Wasanii hunufaikaje (hupataje hela) kupitia youtube?

Wasanii hunufaikaje (hupataje hela) kupitia youtube?

yello masai

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
3,917
Reaction score
4,170
Wakuu naomba mnisaidie kujibu swali hili ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa kipindi kirefu sana.
Nimekuwa nikiona wasanii wakishindana kuongeza idadi ya viewers wa video zao youtube, nikawa najiuliza huwa wananufaika vipi wakiongeza viewers.

Leo kidogo swali langu likapata jibu baada ya kumsikia Luge muda huu akitoa kauli hii kwenye XXL " BASATA huwa wanadhani wakimfungia msanii wanamkomoa kumbe wanamuongezea nafasi ya kupata hela zaidi kupitia youtube kwa sababu hiyo nyimbo iliyofungiwa itatazamwa zaidi kule kuliko kuangalia bure kwenye TV stations, na kuna wasanii wengine wanaomba wafungiwe".

Kutokana na kauli hii nimepata jibu kuwa wasanii huwa wanapata hela kupitia youtube wakiweka nyimbo zao. Je wanapataje hizo pesa? Wanalipwa kwa njia gani?

Na je, nikiweka video yoyote youtube watu wakaangalia nitapata hela??
Anayejua anisaidie.
 
Back
Top Bottom