Wasakwa kwa kumvisha mbwa fulana ya Kikwete

mojoki

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
1,314
290
Mtuhumiwa mahui na kijana mmoja wa Darasa la sita (Mwanza)wanatuhumiwa kwa kumvisha Mbwa Sare ya Chama,Ambapo baada ya wafuasi wa CCM kumuona Mbwa huyo walimkimbiza kwa takribani Lisaa limoja na kufanikiwa kumkamata kisha kumvua sare hizo...ME SIONI TATIZO KUMVISHA MBWA NGUO ZA BINADAMU
 
Nguo za bure, hivi wao walifikiri kila mwananchi anazihitaji!!! Watu wanataka maendeleo siyo T-shirt moja ila baada ya miak mitano.
 
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linawatafuta watu wawili akiwemo mwanafunzi wa darasa la sita wakazi wa kijiji cha Lilondo wilayani Songea kwa tuhuma za kumvalisha mbwa fulana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye picha ya mgombea urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 24, mwaka huu saa 9:00 alasiri eneo la Lilondo wilayani Songea.

Kamanda Kamuhanda aliwataja watuhumiwa hao wanatafutwa na polisi kuwa ni Ephraem Mahuwi anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 27, na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Lilondo (jina limehifadhiwa).

Alifafanua kuwa muda mfupi kabla ya tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lilondo, walimwagiwa sare za CCM zikiwemo fulana, kofia, khanga na skafu wakati msafara mkubwa wa magari yaliyokuwa yakimsindikiza mke wa mgombea urais kupitia CCM, Mama Salma Kikwete, ukipita kutokea Ruvuma kwenda mkoani Iringa.

Kamanda Kamuhanda aliongeza kuwa baada ya msafara huo kupita, mtuhumiwa Mahuwi na mwanafunzi huyo, walichukua moja ya fulana za CCM walizogawiwa ikiwa na picha ya mgombea urais kupitia chama hicho na kumvalisha mbwa.

Alisema baada ya kumvalisha mbwa huyo, watuhumiwa hao walimuacha aendelee kurandaranda sehemu mbalimbali za kijijini humo.

Kamanda Kamuhanda alisema wafuasi wa CCM walimuona mbwa huyo aliyevalishwa sare za chama chao na kuanza kumkimbiza kwa takriban saa moja na kufanikiwa kumkamata.

Alisema wafuasi hao wa CCM walibaini kuwa mbwa huyo ni mali ya Mahuwi na kwamba baada ya kusikia mbwa wake amekamatwa, yeye na mwanafunzi huyo, walikimbia na kwenda kusikojulikana
.

Hata hivyo, Kamanda Kamuhanda alisema polisi wanafanya kila liwezekano kuhakikisha kwamba watuhumiwa hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

CHANZO: NIPASHE
 
Hivi sisiemu hawajifunzi tu? Mwaka jana kule Tarime, vijana walimvika mbwa jezi hizo hizo za sisiemu ambazo wao wanagawa bure. Watu wanataka maendeleo ya kweli (mbolea za ruzuku, maji safi, zahanati zenye dawa na madaktari n.k.) sio nguo na pombe.
 
safi sana, watu siku hizi hawadanganyiki kwa rushwa ya vijitisheti!
 
Ya Tarime yanajirudia safari hii Ruvuma, acha mbwa nao wavae nani atavaa matambala hayo, tshet zenyewe hazina thamani zimezagaa kila sehemu kwangu nimempa housgeli anafanya dekio.
 
Pole sana Mheshimiwa Quinine. Mimi nashauri hata hii AVITAR yako uibadilishe ili isionekane ime kaa ki CCM, CCM. Umesema kweli tusije tuka pata shida ya kuingia gharama za uchaguzi mara 2
 
mtuhumiwa mahui na kijana mmoja wa darasa la sita (mwanza)wanatuhumiwa kwa kumvisha mbwa sare ya chama,ambapo baada ya wafuasi wa ccm kumuona mbwa huyo walimkimbiza kwa takribani lisaa limoja na kufanikiwa kumkamata kisha kumvua sare hizo...me sioni tatizo kumvisha mbwa nguo za binadamu

hii mbaya!
 
ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS!!!! Hivi hawa jamaa wana mtindio wa ubongo!!!!??? wanataka wananchi wawaambieje zaidi ya haya yanayo tokea???:
 
Sasa wanawasaka wamefanya kosa gani? Kwani ni marufuku kumvalisha mbwa nguo? Mbona wengine wanadekia hizo t-shirt za ccm? Waache hizo hawa nao!
 
Mambo ya kawaida sana haya...ona wakwangu alivyopendeza

To-Pee-Or-Not-To-Pee-Funny-Dog-T-Shirt-Dog-Tshirts-pee_dog.jpg
 
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linawatafuta watu wawili akiwemo mwanafunzi wa darasa la sita wakazi wa kijiji cha Lilondo wilayani Songea kwa tuhuma za kumvalisha mbwa fulana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye picha ya mgombea urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 24, mwaka huu saa 9:00 alasiri eneo la Lilondo wilayani Songea.

Kamanda Kamuhanda aliwataja watuhumiwa hao wanatafutwa na polisi kuwa ni Ephraem Mahuwi anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 27, na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Lilondo (jina limehifadhiwa).

Alifafanua kuwa muda mfupi kabla ya tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lilondo, walimwagiwa sare za CCM zikiwemo fulana, kofia, khanga na skafu wakati msafara mkubwa wa magari yaliyokuwa yakimsindikiza mke wa mgombea urais kupitia CCM, Mama Salma Kikwete, ukipita kutokea Ruvuma kwenda mkoani Iringa.

Kamanda Kamuhanda aliongeza kuwa baada ya msafara huo kupita, mtuhumiwa Mahuwi na mwanafunzi huyo, walichukua moja ya fulana za CCM walizogawiwa ikiwa na picha ya mgombea urais kupitia chama hicho na kumvalisha mbwa.

Alisema baada ya kumvalisha mbwa huyo, watuhumiwa hao walimuacha aendelee kurandaranda sehemu mbalimbali za kijijini humo.

Kamanda Kamuhanda alisema wafuasi wa CCM walimuona mbwa huyo aliyevalishwa sare za chama chao na kuanza kumkimbiza kwa takriban saa moja na kufanikiwa kumkamata.

Alisema wafuasi hao wa CCM walibaini kuwa mbwa huyo ni mali ya Mahuwi na kwamba baada ya kusikia mbwa wake amekamatwa, yeye na mwanafunzi huyo, walikimbia na kwenda kusikojulikana
.

Hata hivyo, Kamanda Kamuhanda alisema polisi wanafanya kila liwezekano kuhakikisha kwamba watuhumiwa hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

CHANZO: NIPASHE

Kamuhanda acha wehu, ubaradhuli nk hawa wananchi wana kosa gani chini ya sheria za Tanzania???? Huna kazi za kufanya mpaka unafuatilia masuala ya mbwa??? Mlalamikaji katika hii kesi ni nani, Makamba au ni kiherere chako tuu kujipendezesha mbele ya wakubwa???

Utafunga wengi basi maana mimi t shirt za CCM wanaoshea gari na nyingine wanapigia deki nyumbani. Ukinipa kitu kama zawadi ninajua jinsi ya kutumia hutakiwi kunipangia jinsi ya kutumia umiliki unapokuja kwangu naweza kufanya kitu chochote ambacho kwangu ni bora. Sio chako wewe unayeoteo

Ndugu yako kapigwa na mgombea wa CCM Maswa mmekaa kimya wala hamsemi hilo halikuwa kosa mbwa kuvaa T shirt kosa kubwa. Ak
 
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linawatafuta watu wawili akiwemo mwanafunzi wa darasa la sita wakazi wa kijiji cha Lilondo wilayani Songea kwa tuhuma za kumvalisha mbwa fulana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye picha ya mgombea urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 24, mwaka huu saa 9:00 alasiri eneo la Lilondo wilayani Songea.
Kamanda Kamuhanda aliwataja watuhumiwa hao wanatafutwa na polisi kuwa ni Ephraem Mahuwi anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 27, na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Lilondo (jina limehifadhiwa).
Alifafanua kuwa muda mfupi kabla ya tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lilondo, walimwagiwa sare za CCM zikiwemo fulana, kofia, khanga na skafu wakati msafara mkubwa wa magari yaliyokuwa yakimsindikiza mke wa mgombea urais kupitia CCM, Mama Salma Kikwete, ukipita kutokea Ruvuma kwenda mkoani Iringa.
Kamanda Kamuhanda aliongeza kuwa baada ya msafara huo kupita, mtuhumiwa Mahuwi na mwanafunzi huyo, walichukua moja ya fulana za CCM walizogawiwa ikiwa na picha ya mgombea urais kupitia chama hicho na kumvalisha mbwa.
Alisema baada ya kumvalisha mbwa huyo, watuhumiwa hao walimuacha aendelee kurandaranda sehemu mbalimbali za kijijini humo.
Kamanda Kamuhanda alisema wafuasi wa CCM walimuona mbwa huyo aliyevalishwa sare za chama chao na kuanza kumkimbiza kwa takriban saa moja na kufanikiwa kumkamata.
Alisema wafuasi hao wa CCM walibaini kuwa mbwa huyo ni mali ya Mahuwi na kwamba baada ya kusikia mbwa wake amekamatwa, yeye na mwanafunzi huyo, walikimbia na kwenda kusikojulikana.
Hata hivyo, Kamanda Kamuhanda alisema polisi wanafanya kila liwezekano kuhakikisha kwamba watuhumiwa hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
 
Back
Top Bottom