Wasakwa kwa kumvisha mbwa fulana ya Kikwete

Safi saaaaana Ruvuma. Kama wanawapenda wawape sare za shule za watoto wenu na sio kuwalazimisha kuvaa tshet zao. Keep it up, hata kgoma walifanya passive resistance enzi za ukoloni kama ninyi mnavyowatenda sasa hawa mafisadi.
 
Jamani tuache utani huyu mbwa kapendeza sssssaaaaaaannnnnaaaaaaa, au mnasemaje wadau? tufanye mpango hata kitimoto nao tuwavishe
 
Kuvishwa mbwa mbona kuna hadhi! Mimi ningeitumia kuchambia ****** huko, kama wengine wanavyotumia kudekia maliwatoni.
 
Kwani mbwa kuvaa flana ya ccm ni kuiunga mkono au kuipinga? Na kosa ni nini hasa, flana au flana ya ccm
Mi sijaelewa
 
mimi sioni tatizo...kwani ni sheria gani inasema watu wasiwavalishe wanyama nguo?...tena kapendeza sana...
 
Ni vema watanzania wote nchi nzima wangefanya hivyo wakati huu wa lala salama. Popote pale mbwa walipo wakamatwe na wavishwe Tisheti za CCM kama ishara ya wazi ya kukataa Rushwa!
 
Mimi nitawavalisha hao mbwa t-shirt,khanga kofia nikimalizia na diaper p&*@....ze.....!! Kuvalisha mbwa t-shirt ajabu yake nini?? Message sent CCM TUMEWACHOKA MBAYA KABISA HAMUELEWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII?????????????
 




Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linawatafuta watu wawili akiwemo mwanafunzi wa darasa la sita wakazi wa kijiji cha Lilondo wilayani Songea kwa tuhuma za kumvalisha mbwa fulana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye picha ya mgombea urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 24, mwaka huu saa 9:00 alasiri eneo la Lilondo wilayani Songea.
Kamanda Kamuhanda aliwataja watuhumiwa hao wanatafutwa na polisi kuwa ni Ephraem Mahuwi anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 27, na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Lilondo (jina limehifadhiwa).
Alifafanua kuwa muda mfupi kabla ya tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lilondo, walimwagiwa sare za CCM zikiwemo fulana, kofia, khanga na skafu wakati msafara mkubwa wa magari yaliyokuwa yakimsindikiza mke wa mgombea urais kupitia CCM, Mama Salma Kikwete, ukipita kutokea Ruvuma kwenda mkoani Iringa.
Kamanda Kamuhanda aliongeza kuwa baada ya msafara huo kupita, mtuhumiwa Mahuwi na mwanafunzi huyo, walichukua moja ya fulana za CCM walizogawiwa ikiwa na picha ya mgombea urais kupitia chama hicho na kumvalisha mbwa.
Alisema baada ya kumvalisha mbwa huyo, watuhumiwa hao walimuacha aendelee kurandaranda sehemu mbalimbali za kijijini humo.
Kamanda Kamuhanda alisema wafuasi wa CCM walimuona mbwa huyo aliyevalishwa sare za chama chao na kuanza kumkimbiza kwa takriban saa moja na kufanikiwa kumkamata.
Alisema wafuasi hao wa CCM walibaini kuwa mbwa huyo ni mali ya Mahuwi na kwamba baada ya kusikia mbwa wake amekamatwa, yeye na mwanafunzi huyo, walikimbia na kwenda kusikojulikana.
Hata hivyo, Kamanda Kamuhanda alisema polisi wanafanya kila liwezekano kuhakikisha kwamba watuhumiwa hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili

Hadi wanafunzi wa darasa la sita wamemchukia Jk. Maana hawa wanafunzi hawana chama. Haya mambo hayo!!!!!!!!!
 
Ama kweli CCM imekwisha. Huko Ruvuna inasemekana baadala ta wananchi kuvaa tisheti za Kikwete wameanza kuvisha mbwa. Ni vema kama watanzania wangesaka mbwa mitaani na kuwavisha tisheti hizo kama ishara ta wazi ta kukataa rushwa!
 
Iv uzuri wa Kikwte ndio kosa la kuwatafuta hao vijana au? Iv nyie Polisi mna matatizo gani, badala ya kufikiria kulinda uhuru wa raia mnakua wa kwanza kuupindisha! na mi ningekua na mbwa ningeitafuta iyo sare na ningemvisha, tena na kofia kabisa!!!
 
Kwani shida iko wapi kumvika mbwa gauni au nguo ya aina yoyote? Check hizi picha za mbwa na tishet ya Obama. Kama obama anvaliwa na mbwa who is Kikwete?

Wewe Opinionated nadhani hauko sawa sawa. Kwani Obama wana uhusiano gani na Kikwete hata ukasema hivyo? Obama ni Mungu wako? Na mila na silka zao ziko sawa na za kwetu?

Hebu jadili mantiki ya hili jambo na sio kusema kama Obama anafanya hivi basi ndiyo dunia nzima waendelee kufanya hivyo.
 
Hadi wanafunzi wa darasa la sita wamemchukia Jk. Maana hawa wanafunzi hawana chama. Haya mambo hayo!!!!!!!!!
Today this afternoon I were taking my son of 6yrs from school. I met one of my friend and he stopped me. I thought he has a something special! Without saying anything he threw a CCM cap to my car. Usishangae mtoto alimuuliza this for what? Akamwambia for your dad to put on. Boy alimwambia MY DAD DONT PUT ON SUCH COLOUR and he hand it over to him. Baadaye dogo akaniuliza kwani wewe ni ccm baba? Nikamwambia hapana, akasema afadhali maana lichama lenyewe la mafisadi kama nini. Nikamuuliza mafisadi ni nini? Akasema ni WEZI. A boy of 6 yeras! Anawajua ccm na rangi zao na ufisadi wao! SHAME YOU CCM!
 
.......Nilivyosoma hii habari nimecheka sana,its so damn funny!!! Sasa CCM wamechukia nini na wakati mbwa anashabikia naye uchaguzi kwa kuvaa t-shirt.
 
Polisi huko Songea wanamtafuta mtoto wa darasa la Sita kwa kumvisha mbwa tisheti ya CCM. Hata watoto wamechoshwa na CCM. Huyo mtoto asisumbuliwe. Ameonyesha uzalendo wake. Watanzania wote waige mfano. Popote pale mbwa walipo wakamatwe, wapewe zawadi za CCM dakika hizi za lala salama.
 
Fulana ya kikwete kivipi? wao wamegawa t-shirt bila kujali nani anawaunga mkono ,na hio t shirt sio ya kikwete ni ya huyo aliyopewa na ni chaguo lake kuifanya anavyotaka.Na chaguo lao ni kumvalisha mbwa sasa kuna kosa gani hapo? inamaana ccm miaka yote mpaka leo bado hawajakomaa kisiasa au ndio "Big baby" wa siasa?
 
.......Nilivyosoma hii habari nimecheka sana,its so damn funny!!! Sasa CCM wamechukia nini na wakati mbwa anashabikia naye uchaguzi kwa kuvaa t-shirt.

Unajua ccm wanamambo ya kitoto sana manake huu sio u-dictator sasa ni utoto mtupu.
 
Mimi nataka wamkamate huyo mtoto wa darasa la sita tuone watamshitaki kwa kosa gani. Haki watoto wataandamana nchi nzima. Hivi Rizwan akimtukana Jakaya atamshitaki?
 
Back
Top Bottom