Wasifu(CV) ya Jenerali Ulimwengu

Wasifu(CV) ya Jenerali Ulimwengu

Uzi ulitulia huu enzi hizo memba wengi hawana mihemko mikubwa naupambe. Leo umefukuliwa ukisoma kila thread unakuta mwandishi kaongea ukweli wa akijuacho.
 
Hakuna ubishi kuhusu elimu ya juu, uelewa mkubwa na uzalendo wa Jenerali Ulimwengu. Na mara nyingi ni mkweli. Lakini ni binadamu, naye huongozwa na hisia binafsi wakati mwingine. Kwa mfano, kumsakama sana Mkapa (ambaye alikuwa na upungufu wa ujeuri kama wa Jenerali) ni kwa kuwa hakuzawadiwa cheo alichokitaka serikalini baada ya kushiriki kampeni vyema. Alipoendelea kumsakama, ndipo wabaya katika system wakaleta hoja ya uraia wake. Technically, kwa sheria ya uraia wa wakati ule, Jenerali, Bandora na wengine hawakuwa raia kwa kuwa hawakuzaliwa Tanganyika. Walizaliwa Rwanda, wakaja nchini wakiwa wadogo. Watu wengi wa mipakani, hata wa ndani sana kama maeneo ya Tabora (kwao Bandora) kulikokuwa na wahamiaji wengi, hasa wakimbizi wa nyakati za ukoloni, hawakuwa raia technically. Ilitakiwa warasimishe kwa kupata uraia wa kujiandikisha. Familia za kisomi mijini zenye utata huu huenda zilirekebisha haya, lakini haikuwa rahisi kwa familia ya kawaida kufanya hivyo, matokeo yake kwenye siku mbaya yakatokea ya akina Jenerali na Bandora. Wenye umri mkubwa mtakumbuka kuwa kwa sheria ile, ili kupata pasipoti ilibidi uonyeshe uraia wa Tanzania wa wazazi wako au upate mzee wa kula kiapo kuwa alishuhudia wazazi wako WAKIZALIWA. Sijui kama mnakumbuka jinsi Azim Premji alivyokosa uraia na kuvuliwa ubunge kwa sababu tu baba yake hakuwahi kukana uraia wa India, shitaka aliloshinda Dr. Walid Aman Kaborou wa CHADEMA. Ukisumbua, watu wa system, lakini hata washindani wako wengine kama wa kisiasa wa Premji, wanakupiga pale ulipo na kasoro hata usiyoijua. Jenerali, Bandora, Premji walirekebisha kiliechotakiwa, na sheria ile pia imerekebishwa kiasi. Wote wapo nchini na ni raia.
J
Huyo ni Ghadafi mkuu?
Ndio
 
Tunajidhalilisha sana kufikiria watu wote wenye akili kubwa za kuhoji mambo hawawezi kuwa Watanzania.
Povu mnatoa nyie wenye roho mbaya, mmekalia kuwavua uraia Watz wenzenu. Tena bila haya, miongoni waliomuunga mkono Kabila ni Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere, mbona yeye hujamtaja. Moja ya tatizo letu kubwa, tukitofautiana na mwenzetu kimawazo, na hasa ukikuzidi uwezo wa kiakili. Badala ya kujifunza kutoka kwake, unavua uraia. Dunia ilitusuta kwa kumvua uraia Jenerali Ulimwengu na kumfanya stateless, wakaona aibu wakamrejeshea uraia wake. Leo nawe unakuja na ujinga ule ule wa kumvua uraia. Kazaliwa Tanzania, kakulia Tanzania, kazeekea Tanzania. Acheni roho mbaya
 
Ningependa kujua wasifu mdogo wa Jenerali Ulimwengu kwani nimefurahia uzalendo aliouonesha kuwa pale Mahakamani katika kesi ya Katiba.

Kitaaluma nilikuwa namtambua Jenerali kama mwandishi sio mwanasheria. Nasikia pia alishakuwa mwakilishi wa Tanzania makao makuu ya umoja wa vijana huko Algeria, pia ni mmoja wa vijana waliolelewa na umoja wa vijana wa Tanu na ni muumini mkubwa wa sera za Mwalimu Nyerere ya siasa ya ujamaa na kujitegemea.

----- Michango kutoka kwa WanaJF-----

JENERALI ULIMWENGU was born on 4th April 1948 in Ngara, Kagera Region of Tanzania. He went to school in Kamachumu, Katoke and Nyakato in Kagera and high school in Tabora from 1955 to 1968 and was a student of the then University of East Africa from 1969 to 1972. As a post-Arusha Declaration student at the premier academic and activist University, Ulimwengu was one of the activist radical students espousing progressive causes of African liberation and human emancipation. After leaving the University, he became an active member of the ruling party, then TANU (Tanganyika Afican National Union) and later CCM ('Chama cha Mapinduzi') as the following brief profile of his post-student service shows.
IMG-20211113-WA0002.jpg
 
Ilikuaje mtu asiye raia wa Tanzania akashika nafasi nyeti za uongozi katika nchi, bunge, serikali na chama, ndani na nje ya nchi kwa muda mrefu hivyo???
Hakuna ubishi kuhusu elimu ya juu, uelewa mkubwa na uzalendo wa Jenerali Ulimwengu. Na mara nyingi ni mkweli. Lakini ni binadamu, naye huongozwa na hisia binafsi wakati mwingine. Kwa mfano, kumsakama sana Mkapa (ambaye alikuwa na upungufu wa ujeuri kama wa Jenerali) ni kwa kuwa hakuzawadiwa cheo alichokitaka serikalini baada ya kushiriki kampeni vyema. Alipoendelea kumsakama, ndipo wabaya katika system wakaleta hoja ya uraia wake. Technically, kwa sheria ya uraia wa wakati ule, Jenerali, Bandora na wengine hawakuwa raia kwa kuwa hawakuzaliwa Tanganyika. Walizaliwa Rwanda, wakaja nchini wakiwa wadogo. Watu wengi wa mipakani, hata wa ndani sana kama maeneo ya Tabora (kwao Bandora) kulikokuwa na wahamiaji wengi, hasa wakimbizi wa nyakati za ukoloni, hawakuwa raia technically. Ilitakiwa warasimishe kwa kupata uraia wa kujiandikisha. Familia za kisomi mijini zenye utata huu huenda zilirekebisha haya, lakini haikuwa rahisi kwa familia ya kawaida kufanya hivyo, matokeo yake kwenye siku mbaya yakatokea ya akina Jenerali na Bandora. Wenye umri mkubwa mtakumbuka kuwa kwa sheria ile, ili kupata pasipoti ilibidi uonyeshe uraia wa Tanzania wa wazazi wako au upate mzee wa kula kiapo kuwa alishuhudia wazazi wako WAKIZALIWA. Sijui kama mnakumbuka jinsi Azim Premji alivyokosa uraia na kuvuliwa ubunge kwa sababu tu baba yake hakuwahi kukana uraia wa India, shitaka aliloshinda Dr. Walid Aman Kaborou wa CHADEMA. Ukisumbua, watu wa system, lakini hata washindani wako wengine kama wa kisiasa wa Premji, wanakupiga pale ulipo na kasoro hata usiyoijua. Jenerali, Bandora, Premji walirekebisha kilichotakiwa, na sheria ile pia imerekebishwa kiasi. Wote wapo nchini na ni raia.
 
Ni Mnyarwanda na alinyang'anywa uraia wa Tanzania yeye na akina Balozi Bandora, Castico, nk. Nadhani hakurudishiwa na kwa sasa anafanya kazi kama mgeni.

Ni mwandishi wa Habari na pia miaka kama mitatu nyuma alitunukiwa u advocate. Amewahi kuwa TYL na akawa mwakilishi wa Tanzania kule Algiers.

Amewahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati ule wa kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa.

Wakati vyama vingi vinaanzishwa kulikuwa na sheria kwamba ukitaka kufanya maandamano ama mikutano unaomba kibali kwa mkuu wa wilaya. Basi huyu bwana alikuwa hana hiyana ya kutoa vibali kwa vyama.

Akahamishwa kupelekwa Singida kama mkuu wa Wilaya. Kama sijasahu hakwenda Singida badala yake akajiuzulu ukuu wa Wilaya.

Huyo ndiye Generali Twaha Ulimwengu.
Hii sasa ni kachumbari umeanza kusema ni mnyrwanda alafu alikua mbunge wa kuteuliwa, mkuu wa wilaya ilala etc..
Sasa mnyarwanda gan anakua dc, mbunge, mwakilishi wa TANU?
Hii inaonyesha wazi kuwa hatutafakar kablya ya kuandika jambo..!!
Mnyrwanda ni mtu gan? Labda tuanzie hapo
 
Kwa kukusaidia ipo hivi..
Mnyarwanda ni raia wa nchi iitwayo Rwanda, so automatically Jenerali Ulimwengu sio mnyrwanda kwa sababu sio raia wa Rwanda!!sema wew umechanganya kuwa inawezekana akawa na asili ya ututsi, lkn ututsi haimaanishi ni unyarwanda,ututsi ni kabila na urwanda ni utaifa vitu viwili tofauti.. Uganda kuna kabila la wanyankole ni asili moja na tutsi,
Na asili ya hizo kabila mbili sio rwansa wala uganda ni huko juu habesh huko Ethiopia, Somalia, sudani hukooo.. Sawa na wamasai, na almost kabila nying za Arusha,Manyara, na mikoa jirani...
Wabantu pia ni migratory society, na wao asili zao wanajua!!
Unaijua asili ya Baba wa Taifa? Ukiijua ndo povu litakukauka mdomoni
 
Hii sasa ni kachumbari umeanza kusema ni mnyrwanda alafu alikua mbunge wa kuteuliwa, mkuu wa wilaya ilala etc..
Sasa mnyarwanda gan anakua dc, mbunge, mwakilishi wa TANU?
Hii inaonyesha wazi kuwa hatutafakar kablya ya kuandika jambo..!!
Mnyrwanda ni mtu gan? Labda tuanzie hapo
Fuatilia historia, haya maneno hayatoki kinywani mwangu yalitoka serikalini na akapokwa uraia na kuambiwa ni Mnyarwanda. Hakuwa peke yake alikuwepo pia Balozi Bandora tena yeye alipokwa uraia akiw balozi kule Lagos ama baada tu kidogo ya kuwa amerejeshwa.
Kwani mtu kuwa DC ama Mbunge kunazuia kupokwa uraia?
 
Mkuu na wewe umeamua kuongopa? Jenerali alinyang'anywa uraia lakini baadaye akaomba na kupewa.

Sababu za kunyang'anywa nina imani unazijua. Jenerali ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

Mtu yeyote ambaye wakati Tanganyika inapata uhuru alikuwa ndani ya Jamhuri, ni raia.

Jenerali amezaliwa Tanganyika. Kama suala ni kuwa ana asili ya Nchi jirani, basi mamilioni ya Watanzania si raia.
Upo sahihi mkuu kuhusu mtu kuzaliwa Tanzania kabla ya uhuru kuwa Mtanzania ila hii ilikuwa kwa wale wote waliokuwa jinsi ya mkoloni mwingereza na ndio sababu huwezi kuta mtu mwenye wazazi wenye asili ya Kenya, Uganda, Malawi na Zambia wanapingwa zengwe ila waliozaliwa kabla ya uhuru ila wana vinasaba na Burundi, Rwanda na Kongo ambazo kihistoria hazikuwa chini ya Uingereza walitakiwa kufuata taratibu flani flani kukamilisha mambo yao na bahati mbaya wanasiasa wetu huwa wanatumia vipengele hivyo kuwatoa watu relini lakini ukweli ni kwamba walitakiwa kuwaambia tu kuna vitu havipo sawa embu weka sawa vielelezo vyako
 
Fuatilia historia, haya maneno hayatoki kinywani mwangu yalitoka serikalini na akapokwa uraia na kuambiwa ni Mnyarwanda. Hakuwa peke yake alikuwepo pia Balozi Bandora tena yeye alipokwa uraia akiw balozi kule Lagos ama baada tu kidogo ya kuwa amerejeshwa.
Kwani mtu kuwa DC ama Mbunge kunazuia kupokwa uraia?
System inaruhusu je mtu asiyekua mtanzania kuwa kiongozi wa serikali na sector muhimu kabisa za serikali? Dc ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya husika, inakua mgeni anahusika kwenye usalama wa nchi yetu haliyakua wapo Watanzania wengi lkn hawapewi nafasi hiyo wanapewa wageni?
 
Hata wew leo hii ukiwa kinyume na watawala, utaambiwa sio mtanzania!!
System ipo hivo kila mpinga system sio mtanzania
 
Ni Mnyarwanda na alinyang'anywa uraia wa Tanzania yeye na akina Balozi Bandora, Castico, nk. Nadhani hakurudishiwa na kwa sasa anafanya kazi kama mgeni.

Ni mwandishi wa Habari na pia miaka kama mitatu nyuma alitunukiwa u advocate. Amewahi kuwa TYL na akawa mwakilishi wa Tanzania kule Algiers.

Amewahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati ule wa kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa.

Wakati vyama vingi vinaanzishwa kulikuwa na sheria kwamba ukitaka kufanya maandamano ama mikutano unaomba kibali kwa mkuu wa wilaya. Basi huyu bwana alikuwa hana hiyana ya kutoa vibali kwa vyama.

Akahamishwa kupelekwa Singida kama mkuu mwenye nada anataka CV hajauliza uraia wake soma dada usikurupuke
Povu mnatoa nyie wenye roho mbaya, mmekalia kuwavua uraia Watz wenzenu. Tena bila haya, miongoni waliomuunga mkono Kabila ni Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere, mbona yeye hujamtaja. Moja ya tatizo letu kubwa, tukitofautiana na mwenzetu kimawazo, na hasa ukikuzidi uwezo wa kiakili. Badala ya kujifunza kutoka kwake, unavua uraia. Dunia ilitusuta kwa kumvua uraia Jenerali Ulimwengu na kumfanya stateless, wakaona aibu wakamrejeshea uraia wake. Leo nawe unakuja na ujinga ule ule wa kumvua uraia. Kazaliwa Tanzania, kakulia Tanzania, kazeekea Tanzania. Acheni roho mbaya

wa Wilaya. Kama sijasahu hakwenda Singida badala yake akajiuzulu ukuu wa Wilaya.
Huyo ndiye Generali Twaha Ulimwengu.
Mwenye nada anauliza CV hajauliza swala la uraia wake. Some I kwa weledi muelewe siyo kujibu kinyume. Seals la uraia hata wewe hatuna uhakika na uraia wako.
 
Baada ya rai wakaanzisha mtanzania na mfadhili wao mkuu aliyetoa kila kitu ni rostam aziz kwahiyo huyo jenerali msimuamini sana njaa ikizidi ndio anajitia kupinga

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Baada ya Kampuni ya Habari Corporation kuanza kuyumba wakaiuza kwa Rostamu na Bashe akawa Mtendaji Mkuu...
 
Back
Top Bottom