“Wasiojulikana” washindwa kumfikia Lissu hospitalini

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
WALE wanaotajwa mara kwa mara kuwa ni “watu wasiojulikana” walikwama kumfikia na kumuua Tundu Lissu, akiwa amelazwa Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Taarifa za uhakika kutoka Nairobi zinaeleza kuwa vyombo vya usalama na walinzi waliokuwapo katika hospitali hiyo, walibaini mapema baadhi ya watu waliokuwa na kile kinachoitwa “nia mbaya kwa Lissu” na kuwadhibiti.

Habari hizi zimepatikana mwezi mmoja baada ya Lissu kuruhusiwa kutoka katika hospitali hiyo alimokuwa amelazwa kwa miezi minne akipatiwa matibabu, baada ya kujeruhiwa kwa risasi mjini Dodoma, Tanzania alikokuwa akiendelea na vikao vya Bunge la Jamhuri.

Lissu alilazwa kuanzia Septemba 7, mwaka jana na aliruhusiwa kutoka Januari 6, mwaka huu. Hivi sasa mbunge huyo Singida Mashariki (Chadema) anaendelea na matibabu jijini Brussels, Ubelgiji.

Ally Hemed, mmoja wa viongozi wa Chadema waliokuwa wakimuuguza Lissu kwa miezi hiyo, alithibitishia FikraPevu na kueleza kwamba majaribio hayo “yalizimwa” mapema.

“Napenda kukuhakikishia kuwa hapa kulikuwa na vita, hatukulala, maaskari hawakulala ili kuhakikisha usalama wa Lissu. Tulikuwa tunapata taarifa za kiintelijensia na kujipanga ili kuzuia lolote baya kutokea kwa Lissu akiwa hapa hospitali.

“Tulikuwa na uhakika kuwa waliopanga kumuua Lissu hawakufurahia uzima wake hapa hospitali, hivyo walikuwa tayari kummaliza ili kutimiza lengo lao kuu; kuua,” amesema Hemed.

Hemed ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uenezi wa Chadema, alisema pamoja kuhangaikia tiba na kupona kwake, nguvu nyingine ziliwekwa kuhakikisha usalama wake unakuwa imara.

“Hatukupata muda wa kupumzika, kila mara watu wa usalama walikuwa pamoja na sisi kuona hakuna upenyo wowote unapatikana kwa watesi wa Lissu kuja kummaliza,” amesisitiza Hemed.


Lissu anena

Alipoulizwa kuhusu usalama wake alipokuwa hospitali ya Nairobi, Lissu amesema hakuwa na wasiwasi sana kwa kuwa aliamini vipo vyombo vya usalama na watu waliokuwa wamejitoa kuhakikisha anakuwa salama.

“Sikuwa na shaka na timu ya walinzi na wana usalama waliowekwa kunilinda, tishio lazima lingekuwepo, kwamba wabaya wangu, waliotaka kuniua, wasingependa kuona naishi, hivyo lazima wangejaribu kuja kunimaliza nikiwa Nairobi.

“Lakini niko huku natibiwa, naamini kazi kubwa ilifanyika kwa hawa wanausalama wangu, kwa kweli nawashukuru sana.

“Nilisikia na kuelezwa kwamba kulikuwepo na mambo kadhaa ya hovyo, yaliyokuwa yakipangwa dhidi yangu, lakini Mungu ni mwema watesi wangu wameshindwa,” amesema Lissu.

Lissu amesema mauaji yaliyokuwa yakipangwa kwake yamejaa dhana ya kisiasa, jambo ambalo anaamini lisipopigiwa kelele sasa, litasambaa na kuwa jadi ili kuwatisha wale wenye mitazamo tofauti dhidi ya utendaji wa serikali na viongozi wake.


Mlinzi mkuu azungumza

Aliyetambulishwa kwa FikraPevu kuwa ni kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa Lissu, (jina lake halitajwi kwa sababu maalum) amesema anashangaa kuona Tanzania aliyoiacha Mwalimu Julius Nyerere inatoweka kwa kasi.

Kiongozi huyo alisema hakuwahi kusikia Tanzania inakuwa na kile alichookiita “vita ya siasa” kama Kenya, lakini jaribio la kuuwa kwa Lissu limemshitua na kushangaza Wakenya wengi.

“Sisi Kenya tuna vita kubwa ya kisiasa, lakini hatupigani marisasi (risasi), tunapingana tu na maisha ya wanasiasa na wafuasi wao yanasonga mbele, nyie mmeingiwa na mdudu gani watizedi (Watanzania),” alilalamika.

Anasema baadhi ya watu waliokuwa na nia mbaya na Lissu walidhibitiwa hata kabla ya kufika hospitali, wengine wakibainishwa kutoka mipaka waliyopitia.

“Hatukuwa na mchezo na uhai wa huyu mtu, tulijipanga vilivyo, kulikuwa na maelekezo kutoka juu, hivyo tuliweka mzizi mkubwa kumlinda mheshimiwa wenu,” ameongeza.


Zaidi, soma hapa => “Wasiojulikana” washindwa kumfikia Lissu hospitalini | FikraPevu
 
Kumbe unajua kuwa polisi na tiss wetu hawana uwezo wa intelejensia ya kugundua watu wenye nia ovu ila wana intelejensia ya kuzuia mikutano ya upinzani wa Kweli, acha sasa kujitoa ufahamu
Yaani! sijakuelewa mkuu,uwatukane halafu wakulinde!hilo hata malaika hafanyi. Mshauri tu apunguze ngenga atakula mema ya nchi.
 
Mtoa uzi hamaanishi intelijensia ya chadema, anamaanisha intelijensia kutoa kwa jeshi la polisi ka kenya. Hebu tuambie kwanini intelijensia ya polisi wa Tz haikufanya kazi kule Dodoma?
Kwani Kenya imezaliwa leo?ilipaswa kumlinda hata huko dodoma kwa kuwa anaiamini zaidi ya mama yake.
 
Back
Top Bottom