Wasichana /Wanawake wenzangu

hahaahahahaha

mm mwenyewe natafuta mwenye tabia hzo tuyajenge lakin wap mpaka nasemaga i will marry when I want because beautiful once is not yet born
Kuoa skuizi imekuwa ni bahati nasibu, ukibugi umeumia, yani ni tofauti na zamani
 
Mbona ivo jamani.. Kuweni na imani nasisi basi hio dhana mlojijengea kichwani si nzuri kwa afya na ustawi wa mahusiano
Kwani uongo jamani? Kuwa tu mkweli usiidanganye nafsi yako. Kufuatia ongezeko la watu wasiojielewa basi probability ya kumpata mtu anayejielewa inapungua japo wapo.

Mfano wewe leo hii katika marafiki zako hao wa kike ulionao ungeambiwa uoneshe wanaofaa ili kaka yako aoe mmoja wao. Je ni wangapi ungewapendekeza ili kaka yako aishi naye kama mke ili afurahie maisha yake ya ndoa na nyie kama ndugu mfurahie jinsi kaka yenu anavyoishi na mke anayejielewa na mwenye upendo wa kweli?

Unaweza kumwona mtu anajielewa sana lakini ukimwambia samahani shida yangu natafuta rafiki wa kike/kiume anayejielewa kama wewe. Mtu huyo anaweza kukwambia subiri nifanye kwanza uchunguzi au akakwambia naweza kukuonesha halafu ukaja kunilaumu maana yake pamoja na kuwa yeye anajielewa lakini bado hata rafiki zake anaona bado hawajielewi kiasi cha kumwezesha yeye kutoa majibu ya moja kwa moja.

Ukitaka kuamini hili mtafute mtu mzima mwenye busara zake. Kaa naye mdadisi kuhusu maisha, mwombe akushauri namna maisha yanavyoendeshwa katika kipengele ambacho utaona kinafaa. Halafu mwisho mwambie yeye kama mzazi unajua amekua zamani na anazijua tabia za watu na pengine anaweza kumsoma mtu tabia zake na akaweza kuproject maisha yake atakavyokuja kuishi na familia yake na jamii nzima. Mwambie ninakakuomba unioneshe msichana au mvulana ambaye akiolewa/kuoa atakuwa ni mke/Mme mwenye kujua majukumu na wajibu wake kwa Mme/mke wake na familia kwa ujumla. Mzazi huyo atakwambia nipe mda niwachunguze kwanza maana yake hana jibu la moja kwa moja na pengine hata kama familia za rafiki zake kuna wavulana/wasichana wakubwa hatawataja hao moja kwa moja.

Kwa kifupi watu wasiojielewa wameongezeka sana kiasi cha kuwafanya watu wanaojielewa wapatikane kwa kupekua sana.

Kadiri unavyokuwa na sample nyingi na katika sample hizo kuna nzuri na mbovu na Kibaya zaidi sample mbovu zikawa nyingi kuzidi nzuri basi probability ya kupick sample nzuri hupungua.
 
Inawezekana umejificha kwenye story kumbe ww ni single mother's.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…