jameni hebu nisaidieni kuna uhusiano wowote kati ya uwezo wa mtu darasani na uwezo na umakini wake kwenye uongozi?
mana kumekuwa na watu wengi wengi ambao wamekuwa wakifanya harakati za chini chini za kuutaka Urais wa nchi yetu. wengine tunawafahamu namna ambavyo hawako makini toka utotoni mwao, hivi ikitokea kweli wakawa tutakuwa tunalipeleka wapi taifa letu? mfano ni hizi harakati za chini chini zinazofanywa na mbunge wa bumbuli, mh januari makamba ambaye anajipanga kugombea kwa kufanya mikutano ya hapa na pale na pia kujinadi ili kujitia umaarufu kwa wananchi na haswa kupitia ujana wake na kiu ya mabadiliko iliyopo nchini. hapa ofisini kwetu kuna mtu alisoma na huyu mheshimiwa. baada ya mimi kusoma post ya hawa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa JF niliwashirikisha wenzangu nikiwaambia kuwa katika wabunge vijana huwa namfagilia sana Januari kwa namna anavyoonesha weledi kwenye kazi zake. ndipo jamaa akasema kuwa huyo hana kitu sababu alifeli kidato cha nne na cha sita na kutumia hela za usalama wa taifa kwenda kusoma nje kwa ushawishi wa baba yake mzee makamba. jamaa akathibitisha kuwa alisoma naye form six pale forest hill na kwamba januari makamba alipata division zero. kauli hii ilinishtua sana na kuniakatisha tamaa kabisa ndipo nikaamua kuwauliza hapa hivi akifanikiwa kuingia ikulu huyu itakuwaje?
We jamaa bana. Umesema kwamba mtu kaiba mitihani. Then unasema unless he comes out clean.
Basi sawa
==>> January Makamba like father like son...wote hovyo hovyo....
==>> F4 kafutiwa matokeo Div 0 kwa wizi wa exams Galanos...
==>> F6 Div 0 Forest hill...
===>> Na ukitaka kujua January ni KILAZA...has too
low IQ & EQ....he used to popularize himself kwa kuwanunua VIJANA WALIO KATIKA UONGOZI WA VIKUNDI fulani fulani...mfano...hao wa VYUO VIKUU OF
WHICH, nao bila aibu wameuzika .... so January hana kitu, sifa na sio intellectual wa kitu chochote zaidi ya KUSOMEA USULUHISHI WA MIGOGORO TU NJE OF WHICH sio issue...
==>> January hajijui....but he pretends to know kweli
kweli....& like anatumia akili kweli kweli KUHUSU DIFFERENT ISSUES....huyu MWEUPE KABISA ....
==>> URAIS labda wa nyumbani kwao...yeye na bumbuli yake....A DAY DREAM....
==>> January kila siku akiamka ANATAKIWA AMSHUKURU JK....hadi kufa....amwone Mungu wake wa pili..
Una tatizo la msingi katika fasihi andishi!
Kama una ushahidi tuwekee, tuache kuendeleza mapambio ya mitaani yanayoibuliwa na kuenezwa na watu waliokosa hoja za ushindani.
Nilitaka kusoma reply Zote mpaka Mwisho lakini hii imenifanya niseme nijuavyo kuhusu January. Alimaliza kidato cha nne Forest hill sec school mwaka 1993 na alipata div 4, Forest ilikuwa inamitaala mingi ya comarce yeye alikuwa com 1 ambayo ndo waliwekwa walio vizuri class. Baada ya forest sijui alikwenda ila naamini a Rudia mitihani ya kidato cha nne kitu ambacho ni kawaida sana kwa mtu asiye kata Tamaa kutimiza malengo yake ya maisha. Naamini hata Hapa JF kunawengi wamerudia mitihani kwa kutoridhika na elimu ya kidato cha nne. Kwalolote alilofanya hakupenda kubaki na elimu ya kidato cha nne. Kwahiyo ukweli ni kwamba January hakupata div 0 kwenye sitting yake ya kwanza Bali ni div 4, maelezo hapo juu ni sahihi Kama alipohamia Forest hill form 3 hakuwa amefanya mtihani shule nyingineThis Forum seems to have officially been converted into a gossiping place. What's worse, those who are supposed to preserve its reputation appear to either be fast asleep or are themseleves part of the campaign to destruct what was once the most credible and respectable site.
January Makamba didn't score Division 0 in his A-level final exams as the person who made this post attempts to make us believe. The truth is that he scored an impressive Division 1, with his headmaster decribing him as one of the most talented students his school had ever had. He even presented him with the job of teaching Geography at the school during the gap year, but January reportedly turned the offer down because he wanted to work at refugee camps.
It's hard to see what might have motivated anyone to post an information as maliciously wrong as this one. But it also raises concerns that moderators are doing nothing about it.
Yaani kuwa secretary wa rais tu na yeye anataka kuwa rais.jimbo lenyewe limemshinda analiongoza kwa twiter nchi si ataiongoza kwa instagram!
Jamaa Kaandika hivi Kwenye Website yake (January Makamba)
"So, we did our exams and the day to go and look for the result came. And, to the shock of friends and family and teachers, my name was not there in the results sheet. I felt like collapsing. I went to another result centre thinking that there was a mistake again, nothing. Inquiries to the reasons were not responded to immediately. Later we learnt that I was mistakenly linked to a cheating scam that one of the teachers was involved in. I was a pawn in a terrible mistake. A really long and painful story. So, what was the alternative? To resit the exams. I quickly registered as private candidate and pursued High School studies at Forest Hill High School on a tentative basis while resitting so that when I get my results I can proceed on to Form Six. It was such a task, but I succeeded"
Bado najiuliza, kama kweli alisingiziwa, kwa nini hakuruhisiwa kupewa majibu yake na badala yake akatafuta alternative?? Manake, kwa connections zile na kama kweli alikuwa ameonewa, sidhani kama majibu yake yasingetolewa, Tafakari!
Eti anaropoka "Upinzani hakuna mwenye sura ya urais". Simcard imemshinda ataweza kukabiliana na mikataba ya Nyuklia?Ushamba tu.
By the way,huwezi kusomea shahada ya conflict resolution kama una akili timamu.Je,Migogoro ikiisha utafanya nini?Utafitini na kuomba watu wagombane?Ndiyo future hii?Je,taaluma hii isingesaidia usuluhishi na mzee shelukindo huko Bumbuli?Conflict haihitaji digrii bali busara na kujitambua tu.Kwani wafalme wetu miaka ya zamani waliwezaje kutatua migogoro?Only,Weak Creatures watafanya promotion ya taaluma hii na kujisifia kwa vyeti na majoho.
Mkuu wewe mwenyewe umekiri kuwa unamfagilia lakini kusikia ati kapata division zero unaonekana kuhoji tena uwezo wake! Usingepata hiyo habari basi ungeendelea kumkubali? Kama ni ufaulu wa darasani basi nchi zingekuwa zinaongozwa na maprofessor.
Siasa tuache pembeni.
Hayo ya daraja sifuri kidato cha nne au cha sita hayana uhusiano wa moja kwa moja na maswala ya uongozi.
Profesa Abdoulaye Wade ambaye amepata kuwa rais wa Senegal ni moja ya marais wasomi wa Afrika waliowahi kushika nafasi hiyo pia Profesa Bingu wa Mutharika aliyetawala Malawi.Utawala wao haukuakisi uprofesa wao na kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya wananchi wa nchi zao.
Katika orodha hiyo, mfano mdogo hapa Tanzania kwa kutumia kipimo cha madaraja kwa kidato cha nne na sita, Dk. Cyril Chami, aliyepata kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko katika Awamu ya Nne,anatajwa kuwa moja ya wanafunzi bora kutokea nchini, Kidato cha Nne-Daraja la Kwanza Alama 7 (Div.I.7) na Kidato cha Sita-Daraja la Kwanza Alama 3(Div.I.3).Chuo Kikuu-First Class. Pamoja na matokeo yake hayo, wizara bado ilimshinda kuongoza.
Fundisho: Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa maswala ya utawala na uwezo wa darasani.Isipokuwa elimu nzuri ya jumla inaweza kumsadia mtawala kuwa na upana wa uelewa wa ulimwengu unaomzunguka.
Busara.Hekima.Kuwajibika.Nidhamu.Kujitambua kwamba yeye ni mwajiriwa wa wapiga kura wake,hayo na mengine yanaweza kumfanya kuwa kiongozi bora.
Hitimisho:Januari Makamba au yeyote yule anaweza kufaa au asifae iwapo hatokuwa na maono katika nia yake ya kutaka kuwa rais wa nchi yetu tukufu.Wengine wanataka sifa tu, awe magogoni, kila kitu chake.Asafiri atakako,kwa kutaja machache. (Haya ni maoni yangu tu,sio msahafu huu!)
Dr Cyril Chami hakushindwa mkuu ni siasa tu......