“Wasiojulikana” washindwa kumfikia Lissu hospitalini

Haha! Waliwathibiti means wanawashilia? Au waliwathibiti kisha wakawaacha waende zao?

Hata baada ya kuwathibiti wanabaki kuwa wasiojulikana? Au wamejulikana sasa.

Haha.
 
Yaani! sijakuelewa mkuu,uwatukane halafu wakulinde!hilo hata malaika hafanyi. Mshauri tu apunguze ngenga atakula mema ya nchi.
Hata wauaji wanalindwa huko magerezani. Serikali ya JMT inatoa ulinzi kwa raia wake wote. Acha kupotosha.
 
wanamngoja akirudi

Nilishauri na nikasisitiza umuhimu na ulazima wa Mhe Lissu kutorudi Tanzania..
Wana magruzi wengi (hasa Afrika) walioleta mabadiliko makubwa kwenye nchi zao walikuwa wakimbizi wa kisiasa na walirejea muda muafaka toka ukimbizini.!!
 
Kama anawindwa kwa kiasi hicho unadhani hata akipona atakuwa salama? Labda aendelee kuishi huko huko alipo.
 
"Madaktari wa Serikali?" Drs wanawafanya kazi kwa nidhamu ya udaktari, kazi yao ilikuwa kuokoa maisha ya Mgonjwa wao, mtanzania mwenzao, acha kuligawa taifa kwa lugha yako ya ajabu ajabu, yaani wewe huna maana kabisa. acheni vyombo vya usalama vifanye kazi yao kwa tarifa iliyoletwa hapa, hii ni tarifa toka walinzi wa TL sasa ni kazi ya vyombo vyetu kufanyia kazi na kuja na ufafanuzi juu ya ukweli ama uongo wa tarifa hii.

mbogo31
Mkuu,
Hiyo taarifa unayoisubiria na nilichoandika hakina tofauti.

Wala sijagawa Taifa nimeonesha kuwa Serikali haihusiki na issue ya TL .

Zaidi ya hapo usinilishe maneno mkuu.
 
Waliomshambulia hawakuweka plan b kwa kuwa waliamini na kuwa na uhakika hawezi ku survive kwa sababu MVUA YA RISASI iliyotumika kumshambulia nivigumu kuamini kama ataishi tena.

Hivyo hata waliposikia bado anapumua na kakimbiziwa hospital ya Dodoma bado waliamini ni suala la kusubiri muda tu amalizike na ndio maana plan ya kuwatumia madaktari wammalize hawakuwa na shida nayo.

Ila walisahau kuwa anachokipanga M/Mungu mwanadamu hawezi kukipangua. Risasi 16 zilizoingia kwenye mwili wa Tundu hata tembo 20 au wanyama wakubwa wengine wowote 20 zinatosha kuwauwa.

M/Mungu ni mkubwa na nimuweza wa kila kitu.
 
Huo ni uongo.

Kama hiyo nia ya kummaliza TL ilikuwepo asingeondoka salama mikononi mwa madaktari waliokuwa wanampa huduma ya kwanza pale Dodoma.

Na kama TL na timu yake wanadai hivyo kuwa pana watu walikuwa wanamfatilia NBI basi Serikali haina mkono wake kwake mean that, ni maadui wa TL nje ya mfumo wa Serikali ndiyo wanaomwanadama.

Maana yake ni kwamba, wakati akiwa kwenye first aid pale Dodoma hao maadui wake ambao sasa hapa siyo serikali kama tunavyoaminishwa hawakuwa na agent wao maana pale walikuwepo wafanyakazi wa Serikali/madaktari wa Serikali.

Ila kama, tutaaaminishwa kuwa ni Serikali inahusika na masahibu yake basi hii nadharia inakuwa siyo sahihi kwa sababu madkatari wa Serikali ndiyo wameokoa uhai wake pale Dodoma.

Wakati mwingine tuache porojo.
 
WALE wanaotajwa mara kwa mara kuwa ni “watu wasiojulikana” walikwama kumfikia na kumuua Tundu Lissu, akiwa amelazwa Hospitali ya Nairobi, Kenya.
....
Hizi bandiko za shambulio la Mh Lissu hazina jipya. Kama ni kweli watu wasiojulikana bado wana nia ya kummaliza Mh Lissu, je, atakaporudi atakuwa salama kiasi gani? Je, kama ni kweli Serikali ina mkono wake, Mh Lissu atakapokuwa amerudi atakuwa salama?

Mh Lissu, kama raia yeyote ulinzi na usalama wake uko mikononi mwa Polisi na raia wema. Hivyo, siyo vyema kushabikia uhalifu kisiasa.
 
Kwa kweli!
 
Wasiojulikana wanatumika tu, wengi elim yao wameishia la 7, kwa lugha nyingine ni mbumbumbu wa kutosha ingawa wanamisuli lakini misuli ya ubongo hawana. Ona walivyomwaga risasi 38+ bila kuua hata nzi maanake weledi wao ni 0000%. Kuwatuma watu wa aina hii ni hatari unaweza ukajikuta wakikuanika hadharani bila kutegemea.
 
Halafu 100% ni wavuja jasho mkuu,ukiwadhulumu tu,wana ile style ya kumwaga mbogaukicheza nao dili walipe tu.!huwa hawaachi mtu salama.
 
Back
Top Bottom