Washauri wapya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Serikali ya Tanzania inadaiwa iko mbioni kuleta washauri wapya wa Ikulu na Wizara mbalimbali. Washauri hao toka nchi za Scandinavia wanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote ili kusaidia kutoa ushauri wa kuendesha Ikulu na Wizara mbalimbali.

Baadhi ya washauri hao wamewahi kufanya kazi na viongozi mbalimbali wa mataifa ya magharibi wakiwemo Mawaziri Wakuu, Marais na katika taasisi mbalimbali za Kimataifa.

"Unajua nchi yetu tumekuwa na matatizo katika uendeshaji wa mambo mbalimbali, na tumeona kuwa tusione haya kuomba ushauri wa kuendesha Ikulu" alisema mmoja wa watu ambao wanajua juu ya mpango huo.

"Huyu mjapani aliyekuja kutoa ushauri kwenye mambo ya viwanda ni mwanzo tu" alisema afisa huyo wa ngazi zajuu aliyekataa kutajwa jina lake kuwa si msemaji wa serikali.

Mtaalamu mwingine aliyeunga mkono mpango huo alisema kuwa "hatimaye serikali mefanya kile ambacho watanzania wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu; kutafuta ushauri kwa watu wasio na maslahi binafsi".

Mpango huo wa kuleta wataalamu wa kuendesha serikali toka nje endapo utafanikiwa inadaiwa utafuatwa na nchi nyingine mbalimbali za kiafrika zenye migogoro ya ndani. Baadhi ya nchi zinazofuatilia mpango huo wa Tanzania ambao umebatizwa jina la "Rent a Leader-Lend a Hand Project 2008" unaungwa mkono na Watanzania wengi hasa baada ya viongozi wengi wa kizalendo kuonekana kuwa ni wabangaizaji ambao miaka zaidi ya 45 baada ya uhuru hawajajua jinsi ya kuongoza nchi.

Semina ya kwanza itakayoendeshwa na wataalamu hao ili kuweza kujua kiini cha tatizo la uongozi nchini, inatarajiwa kufanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, Mkoani Arusha mapema mwezi wa nne.

Habari hizi hata hivyo hazijathibitishwa na kiongozi yeyote wa serikali kwani hadi tunakwenda mitamboni hakuna hata mmoja aliyeweza kupatikana kwa sababu sikumtafuta.
 
Hahahaha utafikiria jamaa walisoma nilichoandika kwenye ile thread ya Mjapana kuwa ipo siku tutakodisha hata raisi ili aje atuongozee nchi yetu. Its funny.
 
That is right.

Kwa nchi inayoendeshwa na watu walioshindwa siku nyingi zilizo pita ni kweli lazima washauri watoke nje kuja kuwaambia namna ya kuendesha Ikulu na namna ya kujizuia kujaa tamaa ya kupokea Rushwa.

Ieleweke kwamba ni kikundi cha watu wachache na chama chao cha SISIEMU ndiyo walio shindwa. Kama nchi, kama watanzania hatujashindwa bado, tuna uwezo na tuna hamu ya kuiongoza na kuendeleza nchi yetu.

Pendekezo langu;

Serikali ya SISIEMU Watoe Zabuni ya vyama mbalimbali duniani kuja kuunda serikali na kuiongoza Tanzania kwa mkataba wa kipindi cha miaka kumi kumi,kuwe na kipengele kwamba kitakacho patikana katika kodi na rushwa SISIEMU wapate 3% ya Net Value.
 
Yule mshauri maarufu kutoka Japan aliyejulikana kwa jina la DR Kobayashi aliyeletwa na BWK kwa jina kubwa la " MINI TIGER PLAN ya 2020" kaishia wapi? Mipango yake imewekwa kapuni?
 
Jamani hawa washauri mbona wapo tu siku zote na hakuna mabadiliko wanayoleta? Ukiitisha wajipange mstari kutoka dar watafika chalinze. Kwani wazungu mnaowaona humu nchini hamjua wengi wamekuja kwa gera hiyo. Baadhi yao baada ya mikataba yao kwisha huishia kukaa nchini na kuendeleza ufisadi kwani wanakuwa wamejiweka karibu na wanasiasa.

Tatizo siyo washauri ila tatizo liko kwa washauriwa. Maana kama ni ushauri tu hata hapa JF kuna ushauri kibao tu.

Ninacho kiona mimi kuhusiana na swala la washauri ni mpango wa nchi wahisani kujirudishia fedha. Karibu kila mradi unao fadhiliwa na nchi wafadhili unakuja na washauri wake (advisors) ambao hulipwa pesa nyingi. Pamoja na kutoa ushauri lakini pia wana kazi ya siri ambayo ni kulinda maslahi ya nchi zao katika sector husika.

Unaweza kukuta japani wana mpango wa kuja kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini. Hivyo ili kupata detailed data za mambo yalivyo na kujiweka karibu na wanasiasa wanamtuma spy wao kwa kofia ya ushauri. Baada ya kupata kile alichokuja kutafuta anaishia zake, mnabaki vile vile.

Ukifanya kazi na hawa watu utagundua agenda zao za siri. Baadhi ya washauri wanaokuja ukiangalia uwezo wao unaweza hata ukashangaa imekuwaje huyu kaletwa huku? Ni namna tu yakuchukua pesa zao na kufanikisha malengo yao.

Nimekuwa nikifanya kazi na watu wa namna hiyo (advisors) kwa miaka kadhaa sasa. Baadhi wana mchango mzuri ingawa mara nyingi haufanyiwi kazi na baadhi ni mafisadi wa kutupwa. Tender zote kubwa za miradi huakikisha zinaenda kwenye kampuni zao.
Wengi wao wanakuwa na malengo maalum ya kutafuta nyeti kuhusu nchi hii.
 
Ufisadi na manufaa binafsi vinachukua sura mpya jamani
Kwa sababu huu si udhalilishwaji kabisa wa wasomi wetu, Kuna maprofesa wangapi, Madokta wangapi, professional kibao Tanzania, Lakini eti tunatafuta wataalamu kutoka nje!!!!
Loooo, kazi kweli kweli ndugu zangu, siamini kabisa labda kuna mkono wa mtu, ina maana Kikwete awakubali wataalamu wa Kitengo cha Uchumi pale UDSM jamani

Tutaleta mpaka washauri wa Usalama wa Taifa a.k.a Usalama wa Mafisadi

Nakubaliana na wewe. Nini maana ya nchi kuwa na wasomi wake? Nini maana ya nchi hii kuwa na vyuo vikuu? Nini maana ya kuwa na shule za aina zote ndani ya nchi hii? Sawa,tuna wasomi tena wenye PhD na ni maprofesa katika chama tawala,wanafanya nini? Maslahi binafsi na ufisadi,ndiyo jibu la haraka. Ina maana wasomi wote wa uchumi wameshindwa kutusaidia tukaweza kufika? Sawa siasa na shule wakati mwingine vinaendana na wakati mwingine havifanani,ndiyo maana mawazo ya wasomi hayana nafasi katika jamii za wanasiasa,hasa siasa za bongo. Kwa hili naanza kukubaliana taratibu na Prof. Watson kuhusu walakini wa akili za watu weusi,mawazo yake yana ukweli fulani japo tulimshambulia. Tunayoyaoona ndiyo yale aliyosema Prof.Watson. Hii ni aibu,serikali ya CCM mnatuhaibisha
 
Hawa wataalamu wa WOrld Bank na mashirika mbuzi yote si ndo walitushauri kuhusu madini kuwa tusiweke mashariti yoyote ili kuvutia wezi akina BARICK na wengine?

Shida moja ya hawa wataalam nchi kama Tanzania hatuna ubavu wa kukataa wataalam uchwara yaani tunaletewa tu. Je CV zao nami atazihakiki kwanza kabla ya kufanya huoushauri. Kwa wale ambao wamefanya na hao wanaoitwa advisors toka nje ya nchi kwenye miradi mbali mbali wanachofanya ni kujifunza kwanza sababu mazingira ya Tz hawayajui au hawawezi kudeliver. Wengi wanakuwa ni report compiller badala ya kuwa report analyser.

Lakini nafikiri Rais wetu anapenda sana wataalam kutoka nje kwani nakumbuka wakati akiwa kwenye ziara nchi za scandinavia aliomba kupewa msaada wa wataalam hasa wa kusimamia mikataba. Ila kwa mtu ambaye anajua mazingira ya Tz, wanasiasa wana nguvu kuzidi wataalam so na mambo ya kitaalam yanafanyika kisiasa ili wanasiasa wafurahi. BADO TUNA KAZI KUBWA MBELENI HADI PALE MINDSET ZA WANASIASA ZITAKAPOBADILIKA.
 
Ufisadi na manufaa binafsi vinachukua sura mpya jamani
Kwa sababu huu si udhalilishwaji kabisa wa wasomi wetu, Kuna maprofesa wangapi, Madokta wangapi, professional kibao Tanzania, Lakini eti tunatafuta wataalamu kutoka nje!!!!
Loooo, kazi kweli kweli ndugu zangu, siamini kabisa labda kuna mkono wa mtu, ina maana Kikwete awakubali wataalamu wa Kitengo cha Uchumi pale UDSM jamani

Tutaleta mpaka washauri wa Usalama wa Taifa a.k.a Usalama wa Mafisadi

BabaH,
Wazungu ndugu yangu, viongozi wetu wakishauriwa na Mtanzania hawaamini. Mtegemea cha nduguye ...., kweli wazungu wanaabudiwa tanzania....
 
Paul Kagame amemwomba Tony Bleya awe mshauri wake wa uchumi na mahusiano ya kimataifa, Tony ameshakubari ombi hilo kasema wala hatahitaji malipo kutoka serikali ya Rwanda kwani anayopesa yakumtosha, Tony amesema anatamani Rwanda ipige hatua kiuchumi kama uk.

Naungana na Madilu, sie tunahitaji kubinafsisha serikali tulete management mpya, Chama tawala kipewe 3% royalty fee.
 
Ni wapi tunaweza kupata washauri wa kizungu ambao wana rekodi nzuri na watatusaidia kuendesha vitu kama Benki Kuu n.k.. sitaona ubaya hata tukiomba washauri wa Usalama wa Taifa...
 
Heko JK, naona sasa umeamua kufanya kweli, nchi nyingi duniani huwa na washauri katika nyanda zote za uongozi hata Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa Museveni wa uchumi na kuwa na washauri ni jambo jema kabisa. Na linafaa liungwe mkono kwani haliharibu linatengeneza.

Mkuu nyerere alikuwa na personal assistant wake mama wa kizungu na kabla ya hapo alikuwa na mshauri mmerakani, ni vipi utautumia ushauri ndio inavyo matter lakini si kuwa na ushauri kuna ubaya.
 
Tatizo sio ushauri tatizo ni ufisadi na wizi. Hao jamaa watakachokuja kushauri ni kuwa viongozi waache wizi na ufisadi, na wakisema hivyo watapewa siku moja kufungasha na kuondoka na mchezo ule utaendelea palepale. Ni vizuri tuki-import mawaziri, makatibu na wakurugenzi, maana huko ndio kumeonekana kuwa na mafisadi, na ni huko ambako kuna loop holes za ufisadi.
Na kama lengo ni kuleta efficiency, kama hao jama wanaweza kukubali hata kututafutia rais itakuwa bomba tu, bora atuletea maisha raha na mazuri.
Kwa ufupi ni wazo la kujinga kuleta mtu ambaye hajyui utamaduni wako wala situation yako kuja kukushauri!
 
Sioni ubaya wowote,ila mimi naona tungewaajiri kabisa na tuwalipe watuendeshee TRA na mipango ya uchumi na maendeleo,maana tulionao ndio wame srew up big time
 
I know this is outrageous and controversial lakini nigependa kuona huu utaratibu ukitumika hata kwenye nafasi ya uraisi kwa sasa.
 
Tatizo sio ushauri tatizo ni ufisadi na wizi. Hao jamaa watakachokuja kushauri ni kuwa viongozi waache wizi na ufisadi, na wakisema hivyo watapewa siku moja kufungasha na kuondoka na mchezo ule utaendelea palepale. Ni vizuri tuki-import mawaziri, makatibu na wakurugenzi, maana huko ndio kumeonekana kuwa na mafisadi, na ni huko ambako kuna loop holes za ufisadi.
Na kama lengo ni kuleta efficiency, kama hao jama wanaweza kukubali hata kututafutia rais itakuwa bomba tu, bora atuletea maisha raha na mazuri.
Kwa ufupi ni wazo la kujinga kuleta mtu ambaye hajyui utamaduni wako wala situation yako kuja kukushauri!

Hao wakija watapigwa zengwe hadi ushangae, maana watakuwa wanaziba mianya ya ulaji ... yaliyotokea kwa Mkurugenzi Muhimbili umeyasahau? Ebu nisikilizie kinachoendelea huko sasa hivi ... ni kula kwa kwenda mbele bila hata aibu na sasa wanaanza kutupiana mpira wao wenyewe. Hii nchi nilishawahi kusema kwamba kama ingekuwa ni computer, basi inatakiwa ifanyiwe namna.
 
Heko JK, naona sasa umeamua kufanya kweli, nchi nyingi duniani huwa na washauri katika nyanda zote za uongozi hata Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa Museveni wa uchumi na kuwa na washauri ni jambo jema kabisa. Na linafaa liungwe mkono kwani haliharibu linatengeneza.

Mkuu nyerere alikuwa na personal assistant wake mama wa kizungu na kabla ya hapo alikuwa na mshauri mmerakani, ni vipi utautumia ushauri ndio inavyo matter lakini si kuwa na ushauri kuna ubaya.

Unakumbuka wakoloni walipokuja Afrika kutawala walisema kuwa wanakuja kuendeleza Afrika maana bara hilo liko nyuma.

Huu ni mwanzo tu wa Kikwete na serikali yake kuwarudisha wakoloni ili kutawala tena maana waafrika tumeshindwa kujitawala wenyewe (kumbuka argument ya Ian Smith wa Rhodesia). Haya ya Nyerere kuwa na mshauri wa kizungu mbona ni historia, au unataka vile turudi kuwa na madakitari chini ya kumi tu wazawa kama vile tulivyokuwa baada ya uhuru? Ni lini huu utegemezi utakoma?
 
Back
Top Bottom