“Wasiojulikana” washindwa kumfikia Lissu hospitalini

WALE wanaotajwa mara kwa mara kuwa ni “watu wasiojulikana” walikwama kumfikia na kumuua Tundu Lissu, akiwa amelazwa Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Taarifa za uhakika kutoka Nairobi zinaeleza kuwa vyombo vya usalama na walinzi waliokuwapo katika hospitali hiyo, walibaini mapema baadhi ya watu waliokuwa na kile kinachoitwa “nia mbaya kwa Lissu” na kuwadhibiti.

Habari hizi zimepatikana Tutakoma mwezi mmoja baada ya Lissu kuruhusiwa kutoka katika hospitali hiyo alimokuwa amelazwa kwa miezi minne akipatiwa matibabu, baada ya kujeruhiwa kwa risasi mjini Dodoma, Tanzania alikokuwa akiendelea na vikao vya Bunge la Jamhuri.

Lissu alilazwa kuanzia Septemba 7, mwaka jana na aliruhusiwa kutoka Januari 6, mwaka huu. Hivi sasa mbunge huyo Singida Mashariki (Chadema) anaendelea na matibabu jijini Brussels, Ubelgiji.

Ally Hemed, mmoja wa viongozi wa Chadema waliokuwa wakimuuguza Lissu kwa miezi hiyo, alithibitishia FikraPevu na kueleza kwamba majaribio hayo “yalizimwa” mapema.

“Napenda kukuhakikishia kuwa hapa kulikuwa na vita, hatukulala, maaskari hawakulala ili kuhakikisha usalama wa Lissu. Tulikuwa tunapata taarifa za kiintelijensia na kujipanga ili kuzuia lolote baya kutokea kwa Lissu akiwa hapa hospitali.

“Tulikuwa na uhakika kuwa waliopanga kumuua Lissu hawakufurahia uzima wake hapa hospitali, hivyo walikuwa tayari kummaliza ili kutimiza lengo lao kuu; kuua,” amesema Hemed.

Hemed ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uenezi wa Chadema, alisema pamoja kuhangaikia tiba na kupona kwake, nguvu nyingine ziliwekwa kuhakikisha usalama wake unakuwa imara.

“Hatukupata muda wa kupumzika, kila mara watu wa usalama walikuwa pamoja na sisi kuona hakuna upenyo wowote unapatikana kwa watesi wa Lissu kuja kummaliza,” amesisitiza Hemed.

Lissu anena

Alipoulizwa kuhusu usalama wake alipokuwa hospitali ya Nairobi, Lissu amesema hakuwa na wasiwasi sana kwa kuwa aliamini vipo vyombo vya usalama na watu waliokuwa wamejitoa kuhakikisha anakuwa salama.

“Sikuwa na shaka na timu ya walinzi na wana usalama waliowekwa kunilinda, tishio lazima lingekuwepo, kwamba wabaya wangu, waliotaka kuniua, wasingependa kuona naishi, hivyo lazima wangejaribu kuja kunimaliza nikiwa Nairobi.

“Lakini niko huku natibiwa, naamini kazi kubwa ilifanyika kwa hawa wanausalama wangu, kwa kweli nawashukuru sana.

“Nilisikia na kuelezwa kwamba kulikuwepo na mambo kadhaa ya hovyo, yaliyokuwa yakipangwa dhidi yangu, lakini Mungu ni mwema watesi wangu wameshindwa,” amesema Lissu.

Lissu amesema mauaji yaliyokuwa yakipangwa kwake yamejaa dhana ya kisiasa, jambo ambalo anaamini lisipopigiwa kelele sasa, litasambaa na kuwa jadi ili kuwatisha wale wenye mitazamo tofauti dhidi ya utendaji wa serikali na viongozi wake.

Mlinzi mkuu azungumza

Aliyetambulishwa kwa FikraPevu kuwa ni kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa Lissu, (jina lake halitajwi kwa sababu maalum) amesema anashangaa kuona Tanzania aliyoiacha Mwalimu Julius Nyerere inatoweka kwa kasi.

Kiongozi huyo alisema hakuwahi kusikia Tanzania inakuwa na kile alichookiita “vita ya siasa” kama Kenya, lakini jaribio la kuuwa kwa Lissu limemshitua na kushangaza Wakenya wengi.

“Sisi Kenya tuna vita kubwa ya kisiasa, lakini hatupigani marisasi (risasi), tunapingana tu na maisha ya wanasiasa na wafuasi wao yanasonga mbele, nyie mmeingiwa na mdudu gani watizedi (Watanzania),” alilalamika.

Anasema baadhi ya watu waliokuwa na nia mbaya na Lissu walidhibitiwa hata kabla ya kufika hospitali, wengine wakibainishwa kutoka mipaka waliyopitia.

“Hatukuwa na mchezo na uhai wa huyu mtu, tulijipanga vilivyo, kulikuwa na maelekezo kutoka juu, hivyo tuliweka mzizi mkubwa kumlinda mheshimiwa wenu,” ameongeza.

Zaidi, soma hapa => “Wasiojulikana” washindwa kumfikia Lissu hospitalini | FikraPevu
Viongoziwa awamu hii hawana dini kabisa japo majina yao yanafanana na waumin, Mashetani wakubwa
 
WALE wanaotajwa mara kwa mara kuwa ni “watu wasiojulikana” walikwama kumfikia na kumuua Tundu Lissu, akiwa amelazwa Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Taarifa za uhakika kutoka Nairobi zinaeleza kuwa vyombo vya usalama na walinzi waliokuwapo katika hospitali hiyo, walibaini mapema baadhi ya watu waliokuwa na kile kinachoitwa “nia mbaya kwa Lissu” na kuwadhibiti.

Habari hizi zimepatikana mwezi mmoja baada ya Lissu kuruhusiwa kutoka katika hospitali hiyo alimokuwa amelazwa kwa miezi minne akipatiwa matibabu, baada ya kujeruhiwa kwa risasi mjini Dodoma, Tanzania alikokuwa akiendelea na vikao vya Bunge la Jamhuri.

This is a bogus story. Hivi kusipokuwa na tukio lolote hamwezi kufanya siasa hadi muanze kutunga upuuzi kama huu? Very terrible politics of yours! Ninajiuliza maudhui ya manifesto yenu yatakavyokuwa 2020. Pole.
 
nasikia jitihada zinafanyika za kumtafutia uraia nje ya nchi!!! na jitihada zenyewe zinafanywa na Mange Kinambi
 
If Jah guides no one can destroy!
 
Hivu hawawezi msubiri arudi bongo wammalizee?
Kisha iweje? Itakuwaje kabla ya kurudi upigwe wewe risasi nyingi baada ya kufananishwa na jambazi sugu la magari ili yeye akirudi aje aweke maua juu ya shimo ulimofukiwa? Itapendeza sana siyo?
 
Intelijensia my foot,kwa nini haikugundua kuwa kuna wakora pale dodoma! Tusichoshane.
Soma vizuri uelewe hapo kuna kauli za maafisa ulinzi wa kenya waliokuwapo hapo kumlinda kwa maagizo kutoka mamlaka za juu kenya
 
Watakuwa wanajisikia vibaya sana mioyoni mwao
Hizo ni cheap propaganda, kama hao watu wasiojulikana bado wanamuhitaji si watamsubiri arudi alafu watekeleze. Kitu cha msingi tumuombe Mwenyezi Mungu amuepushe ndugu yetu na balaa zot zilizopo mbele yake.
 
This is a bogus story. Hivi kusipokuwa na tukio lolote hamwezi kufanya siasa hadi muanze kutunga upuuzi kama huu? Very terrible politics of yours! Ninajiuliza maudhui ya manifesto yenu yatakavyokuwa 2020. Pole.

..POLISI wanatakiwa wakamilishe uchunguzi haraka ili propaganda kama hizi zisipate nafasi.

..kwa mfano, nini kinawazuia Polisi kuwatambua wahusika wakati eneo aliposhambuliwa TL kulikuwa na cctv cameras?
 
Back
Top Bottom