Me sijui nimetokea familia gani teh. But kwa nilichokiobserve kidogo nikiwa college ni kwamba, wengi wa mabinti waliokuwa wanababaika na wanaume wenye uwezo mitaani ni mabinti waliotoka familia zenye uwezo Ila tu walikuwa na tatizo la kujikweza/kuendekeza dhiki, wanataka waishi maisha ya juu zaidi kuliko reality yao (kumaintain status). Stories za sijui kuna mtu anatoka na kigogo gani, nyingi ni za mabinti wanaojiweza kwao.
Kuna mabinti waliotoka familia zenye uwezo mdogo sana, hilo hilo boom walituma lisaidie nyumbani, hawaoni tabu kula wali maharage semister nzima, and there are times kuna mabinti walikuwa wanaomba kusaidia kufanya usafi cafeteria then wanapewa sahani ya wali (Mungu uwakumbuke watoto wako) na ratiba zao ni room, class, kanisani/msikitini then kulala, ndo wale most kina John kisomo. Wengi wao walikuwa watu wanaojali zaidi dignity zao.
Ingawa wapo wachache pia waliotokea familia dunia then wakajanjarukia vyuoni wee hatari, kama baby uliachwa village ndo sahau mazima, ukimfuata chuo utakanwa teh. But all in all, kuendekeza dhiki; kutoridhika na maisha haina tajiri wala maskini, ni mtu tu binafsi. Happy Easter to you all