Wasifu (CV) wa January Makamba

NOT FOUND

Senior Member
Mar 14, 2011
157
0
wakuu ningependa kufahamu maelezo (cv) ya mbunge januari makamba.

Kuanzia elimu yake, (na alama alizopata) na maisha yake kwa ujumla.

Na ni sifa gani ya pekee ambayo ilimfanya apate nafasi ya kuwa msaidizi wa j.k (2005 -2010)

Inasemekana jamaa anaandaliwa kuja kuwa president wa Tanzania.

==================
Katika Interview akijibu mwenyewe:
Swali: Tungeanza na wewe kutupa historia yako (Elimu, Kazi, Maisha kwa ujumla):

J. Makamba:
Nilizaliwa tarehe 28 Januari 1974. Nalipenda sana jina langu kwasababu mara nyingi ninapojitambulisha kwa watu, automatically linaanzisha mazungumzo. Mara nyingi huulizwa kama nilizaliwa mwezi Januari ndio maana nikapewa jina hilo. Ukweli ni kwamba hiyo sio sababu per se. Sababu kubwa ni kwamba, wakati nazaliwa, Mzee wangu alikuwa na rafiki yake mkubwa aliyempenda sana aliyeitwa Januari. Akaamua kunipa jina lake kwa mapenzi yake kwa rafiki yake. Ilikuwa ni coincedence tu kwamba nilizaliwa mwezi wa kwanza. Lakini jina ambalo Babu yangu mzaa baba alinipa na alipenda kuniita kabla hajafariki mwaka 1984 ni Rajab, ambalo ni jina lake yeye. Kwahiyo hadi leo, kijijini kwetu Mahezangulu, Lushoto, hasa kwa wale wazee wa kule, na hata kwa bibi yangu, najulikana kama Rajab.

Nimesoma kwenye shule mbalimbali za msingi katika mikoa mbalimbali nchini, kadri wazazi wangu walivyohama kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine. Nilianzia Monduli mwaka 1981. Mwaka 1983, nikapelekewa kukaa na bibi mzaa mama kijijini Kituntu, karibu na Kyaka, Bukoba Vijijini. Mama yangu kwao amezaliwa peke yake, kwahiyo bibi alihitaji mjukuu wa kukaa naye kumsaidia. Ndio nikatolewa kafara. Hahahaha! Kwahiyo darasa la tatu, la nne na la tano, nimesoma kijijini. Siwezi kusahau maisha yale: asubuhi ni kupiga umande literally kwenda shule umbali wa kama kilomita nne na nusu hivi kutoka nyumbani, ukirudi saa tisa ni kwenda kuchunga mbuzi, ukisharudisha mbuzi zizini saa kumi na mbili jioni ni kwenda kuchota maji mtoni, usiku kazi ni kumsaidia bibi kuuza pombe ya ndizi inayoitwa lubisi (bibi alikuwa na kilabu maarufu pale kijijini).

Samahani hapa nime-digress kidogo kwa kukumbuka na kuelezea zaidi kipindi hiki. Lakini experience hii ni sehemu ya mimi. Siku hizi NGOs zinayaita haya "mazingira hatarishi", lakini watoto wengi vijijini ndio maisha yao ya kila siku. Some make it, through pure luck or strength of character, some don't.

Anyway, nilirudi kukaa na wazazi wangu tena wakiwa Lushoto kwahiyo nikasoma darasa la sita pale, Shule ya Msingi Kitopeni, na kwenda kumalizia darasa la saba shule ya Msingi Masiwani Tanga Mjini. Hapa Tanga Mjini niliingia na kusoma madras which was quite rewarding ingawa sikumaliza msahafu. Pamoja na kuhamahama, na dhahama za maisha ya kijijini, I have always done well in school. Sikumbuki kama nilishawahi kushuka chini ya nafasi ya nne.

Form one nilisoma Handeni Secondary School, hii ilikuwa ni shule mpya, sisi tulikuwa Form One ya pili – kulikuwa hakuna walimu, madawati, maabara, n.k. Form Two hadi Form Four nikasoma Galanos, Tanga Mjini. Wakati nikiwa Form Three nilichaguliwa Deputy Head Prefect pale Galanos. Form Five na Six nikawa Forest Hill Secondary School, Morogoro, ambapo siku ya graduation nilitunikiwa cheti cha Overall Best Student.

Anyway, wakati nasuburi kwenda university, nikaenda kutafuta kazi kwenye kambi za wakimbizi Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma. Nikafanikiwa Kasulu. Ukiacha maisha ya kijijini na bibi, this was another rewarding experience kwenye maisha yangu. Nilipata responsibilities kubwa kadri muda ulivyoenda, hadi kufikia ngazi ya Assistant Camp Manager kwenye kambi ya Mtabila Extension au Mtabila II, ambayo literally niliianzisha mimi (baada ya kuwa Serikali imetoa eneo) from the scratch kwa maana ya kusimamia ujenzi wa infrastructure za kambi na kugawa plots kwa wakimbizi. Kwenye kazi hii ndipo kwa mara ya kwanza nilipokutana na kuanza ku-engage na kujenga urafiki na watu wa mataifa mbalimbali waliokuwa expatriates kwenye camps. Muda wa kwenda Chuo ulivyofika, sikwenda kwani nilinogewa na kazi, mwaka uliofuatia sikwenda tena kwani nilipata responsibilities kubwa zaidi kambini and I was making and saving good money.

Eventually nikapata Chuo Marekani. Nilianza Boston baadaye nikajiunga na St. John's University, Minnesota. Hiki ni Chuo cha Wakatoliki Wabenedicto kilichokuwa katikati ya pori na lakes, a very beautiful and quiet place, katikati ya Jimbo la Minnesota. Pale, degree niliyochukua ni BSc in Peace and Conflict Studies. Niliamua kusoma hii kozi kutokana na experience yangu kwenya makambi ya wakimbizi. Nilitaka kuelewa ni kwa namna gani tunaweza kuzuia watu wasikimbie kabisa nchi zao, kwani maisha ya ukimbizi, kwa nilivyoyaona, ni ya udhalilishaji mkubwa sana na yanaondoa dignity ya mtu.

Wakati nikiwa St. John's University, nilirudi tena kufanya research yangu na UNHCR kwenye makambi ya wakimbizi Kasulu na Kibondo lakini pia kwenye way stations ndani ya Burundi na DRC.

Baada ya kumaliza St. John's, nikapata research assistantship kwenye ofisi ya Rais wa zamani wa Marekani, Mzee Jimmy Carter, Carter Presidential Centre, kule Atlanta, Georgia. Kazi hiyo ilinipeleka hadi kufanya kazi Sierra Leone, ambako pia nilijifunza mengi. Pia Atlanta ndiko nilikofanikiwa kukutana na mke wangu mpendwa, Mona, ambaye mwakani itakuwa miaka kumi tangu tujuane, na ambaye, pamoja naye, tuna mtoto mmoja wa kike wa miaka mitatu na nusu.

Baada ya Carter Center, nikajiunga na George Mason University, iliyoko maeneo ya Fairax, Washington DC metro area, kusoma Masters kwenye fani ile ile ya diplomasia na usuluhishi wa migogoro. Nilikuwa a very active graduate student kwa maana ya kushiriki mijadala na professional and advocacy associations mbalimbali pale DC. I created a vast network of friendships in DC ambayo hadi leo nafaidika nayo. Nikiwa graduate school, nilipata fursa ya kufanya internship Wizara ya Mambo ya Nje.

Baada ya kumaliza graduate school nikaomba kazi Serikalini na kuajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje kama Afisa wa Mambo ya Nje Daraja la Pili (Foreign Service Officer II). Nikiwa Wizara ya Mambo ya Nje, nilipata fursa ya kufanya kazi kwa karibu na Waziri wetu wakati ule (Mhe. Kikwete), hasa kwenye harakati za kutafuta suluhu ya mambo ya Burundi na DRC. Kwahiyo, wakati alipoamua kugombea Urais, akaniomba nichukue likizo isiyo na malipo Serikalini nisaidie kuwa errand boy kwenye kampeni yake, ku-organise makaratasi na notes zake, na kuchangia hapa na pale kwenye tafakuri za kuendesha na ku-organise kampeni yake wakati ule. Tulifanikiwa kufanya mambo mengi mapya na ya kisasa kwenye kampeni ile (including TV campaign ads kwa mara ya kwanza). Nilishukuru sana kupata fursa ya kuzunguka Mikoa yote na Wilaya zote nchini, kwa kweli kila kona ya nchi, kwa njia ya barabara na kujua na kujuana na watu na kujua kwa kina changamoto na fursa za maendeleo katika maeneo yote. Mhe. Kikwete alipofanikiwa kuchaguliwa, akaniteua nije kumsaidia hapa Ikulu na hapa ndipo nilipo hadi leo.

Kazi hii ni ya heshima kubwa sana na ni muhimu kui-approach with humility. In fact, kuna nyakati natafakari sana kwamba, katika kufanya kazi hii, inawezekana nafaidika zaidi mimi katika kujifunza kuhusu nchi yetu, Serikali inayoendeshwa, maamuzi yanavyofanywa, sera zinavyotengenezwa, na siasa na uongozi wa nchi kwa ujumla unavyoendeshwa, kulivyo Rais anavyofaidika na usaidizi wangu.

Soma zaidi - From Mo's Blog: Exclusive Interview With January Makamba
 
Smafuru

Member
Jul 25, 2011
37
0
wakuu ningependa kufahamu maelezo (cv) ya mbunge januari makamba.
Kuanzia elimu yake, (na alama alizopata) na maisha yake kwa ujumla.
Na ni sifa gani ya pekee ambayo ilimfanya apate nafasi ya kuwa msaidizi wa j.k (2005 -2010)
inasemekana jamaa anaandaliwa kuja kuwa president wa tanzania. Hmmm...! Urais at that age ?
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,759
2,000
ingia kwenye tovuti ya bunge..wait a minute..kakutuma uje kumpigia kampeni,..apate airtime a.k.a comments za wanajf..tuko bize na shimbo
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,604
2,000
wakuu ningependa kufahamu maelezo (cv) ya mbunge januari makamba.

Kuanzia elimu yake, (na alama alizopata) na maisha yake kwa ujumla.

Na ni sifa gani ya pekee ambayo ilimfanya apate nafasi ya kuwa msaidizi wa j.k (2005 -2010)

inasemekana jamaa
anaandaliwa kuja kuwa president wa tanzania.

Hivi ma president wa Tanzania huwa wanaandaliwa na binaadam? mie nilifikiri huwa ni "chaguo la mungu"!
 
First Born

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
5,328
2,000
Unataka kumzuia?
Watanzania wengine bwana. We alama na performance ya mtu inakuhusu nini, we angalia anaperform vp shughuli za maendeleo ya Taifa.
 
Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
24,207
2,000
Hv huyu faizafoxy anaga shughuli nyngne kwnye kila thread lazma ukute comments zake za utata.
 
jonasadam

Member
Aug 3, 2011
31
0
kwa cv yake fupi january ni mwanadiplomasia kitaaluma. alichukua mikoba ya jairo kama msaidizi wa jk baada ya jk kupata uraisi 2005 akaonelea asindelee na jairo aliekuwa msaidizi wake kwa miaka mingi. aliamua kumpa ukatibu mkuu kama asante ya kumsaidia kwa miakamingi. fununu ni kwamba january ambae amechaguliwa hivi karibuni kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje wa ccm anateuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje kuchukuwa nafasi ya membe ambae inasemekana na ni mmoja wa watu watatu ambao wanaweza kumrithi ngeleja. wengine ni magufuli na sitta. kwa taarifa tu ni hayo.
 
gwaigwa

Member
Mar 16, 2012
29
0
jameni hebu nisaidieni kuna uhusiano wowote kati ya uwezo wa mtu darasani na uwezo na umakini wake kwenye uongozi?

mana kumekuwa na watu wengi wengi ambao wamekuwa wakifanya harakati za chini chini za kuutaka Urais wa nchi yetu. wengine tunawafahamu namna ambavyo hawako makini toka utotoni mwao, hivi ikitokea kweli wakawa tutakuwa tunalipeleka wapi taifa letu? mfano ni hizi harakati za chini chini zinazofanywa na mbunge wa bumbuli, mh januari makamba ambaye anajipanga kugombea kwa kufanya mikutano ya hapa na pale na pia kujinadi ili kujitia umaarufu kwa wananchi na haswa kupitia ujana wake na kiu ya mabadiliko iliyopo nchini. hapa ofisini kwetu kuna mtu alisoma na huyu mheshimiwa. baada ya mimi kusoma post ya hawa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa JF niliwashirikisha wenzangu nikiwaambia kuwa katika wabunge vijana huwa namfagilia sana Januari kwa namna anavyoonesha weledi kwenye kazi zake. ndipo jamaa akasema kuwa huyo hana kitu sababu alifeli kidato cha nne na cha sita na kutumia hela za usalama wa taifa kwenda kusoma nje kwa ushawishi wa baba yake mzee makamba. jamaa akathibitisha kuwa alisoma naye form six pale forest hill na kwamba januari makamba alipata division zero. kauli hii ilinishtua sana na kuniakatisha tamaa kabisa ndipo nikaamua kuwauliza hapa hivi akifanikiwa kuingia ikulu huyu itakuwaje?
 
Mzee wa ngano

Senior Member
May 3, 2012
184
195
Hebu tuambie alimaliza mwaka gani na alitumia jina gani ili twende tukafukunyue Baraza tukishathibitisha tutachangia. kale kaugonjwa ka kutoa habari zisizothibitishwa katika jamvi wengi mnako na sijui lini katakoma. Kuambiwa tu na mtu kuwa kasoma nae sio uthibitisho, mbona hata mimi naweza kusema nimesoma na wewe tukamaliza wote six na ukapata div. one wakati labda uhalisia ulimaliza 7 tena kwa shida na kwamba faida pekee uliyoipata ni kupiga picha na mwl. Mkuu.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,728
2,000
jameni hebu nisaidieni kuna uhusiano wowote kati ya uwezo wa mtu darasani na uwezo na umakini wake kwenye uongozi?

mana kumekuwa na watu wengi wengi ambao wamekuwa wakifanya harakati za chini chini za kuutaka Urais wa nchi yetu. wengine tunawafahamu namna ambavyo hawako makini toka utotoni mwao, hivi ikitokea kweli wakawa tutakuwa tunalipeleka wapi taifa letu? mfano ni hizi harakati za chini chini zinazofanywa na mbunge wa bumbuli, mh januari makamba ambaye anajipanga kugombea kwa kufanya mikutano ya hapa na pale na pia kujinadi ili kujitia umaarufu kwa wananchi na haswa kupitia ujana wake na kiu ya mabadiliko iliyopo nchini. hapa ofisini kwetu kuna mtu alisoma na huyu mheshimiwa. baada ya mimi kusoma post ya hawa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa JF niliwashirikisha wenzangu nikiwaambia kuwa katika wabunge vijana huwa namfagilia sana Januari kwa namna anavyoonesha weledi kwenye kazi zake. ndipo jamaa akasema kuwa huyo hana kitu sababu alifeli kidato cha nne na cha sita na kutumia hela za usalama wa taifa kwenda kusoma nje kwa ushawishi wa baba yake mzee makamba. jamaa akathibitisha kuwa alisoma naye form six pale forest hill na kwamba januari makamba alipata division zero. kauli hii ilinishtua sana na kuniakatisha tamaa kabisa ndipo nikaamua kuwauliza hapa hivi akifanikiwa kuingia ikulu huyu itakuwaje?

Mkuu wewe mwenyewe umekiri kuwa unamfagilia lakini kusikia ati kapata division zero unaonekana kuhoji tena uwezo wake! Usingepata hiyo habari basi ungeendelea kumkubali? Kama ni ufaulu wa darasani basi nchi zingekuwa zinaongozwa na maprofessor.
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,208
2,000
Kwa sasa ninaona uwezo wa makamba kama wa zitto. Haimaanishi kuwa naungana na hao uvccm bali yawezekana kweli alifeli lakini dakika za mwisho alijitambua
 
tofali

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
4,011
2,000
Hivi unaanzaje kumfagilia mtu ambaye ktk uongozi ht miaka 5 hajafika..kwa kifupi na muona wakawaida..sijui ni lipi kafanya la ajabu mpk ashawishi hao vijana hivyo..yale yale kumfagilia kikwete enzi hizo kumbe kazi hawezi
 
Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,588
2,000
jameni hebu nisaidieni kuna uhusiano wowote kati ya uwezo wa mtu darasani na uwezo na umakini wake kwenye uongozi?

mana kumekuwa na watu wengi wengi ambao wamekuwa wakifanya harakati za chini chini za kuutaka Urais wa nchi yetu. wengine tunawafahamu namna ambavyo hawako makini toka utotoni mwao, hivi ikitokea kweli wakawa tutakuwa tunalipeleka wapi taifa letu? mfano ni hizi harakati za chini chini zinazofanywa na mbunge wa bumbuli, mh januari makamba ambaye anajipanga kugombea kwa kufanya mikutano ya hapa na pale na pia kujinadi ili kujitia umaarufu kwa wananchi na haswa kupitia ujana wake na kiu ya mabadiliko iliyopo nchini. hapa ofisini kwetu kuna mtu alisoma na huyu mheshimiwa. baada ya mimi kusoma post ya hawa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa JF niliwashirikisha wenzangu nikiwaambia kuwa katika wabunge vijana huwa namfagilia sana Januari kwa namna anavyoonesha weledi kwenye kazi zake. ndipo jamaa akasema kuwa huyo hana kitu sababu alifeli kidato cha nne na cha sita na kutumia hela za usalama wa taifa kwenda kusoma nje kwa ushawishi wa baba yake mzee makamba. jamaa akathibitisha kuwa alisoma naye form six pale forest hill na kwamba januari makamba alipata division zero. kauli hii ilinishtua sana na kuniakatisha tamaa kabisa ndipo nikaamua kuwauliza hapa hivi akifanikiwa kuingia ikulu huyu itakuwaje?

Siogopi Chochote!

January Makamba ajitokeze sasa kujibu tuhuma za kuiba mitihani Galanos Sekondari kidato cha nne.

Hatuwezi kuwa na naibu waziri wa sayansi na teknolojia mwenye tuhuma za wizi wa mitihani karne hii inayohitaji weledi bila kupata ufafanuzi wa kina.

Kuna wimbi la wanafunzi kukimbia masomo ya sayansi na wengine kutafuta mbinu za wizi.Tunazipinga ila katika kukabiliana nazo tunampa uwaziri mwenye tuhuma hizo.

Nahisi Mfalme Juha atakua kwenye kiti cha enzi!
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Mkuu wewe mwenyewe umekiri kuwa unamfagilia lakini kusikia ati kapata division zero unaonekana kuhoji tena uwezo wake! Usingepata hiyo habari basi ungeendelea kumkubali? Kama ni ufaulu wa darasani basi nchi zingekuwa zinaongozwa na maprofessor.

Mkuu Kimbunga sabah kheri!
Ukipata muda tembelea blogu ya January alivyojikanyaga kanyaga kuhusu kufutiwa matokeo ya kidato cha nne baada ya kuthibitika kuiba (kufanya udanganyifu) mitihani ya kidato cha nne Galanos Secondary School.
Pengine kama si kuwa mtoto wa Yusuph Makamba sashivi January angekuwa anachoma mahindi bumbuli pale Soni sokoni au kijijini kwekitui!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom