Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Status
Not open for further replies.
Kudos to you Ntuzu!ukweli na usemwe na kwa kutumia mafungu ya kwenye bibilia
 
Kuna namna mbili za kunena kwa lugha.Ya kwanza ni ile inayotajwa kitabu cha matendo na ya pili ni ile anayoongea Paulo katika wakorintho.Hii ya kwanza mtu anaongea lugha za wanadamu kama mlivyokwishaeleza hapo kabla,na ya pili ni kuongea lugha za malaika.Hoja inakuwa sasa Je ni muhimu kuomba kwa lugha ya malaika ambayo hata akili yako haipati matunda?Mimi naweza kujibu swali hilo kwa swali jingine,Je mtu aliapo kwa sababu yoyote ile anapata faida gani iwapo kwa sauti ya kilio akili yake haipati matunda?Bila shaka wanaofanya mambo hayo,kila mtu anajua matunda yake,kama mtu anapata wepesi ama uzito ni juu yake afanyaye!Ni nani wewe unayemhukumu mwingine kwa kile kitu alichoona yeye mwenyewe mbele ya Mungu wake kuwa kukifanya ni sawa?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Lete ushahidi Wa maandiko tafadhali! Ili twende sawa!
 
Rafiki hebu lete hilo fungu la Wakorinto linalokufundisha hivo. Si vema kudanganyia neno la Mungu!
 
Ukweli ni juu yako wewe na unachokiamini..Kweli kwako inaweza isiwe kweli kwangu....

Sasa kama nyie mnafanya mambo yenu kama Wasabato, mambo ya Wakatoliki na Walokole yanawawashia nini..???? Kaa kimya fanya yanayowahusu....

Rafiki yng tedo unajua Mimi nakupenda sn!

Kwahiyo nisingependa sn tukaanza kubishana na Wewe na pia Wewe mwenzangu hua huchelewi kuanza kutoa lugha mbaya! Ebu tuyamalize kwanza haya ya walokole then hayo yako tutayaangalia badae!
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa mwitiko wako..
Jumapili nilikua kanisani pale SDA kijenge Arusha kwenye Harusi ya rafiki yangu lakini sikua najua kama wasabato huwa hawavai pete..nisaidie kwanini ndugu swali hili linanoumiza akili kila nnaemuuliza anachekacheka tu na kuniambia karibu kanisani utajua...

Samahani ameline, japo umekuwa specific kwa ntuzu but naomba niingilie kati kama hautojali kwa kuuliza swali kwako. Kwani pete inamaana gani wewe unavoelewa?
 
Ukweli ni juu yako wewe na unachokiamini..Kweli kwako inaweza isiwe kweli kwangu....

Sasa kama nyie mnafanya mambo yenu kama Wasabato, mambo ya Wakatoliki na Walokole yanawawashia nini..???? Kaa kimya fanya yanayowahusu....

Tedo
Naona sasa umeshaelewa kwann huwa mnakasirika mtu akiwaambia tu iliyo kweli ya biblia ndo mnaanza kusema ooooooh!!kila mtu afanye yaliyo yake na afate imani yake na je yule anayeamini miti au mawe yampaswa afundishwe kweli iliyopo ya biblia ili asipotee kwa kile anachoamini na jambo la msingi hapa si tutaendelea kuwaambia ukweli uliopo wa neno la mungu
Balikiwa tido nina imani utafuata imani iliyo bora na sio bora imani.....
 
Mkuu nimeiona hii, duh! halafu eti akitoka hapo mwanamke ambaye hajazaa miaka 10 anapata mtoto........ mmmmmmh!!!! watazaa nyoka shauri zao!!!!!!!!!!!!

Kwa nini nyoka?

Biblia anasemaje kuhusu hiki kiumbe?
 
Biblia inasema.ktk wagalatia 5;16 mkiongozwa na roho humko chini ya sheria..........hawa wa7to hawaongozwi na Roho na ni lazima wamkatae Roho mtakatifu kwani wao wanaangalia sheria tu.Naungana na Padri kuwa hawa siyo wakristo.Ni waganga wa kienyeji tu.
 
Ahsante kwa mwitiko wako..
Jumapili nilikua kanisani pale SDA kijenge Arusha kwenye Harusi ya rafiki yangu lakini sikua najua kama wasabato huwa hawavai pete..nisaidie kwanini ndugu swali hili linanoumiza akili kila nnaemuuliza anachekacheka tu na kuniambia karibu kanisani utajua...

Pete asili yake ilikuwa ishara kwa mtu aliyebakwa kabla ya ndoa ama mwanaume aliyeingiliwa kinyume.Ni kama leo unavyoona wanaume wanavaa Hereni tunashangaa lakini usishangae vizazi vijavyo wakawa wanavalishwa kanisani kama ishara ya ndoa.Haya mambo tunayaiga tu ulaya bila kujua asili yake nini!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Rafiki hebu lete hilo fungu la Wakorinto linalokufundisha hivo. Si vema kudanganyia neno la Mungu!

Ata Mimi namsubiri alete Hilo fungu!

Lkn kuna wenzake wametumia hili fungu la Acts 2:13 kutushambulia sisi km wale walivyowashambulia wale 12 kwa kusema wamekunywa mvinyo wakalewa!

Kwahiyo na sisi wasabato tumelinganishwa na wale!

Lkn swali ni kwamba nani alie Ktk upotevu sisi au wao? Maana wao wanabadili maandiko Ktk Maana Yao waitakayo km vile Petro Wa Pili 3:16 inavyosema!

As also in all his epistles, speaking in them of these things, in which are somethings hard to understand, which those who are untaught and unstable twist to their own destruction, as they do also to the rest of the scriptures.
 
Rafiki hebu lete hilo fungu la Wakorinto linalokufundisha hivo. Si vema kudanganyia neno la Mungu!

Niko kazini sina Biblia hapa karibu ila kama wewe ni msomaji wa Biblia jaribu kuangalia 1 corinth

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
sizani kwamba hapa atapatikana mshindi ni bora kila mtu akaheshimu imani ya mwenzake

Ni kwa sababu Mungu na Shetani hawajapatana na hawatopatana kamwe maana mmoja ni mjuaji sana(shetani). Kwa hiyo hata mafundisho ya Mungu ni lazima yapate upinzani kutoka kwa shetani, na si wote huyaelewa siku moja, lakini ni kwa siku tofauti. Kwa hiyo hakuna binadamu anayesimamia andiko ama.la Mungu ama la shetani akiwa peke yake bila usaidizi wa anayemtumikia. Na wanaoelewa ni wale Waliojaaliwa kuzijua siri za Mungu.
 
Dada rosemarie maandiko yanaseema hivi Mwapotea njia kwa kutokujua maandiko na uwezo wa Mungu. Hebu nikuulize hivi, unaijua historia ya unenaji wa lugha unayoiita kujazwa na roho mtakatifu ilianza lini, wapi na kwa nini mnaponena kwa lugha mnanena maneno yasiyoeleka kwa wengine?. Hebu tuanzie hapo kwanza maana naona Mungu anataka kukuonyesha jambo la maana sana katika kumfuata kwako.

Unaweza kunipa andiko hilo linatoka kitabu gani?
 
Last edited by a moderator:
vipofu mnaongozana!

Na wewe unayeona hauna cha maana. Yesu akajibu akasema Kwa sababu ninyi mwajidai mnaona, hivyo dhambi yenu inakaa. Angalia Yohana 9 mstari wa mwisho. Sisi hapa tunaelekezana katika neno la Mungu maana hakuna aliyezaliwa akiwa anaijua bible, kwa hiyo kila aliye na kiu ua neno ataelewa kupitia njia mbalimbali ikiwepo na hii.
 
Wapendwa,

nimeshangaa sana kusikiliza radio yenu inayoitwa Morning star na kukumbana na kashfa za ajabu juu ya makanisa mengine nashangaa mhuburi anasema eti makanisa mengine wakiomba wanakuwa kama wameingiwa wazimu,haitoshi akaendelea makanisa mengine yanayoitwa ya walokole wakihubiri wanaongea kama wamelewa au wameingiwa wazimu.

Nyie wasabato nyie hamjui biblia wala utendaji kazi wa Roho mtakatifu.

Ngojeni niwaambie nyie wasabato mnaojifariji mnamjua Mungu kuliko makanisa mengine.

Mimi nimeokoka na nimejazwa Roho mtakatifu,nikianza kuomba najikuta nimezama kwenye upako wa Roho mtakatifu,manake ni kwamba Roho mtakatifu sasa anaishi ndani yangu na ananiongoza kwa mambo yote ninayofanya hapa duniani.

Hao mnaofikiri wameingiwa wazimu ni kwamba wamejazwa Roho mtakatifu,kumbuka Yesu alipopaa mbinguni aliwaahidi wanafunzi wake wabaki Jerusalemu mpaka wajazwe Roho mtakatifu.

Mnakumbuka walivyojazwa Roho mtakatifu watu waliwadhihaki wakisema wamelewa kumbe ulikuwa UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.

Nawashangaa sana enyi wasabato badala ya kupambana na shetani mnahangaika na makanisa Yenye imani kama yenu,huu ni uwezo mdogo wa kuelewa maandiko matakatifu.

Enyi wasabato vita yetu siyo ya damu na nyama bali ni katika ulimwengu wa ROHO.

Kaeni kama mlivyo na tutawaombea ili Mungu awatoe hayo yaliyo kwenye moyo wenu.

Kukamuliwa jipu linauma lakini ndio kupona kwenyewe.

Ukweli naona walokole kuna sehemu mnatakiwa kujihoji. Hasa katika eneo la "kunena kwa lugha". Nadhani mnachofanya sio kilichofanywa na mitume ambao waliposhukiwa na roho mtakatifu walizungumza lugha mbazo walikuwa hawazijui awali. Yaani mfano mswahili azungumze kichina ambacho hakuwahi kujifunza na wachina wamuelewe.

Lakini kuna jirani yangu yeye analia saa nzima wiii! Wiii!... mwingine ansema .. paratini, paratini, paratini....

Kisha anaondoka amefurahi kwamba ameshukiwa na roho! 1 Yohana 4:1 inatoa onyo hili. Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabi.

Kwa mchanganuo zaidi wa chanzo cha kile wanachoita kunena kwa lugha walokole tazama hapa.

Watch "225 - Strange Fire / Total Onslaught - Walter Vei…" on YouTube - 225 - Strange Fire / Total Onslaught - Walter Vei…: http://youtu.be/v34dTWJbBu4

Roho mtakatifu sio random feelings. Roho Mtakatifu amekusudiwa kwaajilu ya..

Yoha 16:18 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.-

Imeandikwa. . It is written
 
Unaweza kunipa andiko hilo linatoka kitabu gani?

Hili hapa katika lugha ya mkoloni, ukiona vipi waweza kulipata kwa kiswahili katika Mathayo 22:29 linasema hivi Matthew 22:29 Jesus answered and said to them, Ye do err, not knowing the scriptures, nor the power of God.
 
Biblia inasema.ktk wagalatia 5;16 mkiongozwa na roho humko chini ya sheria..........hawa wa7to hawaongozwi na Roho na ni lazima wamkatae Roho mtakatifu kwani wao wanaangalia sheria tu.Naungana na Padri kuwa hawa siyo wakristo.Ni waganga wa kienyeji tu.

Mkuu Hiyo Galatians yako inasema km hii? Mbona Naona umeleta kitu tofauti kabisa?

Ebu soma hii;

Galatians 5:16

I say then: walk in the Spirit, and you shall not fulfill the lust of the flesh.

Hapo sheria Mbona haizungumziwi? Au ndio unafanya kupindisha andiko Ktk upotevu wako mwenyewe?

Jamani Mbona mnapotea hivi?! Au ndio ile utasoma Na hautoelewa? Au utasikia na hauto tii?

Duh kz kweli kweli!
 
Wasabato si ndo wale wanaotaka kwenda marejani kuhubiri bila visa,pasport tena bila nauli.?

Kanisa la kweli ni katoliki tu,mengine makelele tu.

Pole! Soma andiko hili: Luka 4:16."Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya Sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome".....
Mwanzo 2:2,3 "Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya;akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya"

Katika hili moja uko kinyume cha Mungu, pia angalia jinsi Yesu alivyobatizwa na Yohana katika mto kwa maji mengi na ubatizo mnaoufanya..! Usifanye kinyume na unayemwabudu!!!! Tuonane kanisani Sabato ijayo!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom