumu? The current cheap popularity will cost this nation very soon, hapo ndipo mtakapoelewa!

Ili ueleweke umetumia neno sheria,sheria ila nimesoma between the lines hauna point...
 
Wewe ndo jinga kubwa, hujui kucheza na siasa!
Ona sasa mlivyopuuzwa! Yaani mnadhani mnaweza kuubadili mtizamo wa umma kwa hoja hiyo ya kijinga!?

Kwa Mara nyingine tena, UKAWA mmejiingiza kwenye ujinga wa kiwango cha PhD! Mpigieni magoti Dr Slaa ndo alikuwa na akili za kutosha
hapa ni jukwaa la kutukana au kujenga hoja? you are a disappointment for this forrum
 
Huna lolote, unanataka kusema kufanya reallocation hakutakiwi kufuata sheria? Kwa hiyo hata usiku first lady akimwambia kijijini kwa wakwe zako madarasa ya shule hayatoshi basi akiamka ana allocate fedha za daraja Mtwara ziende huko na hadithi imekwisha? Mamlaka ya rais ni ya kisheria sio kimungu mkuu, panua akili
Bahati nzuri nimeshajua ukomo wa akili yako ngoja niendelee kukusaidia..Baada ya Rais kusema nimebadili matumizi fulani basi wasaidizi wake wakiwemo makatibu wakuuu husika pamoja na Hazina wanaendelea na michakato ya kiserekali ili kuona maagizo ya Mkuu wa Nchi yanatekelezwa..Nadhani wewe ndio unahitajika kupanua akili na mengineyo maana unaonekana una ufinyu wa kufikiri
 
Zamani nilikuwa nadhani wapinzani ni imara,madhubuti,wana misimamo isiyoyumba kumbe bure kabisaaa!!baada ya kusimamia Sera ya uwajibikaji,kuondoa ufisad na rushwa wao wamekuwa ni wapuuzi wa kutetea ufisad uendelee yaani wapinzani especially ukawa haina haja ya kuwafikiria kuwapa Nchi!!CCM tawala hadi vizazi na vizazi hawa viazi, CHADEMA hakuna kuwapatia nafasi labda uwakilishi ili wafuate posho
 
Mtu akikuambia jambo la kijinga na ukamwamini atakudharau- by JK Nyerere.
CCM imewaona wajinga sana baada ya kuwalisha uongo nanyi kama mazuzu mkaamini. UKAWA hawajapinga kununua dawati au dawa, wao wanazungumzia taratibu kufuatwa kama sheria inavyosema tatizo likowapi?
Mbona mnaruhusu CCM iwadharau hivyo kwa kusadiki ujinga?
Tafuta hata wa bunge wa CCM wenye kujielewa watakufahamisha kuwa kuna makosa ila kwa vile hawaruhusiwi na chama chao kukosoa wanaumia moyoni tuu na kujiona watumwa
Politics is a propaganda game mkuu. Always remember that na hakuna chama cha siasa au mwanasiasa anayeshika na kudumu madarakani kwa kusema ukweli (daima). Imagine kwa mfano propaganda kabambe iliyofanyika wakati wa uchaguzi kuwaaminisha na kuwapumbaza watu wazima maelfu kwa maelfu kuanza kuzungusha mikono (hata bila kujua wanafanya nini), kuigiza kuzimia, kudeki barabara, kukesha wakilinda mahoteli "masihi" wao alipofikia n.k. Yote haya yalipangiliwa vizuri sana kuonyesha kuwa mgombea wao alikuwa anakubalika kupita kiasi.

Na ukizidiwa propaganda na mwanasiasa mwenzio usually hulalamiki bali una - counteract. Ndiyo maana huko kwa wenzetu wanasiasa na vyama vyao huajiri makampuni na professionals waliobobea katika mambo ya Public Relations, propaganda na campaigns management. Siasa siyo mchezo wa kulialia mkuu kwani nobody cares na ukiona mwenzio amefanikiwa kuwafanya watu mazuzu nawe zidisha mbinu uwafanye mazuzu mara mbili ili ajenda zako zifanikiwe. That's how you succeed in politics!
 
Nafikiri ni wakati muafaka kutakari sasa kama kuna haja ya UKAWA kuwepo ndani ya Bunge hili ambalo moja kwa moja ni Taasisi ambayo inaendeshwa toka Magogoni.Kwani Ndugai akiambiwa ruka anauliza tu urefu gania? Badala ya kuuliza kwa nini.
 
Bahati nzuri nimeshajua ukomo wa akili yako ngoja niendelee kukusaidia..Baada ya Rais kusema nimebadili matumizi fulani basi wasaidizi wake wakiwemo makatibu wakuuu husika pamoja na Hazina wanaendelea na michakato ya kiserekali ili kuona maagizo ya Mkuu wa Nchi yanatekelezwa..Nadhani wewe ndio unahitajika kupanua akili na mengineyo maana unaonekana una ufinyu wa kufikiri
Sasa kidogo unaelewa, jee hao wasaidizi walifuata hizo taratibu zinazofuata au walikaa kimya kama vile agizo limetoka kwa Mungu? Hicho ndio kinahojiwa. Sasa unatetea nini hapo great thinker?
 
Mtu akikuambia jambo la kijinga na ukamwamini atakudharau- by JK Nyerere.
CCM imewaona wajinga sana baada ya kuwalisha uongo nanyi kama mazuzu mkaamini. UKAWA hawajapinga kununua dawati au dawa, wao wanazungumzia taratibu kufuatwa kama sheria inavyosema tatizo likowapi?
Mbona mnaruhusu CCM iwadharau hivyo kwa kusadiki ujinga?
Tafuta hata wa bunge wa CCM wenye kujielewa watakufahamisha kuwa kuna makosa ila kwa vile hawaruhusiwi na chama chao kukosoa wanaumia moyoni tuu na kujiona watumwa
Kwa hiyo kama sheria haikufuatwa ndii wawe mabubu bungeni na kususa
 
Kwa hiyo kama sheria haikufuatwa ndii wawe mabubu bungeni na kususa
Kila nikiona umeni quote naanza kucheka kabla sijasoma. Najaribu kujiuliza ni kwa nini? Jambo hili hunitokea pia ninapotaka kuangalia futuhi.
 
Back
Top Bottom