wew sijui ni dini Gani ila biblia imeandika.....
Yesu alisema ukimwangalia mwanamke kwa kumtammani, umeshazini naye moyoni
Tuwe wakweli ndg yangu, tuuweke kando unafiki. Tunahubiri na kuvilaani vitu tunavyovipenda na kuvihusudu sisi wenyewe.
Maandiko yanasema kama ulivyoandika. Lkn maandiko ya dini ni mafumbo yanayohitaji tafsiri. Si kila andiko limenyooka kama hadithi za alfulelaulela.
Labda nikuulize, Nabii Mussa katika muktadha wa kuwakomboa wana wa Israel kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi Kaanani, ambayo kwa jiografia ya sasahivi ni Israel na maeneo ya Palestina.
Inaelezwa kuwa safari yao baada ya kuvuka bahari ya shamu, iliwachukua muaka40 kuifikia hiyo nchi ya ahadi ambapo hata Mussa mwenyewe hakujaliwa kufika!
Safari inayoongelewa pale ni kama kutoka Ubungo hadi Chalinze ama Mlandizi.
Je kwa hali ya kawaida hapo unaweza kutembea hata wiki1?
Yote yaliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu ni mafumbo yanayohitaji tafsiri.
Kutamani siyo kuzini. Kutamani kumeumbwa ili kutufanya binadamu tuingiliane, kuzaana, kuongezeka na kuijaza dunia ya Mungu kwa mapenzi yake.
Sitakubaliana na wewe kusema kutamani ni dhambi, bali kuzini ndiyo dhambi.
Hivi wachumba zetu kabla ya kuanza mchakato wa ndoa na hata kabla ya kumsemesha, hatua ya kwanza huwa ni kumtamani na mengineyo kufuata.
Kutamani na kupenda ni vitendo ndugu, ndiyo maisha tunayoishi, hayakwepeki.