Wasomi wahoji ububu wa UKAWA bungeni

Mtu akikuambia jambo la kijinga na ukamwamini atakudharau- by JK Nyerere.
CCM imewaona wajinga sana baada ya kuwalisha uongo nanyi kama mazuzu mkaamini.
Ukawa hawajapinga kununua dawati au dawa, wao wanazungumzia taratibu kufuatwa kama sheria inavyosema tatizo likowapi?
Mbona mnaruhusu ccm iwadharau hivyo kwa kusadiki ujinga?
Tafuta hata wa bunge wa ccm wenye kujielewa watakufahamisha kuwa kuna makosa ila kwa vile hawaruhusiwi na chama chao kukosoa wanaumia moyoni tuu na kujiona watumwa
Ndio kupinga kwenyewe huko umeambiwa Pesa imeenda kununua dawati kwajili ya watoto wewe huridhishwi nini mana yake
 
Kheri ukweli unaodumu kuliko uongo usio na mashiko. Acha watu wapuuze ukweli kwa muda kwa kutokufahamu lakini sio kusimamia uongo kwa ajili ya kupata support danganyifu.
Hao mnaowadanganya siku wakierevuka itakuwa ni kasheshe
Kama walivyo revuka na kuwafahamu UKAWA kama wapo kwajili yakulinda posho
 
UKAWA kweli ni shida, nondo zenyewe sasa,mpaka unajiuliza mara mbili huyu amepataje ubunge. hawa ukawa walikosea kuwashauri CUF watu wakawatosa. Sasa nadhani wanaendelea na sera zao za kususa. Tena mwanaume anasusa ,badala ya kupambana.
 
Mbona Dr. Bana hatujamsikia akisema lolote kuhusu serikali kuzuia matangazo ya TV live bungeni? maana hayo ndiyo yanayomfanya asione nini kinachoendelea huko, ndiyo maana anasema kuna watu wamekuwa bubu.
 
watu wenye Busara kama sisi kina gogo la shamba tunawasifu sana ukawa kwa wafanyavyo na tunawalaumu sana wabunge wa CCM kwa kuungana na serikali kupindisha sheria na kuwakandamiza wananchi
 
Ili tuweze kupiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni lazima wapinzani wawe na uzalendo na waache unafiki wa kuonewa huruma na mataifa ya nje kwa manufaa yao binafsi kwa kuleta migomo uchwara.Kwani kuna dhambi gani kwa pesa kwenda kutumika kwa manufaa ya wengi hata kama tena kwa maaumizi ya mkuu wa nchi.
 
Kwani bunge la Bajeti lililopita halikuidhinisha matumizi ya zile fedha kwa shughuli za Serikali? Anachofanya Rais ni kubadilisha matumizi ya mafungu (reallocation) jambo ambalo lipo kisheria na la kawaida sana. Afu kama kuna mbunge wa ccm ana shindwa kutoa dukuduku lake bungeni kwa hofu unayoisema huyo nae ni JIPU tu mbona wengine wanaongea.
Kama ulikuwa hujui kilichomuuma Mbowe ni kukatwa na kurejeshwa serikalini kwa Billioni Sita za Bunge, kwani katika safari za nje zilizokatwa zipo safari nyingi za Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambazo hazikuwa na tija..Mara nyengine acha kuleta hoja za vijiwe vya kahawa..Ubarikiwe sana
Huna lolote, unanataka kusema kufanya reallocation hakutakiwi kufuata sheria? Kwa hiyo hata usiku first lady akimwambia kijijini kwa wakwe zako madarasa ya shule hayatoshi basi akiamka ana allocate fedha za daraja Mtwara ziende huko na hadithi imekwisha? Mamlaka ya rais ni ya kisheria sio kimungu mkuu, panua akili
 
Mtu akikuambia jambo la kijinga na ukamwamini atakudharau- by JK Nyerere.
CCM imewaona wajinga sana baada ya kuwalisha uongo nanyi kama mazuzu mkaamini.
UKAWA hawajapinga kununua dawati au dawa, wao wanazungumzia taratibu kufuatwa kama sheria inavyosema tatizo likowapi?
Mbona mnaruhusu CCM iwadharau hivyo kwa kusadiki ujinga?
Tafuta hata wa bunge wa CCM wenye kujielewa watakufahamisha kuwa kuna makosa ila kwa vile hawaruhusiwi na chama chao kukosoa wanaumia moyoni tuu na kujiona watumwa
Haya mambo sijui ya utaratibu, mchakato, sijui nini, ndio yameifikisha nchi hii pabaya. UKAWA hamna jipya, kaeni kimya.
 
Ndio kupinga kwenyewe huko umeambiwa Pesa imeenda kununua dawati kwajili ya watoto wewe huridhishwi nini mana yake
Mbona wagumu kuelewa? Kinachopigiwa kelele sio sababu ya kuhamisha fedha bali utaratibu. Pesa ya serikali inatumika kwa kufuata sheria yake. Wewe zako binafsi mfukoni kama ulipanga kunywea beer lakini baadae ukaamua kununua chakula cha watoto hakuna wa kukuzuia, lakini fedha za umma ukibadili matumizi lazima ufuate sheria labda wakati wa hali ya hatari.
Sio sifa nzuri kwa kiongozi kutofata sheria hata kama jambo hilo afanyalo ni zuri
 
Kujadili kauli ya kada wa CCM bwana Benson Bana nayo ni kupoteza muda ,nikikumbuka namna alivyoonesha undumilakuwili wake ktk uvunjwaji wa Katiba /kanuni na Sheria za Nchi ktk Serikali ya Zanzabar pale alipokuwa ktk meza ya duara ktk idhaa ya kiswahili DW radio wakijadili uhalali au uharamu wa marudio ya Uchaguzi kule Zanzibar...sina hamu nae ,ni wale wale tu wanaofanya kazi kwa mzuk..a...
 
Wewe ndo jinga kubwa, hujui kucheza na siasa!
Ona sasa mlivyopuuzwa! Yaani mnadhani mnaweza kuubadili mtizamo wa umma kwa hoja hiyo ya kijinga!?

Kwa Mara nyingine tena, UKAWA mmejiingiza kwenye ujinga wa kiwango cha PhD! Mpigieni magoti Dr Slaa ndo alikuwa na akili za kutosha
huyo Bana atakuwa mchawi labda! amejuaje wako kimya huku bunge live halipo? amejuaje michango wakati jamii hairuhusiwi kiona?
 
Nimeanza kuona unafiki wa ukawa..unalalamika kwa fedha kupelekwa kwenye maeneo ya kuwajali wananchi...afya, barabara, elimu
Ungekuwa mfuatiliaji ungeelewa, kilocholamikiwa ni utaratibu uliyotumika, usiri kwa faida ya nani, ili iweje?
 
Kwa mwenendo huu tutakuwa na CCM imara sana na upinzani dhaifu sana! Wanajua fika kuwa kwa sasa CCM imeteka agenda zote na wao kubakia wakitapatapa!

Uchaguzi wa 2020 utakuwa nzuri sana kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani.
ndilo uliloliona katika hoja hiyo? Au ulikuwa nalo moyoni ukaona pa kulipachika ni hapo? Mbona halifit?
 
Ili tuweze kupiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni lazima wapinzani wawe na uzalendo na waache unafiki wa kuonewa huruma na mataifa ya nje kwa manufaa yao binafsi kwa kuleta migomo uchwara.Kwani kuna dhambi gani kwa pesa kwenda kutumika kwa manufaa ya wengi hata kama tena kwa maaumizi ya mkuu wa nchi.
Hivi ni wapinzani peke yako ndio wanatakiwa kuwa wazalendo?
 
Wabunge wengi wa upinzani mwaka 2020 wataamua kustaafu maana hawatakuwa na mashiko tena kwa serikali!
Eeee Mungu tusaidie watanzania, yaani mbunge anatakiwa awe na mashiko kwa serikali. Hiyo ndo kazi yake, wasipokua na mashiko wastaafu????
 
UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bungeni.

Hadhari hiyo imetolewa na wasomi na viongozi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, walipokuwa wakitoa maoni kuhusu uamuzi wa kambi hiyo kususa hotuba hiyo.

Dk Bana

Mhadhiri wa fani ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ndiye aliyesema kuwa kama uamuzi huo wa kuwa bubu bungeni hautabadilishwa, kambi hiyo itaonekana inalinda posho na kwamba haipo kwa ajili ya kutetea wananchi.

“Kazi yao ni kuwakilisha wananchi na makundi yote bungeni, sasa kitendo cha kuota ububu na kushindwa kueleza kero za wananchi, ni kutotendea haki wananchi maana ni vema wakae bungeni na kutoa hoja zao la sivyo, itafika wakati watatuomba radhi wananchi,” alisisitiza.

Akizungumzia hoja ya kwanza ya Mwenyekiti wa kambi hiyo, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kulalamikia muundo wa Serikali kutowekwa gazetini, Dk Bana alihoji kama Mbowe hajui kuwa muundo wa Serikali hautolewi kwa kila mtu.

Kuhusu suala la fedha zilizokatwa katika Mfuko wa Bunge na kuelekezwa katika utengenezaji wa madawati, Dk Bana aliwashangaa wawakilishi hao wa wananchi wanaopingana na uamuzi wa kumuinua mwananchi wa kawaida.

Alisema wananchi wote walipendezwa na hatua hiyo ya Serikali ya kuchukua fedha zilizotoka bungeni baada ya kubana matumizi na kupeleka katika kununua madawati.

“Hatua hii ni kielelezo kuwa Bunge lilikuwa likipangiwa fedha nyingi kuliko matumizi yake hivyo kusababisha kuwepo matumizi ya hovyo, sasa viongozi wa Bunge kuliona hilo na kurejeshwa kwenye jamii ni jambo jema,” alisema.

Alionya kuwa mikakati ya kambi ya upinzani, ni kutetea wananchi lakini kwenye hilo wananchi wenyewe kila kona wanawashangaa kwani inaonesha kutetea maslahi ya wabunge.

Bashiru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema wananchi wanaangalia vitendo vya wabunge wao ndani ya Bunge na watawahukumu kwani michango yao ndani ya Bunge ni muhimu na njia ya kutatua tatizo si kususa, bali kufuata taratibu za kisheria.

Alisema uamuzi wa kutozungumza, unaondoa maana ya vyama vya upinzani ndani ya Bunge kwa kuwa watashindwa kujadili masuala yenye manufaa ya wananchi, kwani mawazo ya kiongozi wa upinzani bungeni ni muhimu na yanawekwa kwenye kumbukumbu.

“Kuwekwa kwenye kumbukumbu mawazo hayo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo, sasa kitendo cha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kutumia vibaya nafasi anayopewa, ni udhaifu wa kimkakati,” alisisitiza Bashiru.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema wanavyofanya wapinzani ni jambo lisilopendeza katika kuleta umoja wa kitaifa, kwani wao ni wawakilishi wa wananchi ndani ya Bunge na kususa siyo jambo la kiungwana.
Dr Bana kutokuwepo mwongozo ni tatizo kubwa zaidi. Unataka watu waendelee kujindanganya na kudanganya wananchi kuwa yote yako sawa? Unaunga mkono serikali inapoendeshwa kiholela? Eti mwongozo ni siri; ya nani kwa faida ya nani?
 
Back
Top Bottom