Wasichana /Wanawake wenzangu

NATAMANI MKE WANGU ASOME HII THREADY LAKINI KWAVILE AMEFUNGA MASIKIO NA KIBURI AKILINI MWAKE NAJUA KUNA SIKU ATANIKUMBUKA,NDOA NI LAANA NA NI BARAKA,KWA ANAYEVUNJA MAKSUDI HUAMBATANA NA LAANA
NAWASILISHA,,
Pole mkuu kwa huyo mwanamke wako aliyefunga masikio! Ndoa ndio chanzo cha Furaha na wakati huo huo kinaweza kuwa chanzo cha huzuni maishani!
 
Ungejua tuuu kuwa mwanamke huishi kulingana na matakwa ya mwanamke hata usingezungumza yote haya.


Mwanamke ni mama wa mtoto mkubwa wa kiume, ni jukumu lake kumchagulia malezi
"Mwanamke huishi kulingana na matakwa ya mwanamke" Nieleweshe hapa mkuu umeniacha njia panda.

Halafu pia mwanamke ndio anayemchagulia maisha huyo mtoto wake mkubwa wa kiume? Kivipi? Yaani Mme achaguliwe maisha na mke wake? Au sijaelewa vizuri labda. Napo naomba ufafanuzi kidogo pengine nami nijifunze.
 
"Mwanamke huishi kulingana na matakwa ya mwanamke" Nieleweshe hapa mkuu umeniacha njia panda.

Halafu pia mwanamke ndio anayemchagulia maisha huyo mtoto wake mkubwa wa kiume? Kivipi? Yaani Mme achaguliwe maisha na mke wake? Au sijaelewa vizuri labda. Napo naomba ufafanuzi kidogo pengine nami nijifunze.

Kwanza ni kile, nilikosea , ilipaswa iwe hivi,...
"""""' mwanaume huishi kulingana na matakwa ya mwanamke"""
Hii nadhani yenyewe utata wake umeisha.

Yaa wanaume tunachaguliwa namna ya kuishi na wanawake,
Mwanamke ndio hutoa malezi kwa mwanaume hasa katika kila nyanja.
Mathalani:-
Kuelewana/kutoelewana sana na majirani hutengenezwa na mwanamke, usafi au uchafu kwa ujumla hutegemea mwanamke, kipato kwa asilimia kubwa hutegemea mwanamke., nguvu na molari za kufanya kazi hutegemea mwanamke, furaha au huzuni nyumbani humtegemea sana mwanamke
N.k nyingi

Ukitaka mafanikio huwezi mkimbia mwanamke.
 
Kama yupo mwanamke mwenye vigezo hivyo hapo juu, Naomba ajitokeze tukamuweke Kwenye MAKUMBUSHO YA TAIFA kwasababu atakuwa ni hazina kubwa sana iliyobaki
Aisee wapo, mfano mzuri ni mke wangu. Hivyo vigezo vyote anavyo na sifa zingine nzuri ambazo hakutaja. Maisha swafi kabisa.
 
Wanawake wenzangu!
Natamani sana sote humu tuwe wake wema kwa wame zetu au mahusiano yetu kiujumla. Hivo naomba kushea kitu hapa. Hii nimeona mahali nikabarikiwa nayo kuleta kwenu wapendwa.

BUSARA KWA WANAWAKE.

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubutu wako.

2. Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.

3. Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.

4. Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio kuwa mtu wa kulipiza visasi.

5. Kuwa kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa mumeo. Hiyo ni busara.

6. Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongea na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha.

7. Kuwa na ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't help u!

8. Kuwa mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.

9. Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.

10. Hakuna kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.

11. Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.

12. Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki.

13. La mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakin yule mwenye maarifa na ufahamu yeya afaa kwa maisha yote!

Akhsanteni na weekend njema
Namba 13 hapa wengi wanafeli kwa kuongopewa na maumbo yao na hii ndio imepelekea kuvunja mahusiano na mwanamke nilie tokea kumpenda kwa dhati sana
 
Mh. Kama hayajakukuta bhasi
Mkuu inakuaje hiyo? Mapenzi anayostahili kupewe baba/mama ni tofauti na mapenzi ya watoto. Sio kweli kwamba watoto wanachukua mapenzi ya baba au mama, hii ni kisingizio tu. Huyo mtu akichunguzwa vizuri utagundua kuna mchepuko anampa mahaba.
 
Mbona masuala ya Mungu sijayaona hapo? Hilo ndilo la msingi zaidi, ukizingatia hilo kwa dhati mengine yanafuata tu.

Alafu ikumbukwe mke ni reflection ya mumewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom