Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Status
Not open for further replies.
Wapendwa,

Mnakumbuka walivyojazwa Roho mtakatifu watu waliwadhihaki wakisema wamelewa kumbe ulikuwa UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.
Ni kweli walikuwa hawajalewa, ila walinena kwa lugha zilizofahamika kwa wasikilizaji hadi wakashangaa wakisema Hawa si wayahudi, mbona wananena lugha zetu. Kumbe walinena kwa Lugha ambazo kwao walikuwa hawajawahi kujifunza hapo kabla lakini zilizoeleka kwa wasikilizaji na sio makelele ambayo hapa mnenaji mwenyewe hajui maana zake.
 
Wapendwa,

nimeshangaa sana kusikiliza radio yenu inayoitwa Morning star na kukumbana na kashfa za ajabu juu ya makanisa mengine nashangaa mhuburi anasema eti makanisa mengine wakiomba wanakuwa kama wameingiwa wazimu,haitoshi akaendelea makanisa mengine yanayoitwa ya walokole wakihubiri wanaongea kama wamelewa au wameingiwa wazimu.

Nyie wasabato nyie hamjui biblia wala utendaji kazi wa Roho mtakatifu.

Ngojeni niwaambie nyie wasabato mnaojifariji mnamjua Mungu kuliko makanisa mengine.

Mimi nimeokoka na nimejazwa Roho mtakatifu,nikianza kuomba najikuta nimezama kwenye upako wa Roho mtakatifu,manake ni kwamba Roho mtakatifu sasa anaishi ndani yangu na ananiongoza kwa mambo yote ninayofanya hapa duniani.

Hao mnaofikiri wameingiwa wazimu ni kwamba wamejazwa Roho mtakatifu,kumbuka Yesu alipopaa mbinguni aliwaahidi wanafunzi wake wabaki Jerusalemu mpaka wajazwe Roho mtakatifu.

Mnakumbuka walivyojazwa Roho mtakatifu watu waliwadhihaki wakisema wamelewa kumbe ulikuwa UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.

Nawashangaa sana enyi wasabato badala ya kupambana na shetani mnahangaika na makanisa Yenye imani kama yenu,huu ni uwezo mdogo wa kuelewa maandiko matakatifu.

Enyi wasabato vita yetu siyo ya damu na nyama bali ni katika ulimwengu wa ROHO.

Kaeni kama mlivyo na tutawaombea ili Mungu awatoe hayo yaliyo kwenye moyo wenu.

Mkuu Rose Marie tusipende na so vizuri kumsingizia Roho mtakatifu mambo ambayo si sahihi

Ebu tizama hili andiko

Matthew 6:5

And when you pray, you shall not be like the hypocrites. For they love to pray standing in synagogues and on the corners of the streets , that they may be seen by men. Assuredly, I say to you they have their reward.

Ukiendelea kusoma Mstari 6 mpk 8 nane utaona jinsi maombi yanavyo paswa kufanywa! Na si km nyie wenzetu mnavyo fanya!

Kwahiyo Ktk Hilo Mkuu jaribu kuangalia maandiko Vzr!

Na nakuja na sehemu yako ya Pili ya Matendo ya mitume!
 
Last edited by a moderator:
1 Corinthians 14:12-13 Even so ye, forasmuch as ye are zealous of spiritual <FI>gifts<Fi>, seek that ye may excel to the edifying of the church. Wherefore, let him that speaketh in an <FI>unknown<Fi> language, pray that he may interpret.
 
Dada rosemarie maandiko yanaseema hivi Mwapotea njia kwa kutokujua maandiko na uwezo wa Mungu. Hebu nikuulize hivi, unaijua historia ya unenaji wa lugha unayoiita kujazwa na roho mtakatifu ilianza lini, wapi na kwa nini mnaponena kwa lugha mnanena maneno yasiyoeleka kwa wengine?. Hebu tuanzie hapo kwanza maana naona Mungu anataka kukuonyesha jambo la maana sana katika kumfuata kwako.

Rosemarie ni mwanamme na sio mwanamke ila anapenda tu umama.
 
Last edited by a moderator:
Rose marie utaelewa tu nakusihi jaribu kuisikiliza hiyo redio bila jaziba yoyote ndo utaelewa an then morning star TV ipo karibu kuzinduliwa na endelea kufuatilia kitakachojili
Barikiwa..
 
Mimi niliwahi sema, wasabato wanawachukia wakatoliki kuliko hata shetani mwenyewe. Kumbe wanawachukia na walokole pia.
 
hao mitume ulowataja walinena kwa lugha na kila taifa walisikia na kuelewa kwa lugha yao,sasa hii ya leo sijui kama wasikio wanaelewa..,huyo ni roho mtakafujo sio yule aliyeahiwa kutumwa kwetu na YESU KRISTU.
mi si msabato
 
Hivi wasabato ni wakristu?
kuna mahali flani nilishawahi kusikia kuwa wasabato si wakistro na hawaujui u-kistru...
 
Jamani wapendwa wote mnaosoma Uzi huu!

Ebu tuangalie kitabu cha Acts 2:1-13 Maana hapo Roho mtakatifu ndipo alipowashukia wale 12 na kuwafanya waongee lugha ambazo si zao za asili tena bible iko wazi kabisa kwamba waliweza kuongea Kilibya, Kimisri, Kiarabu na lugha zingine nyingi tu! Kitu ambacho Walokole mnalichukua hili Andiko vibaya Na Ktk dua zeno mnapiga makelele tu ya malugha ambayo hayajulikani! Na wakati kunena kwa Lugha Ktk Hiyo acts 2:1-13 ni mtu kuongea kwa lugha ingine ili habari njema isikike!

Ni sawa na Mimi ngosha kuhubiri kwa English ambayo sio lugha Yangu ya asili!

Kwa Hilo ndugu zangu Walokole mmepotea! Na mnamsingizia Roho mtakatifu Ktk uovu! Kumbuka dhambi ya kumkufuru Roho ni dhambi--------
 
Mimi niliwahi sema, wasabato wanawachukia wakatoliki kuliko hata shetani mwenyewe. Kumbe wanawachukia na walokole pia.

Dada yng Kaunga mtu Wa mboka mwenzangu! Hatuna chuki na Imani yoyote! Bali kutokana na sisi kusimamia kweli basi tunaonekana Kua ni kero kwa wengine!
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa,

nimeshangaa sana kusikiliza radio yenu inayoitwa Morning star na kukumbana na kashfa za ajabu juu ya makanisa mengine nashangaa mhuburi anasema eti makanisa mengine wakiomba wanakuwa kama wameingiwa wazimu,haitoshi akaendelea makanisa mengine yanayoitwa ya walokole wakihubiri wanaongea kama wamelewa au wameingiwa wazimu.

Nyie wasabato nyie hamjui biblia wala utendaji kazi wa Roho mtakatifu.

Ngojeni niwaambie nyie wasabato mnaojifariji mnamjua Mungu kuliko makanisa mengine.

Mimi nimeokoka na nimejazwa Roho mtakatifu,nikianza kuomba najikuta nimezama kwenye upako wa Roho mtakatifu,manake ni kwamba Roho mtakatifu sasa anaishi ndani yangu na ananiongoza kwa mambo yote ninayofanya hapa duniani.

Hao mnaofikiri wameingiwa wazimu ni kwamba wamejazwa Roho mtakatifu,kumbuka Yesu alipopaa mbinguni aliwaahidi wanafunzi wake wabaki Jerusalemu mpaka wajazwe Roho mtakatifu.

Mnakumbuka walivyojazwa Roho mtakatifu watu waliwadhihaki wakisema wamelewa kumbe ulikuwa UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.

Nawashangaa sana enyi wasabato badala ya kupambana na shetani mnahangaika na makanisa Yenye imani kama yenu,huu ni uwezo mdogo wa kuelewa maandiko matakatifu.

Enyi wasabato vita yetu siyo ya damu na nyama bali ni katika ulimwengu wa ROHO.

Kaeni kama mlivyo na tutawaombea ili Mungu awatoe hayo yaliyo kwenye moyo wenu.
dada usishangae, hata siku ile ya pentecost pale yerusalemu wanafunzi wa Yesu waliposhukiwa na Roho Mtakatifu wakawa na ndimi kama ndimi za moto ukiwakalia juu ya kila mmoja, wanayerusalemu walisema "watu hawa wamelewa mvinyo asubuhi hiii", walikuwa wanashangaa kama wanavyoshangaa wasabato.

kumbuka yafuatayo, imeandikwa kwamba, "lakini awaye yote asiye na huyo Roho wa Kristo, huyo si wake" ikiwa na maana kwamba hata ukiwa mkristo kama hauna Roho Mtakatifu moyoni mwako wewe si wa kristo.

Yesu atakapokuja kunyakua kanisa lake akiwa mawinguni ni wale tu wenye Roho Mtakatifu ndio watakaonyakuliwa. Roho Mtakatifu ni Mungu mwenyewe kama hauna huyo Roho moyoni mwako ni kwamba Mungu hayupo moyoni mwako. kuwa mkristo ni challenge kubwa sana ambayo mtu inabidi ajikane mwenyewe na atoe garama ya kuyakataa mambo mengi ya dunia ili ayapate ya rohoni kwasababu kuwa wakristo wengi sana ambao hawana Mungu katika maisha yao.

ukiwa na Roho Mtakatifu, atakusaidia kuomba, unajua hautakiwi kuomba kwa akili tu muda wote, kuna wakati maombi ya akili hayafiki mbinguni kwasababu kuna wakuu wa giza na wakuu wa anga huwa wanazuia maombi wakati mwingine kama maombi hayo hayana moto. kasome kitabu cha Daniel utagundua daniel alipokua akiomba siku 21 malaika alishuka kuja kumletea majibu akasema alishajibiwa sasa alicheleweshwa na mkuu wa anga la uajemi hadi alipopata msaada wa malaika mwingine kumshambulia huyo malaika wa giza/mkuu wa anga la uajemi.

maombi ambayo hayana moto wa Roho Mtakatifu yana asilimia ndogo sana kufika kwa Mungu. ila maombi yenye upako wa Roho ndiyo yana asilimia mia kuwa yamefika kwa Mungu na hakuna pepo wa kukaa angani kuyazuia. kumbuka kuwa, Roho mtakatifu hutuombea kwa Baba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, pale anapolia aba, hivyo kama hauna Roho hauna mwombezi. maombi ya Roho Mtakatifu/ukijawa Roho na kunena kwa lugha ndio maombi pekee ambayo Roho Mtakatifu anakuombea kwa mapenzi ya Mungu kwani tukiomba kwa akili tutaomba kwa upumbavu wa kidunia tu kuomba magari kuomba vyakula kuomba vitu ambavyo si vya faida, ila Roho akiomba anaomba vyooote kwa pamoja na hata mambo ambayo Mungu ameyaona yako mbele yako na atakuombea kukuokoa au kukubariki n.k. na Neno la Mungu limeandikwa kwamba '' na ishara hizi zitaambatana na wote watakaoamini, kwa Jina langu watatoa pepo, ....watasema kwa lugha mpya....", that means, ukiamini unatakiwa kusema kwa lugha mpya, na huo ndio ukristo. HAUTAJUA MAMBO HAYA KAMA HAYAJAKUPATA, ILA WALE WENYE NEEMA AMBAO WALISHAYAPATA WANAJUA KUWA ROHO HUA ANAWAFUNULIA HAYA MAMBO HALAFU UNAKUWA HUNA HATA MASWALI YA KUJIULIZA MAJIBU YOTE UNAYAPATA KWA SAUTI YA UKIMYA ROHONI MWAKO AU KWA NJIA MBALIMBALI AMBAZO MUNGU HUONGEA NA WANADAMU. Mungu akubariki sana ndugu.
 
Mkuu rosemarie una hoja ingine? Maana Naona Ktk hili hauna la kujitetea?

Roho mtakatifu ana kz nyingi ikiwemo kutuongoza Ktk kweli yote na ukumbuke Yesu anasema neno lake ndio kweli!

Kwahiyo km na Wewe ulikua unapiga mikelele hovyo ukidai Kua unanena kwa lugha au unaongea lugha ya kimbingu na Mungu! Huenda ulikua hujui kweli! Lkn Leo umepata kweli! Nikuombe tu Mkuu acha kufanya hivyo ni machukizo mbele za Mungu!
 
Last edited by a moderator:
dada usishangae, hata siku ile ya pentecost pale yerusalemu wanafunzi wa Yesu waliposhukiwa na Roho Mtakatifu wakawa na ndimi kama ndimi za moto ukiwakalia juu ya kila mmoja, wanayerusalemu walisema "watu hawa wamelewa mvinyo asubuhi hiii", walikuwa wanashangaa kama wanavyoshangaa wasabato.

kumbuka yafuatayo, imeandikwa kwamba, "lakini awaye yote asiye na huyo Roho wa Kristo, huyo si wake" ikiwa na maana kwamba hata ukiwa mkristo kama hauna Roho Mtakatifu moyoni mwako wewe si wa kristo.

Yesu atakapokuja kunyakua kanisa lake akiwa mawinguni ni wale tu wenye Roho Mtakatifu ndio watakaonyakuliwa. Roho Mtakatifu ni Mungu mwenyewe kama hauna huyo Roho moyoni mwako ni kwamba Mungu hayupo moyoni mwako. kuwa mkristo ni challenge kubwa sana ambayo mtu inabidi ajikane mwenyewe na atoe garama ya kuyakataa mambo mengi ya dunia ili ayapate ya rohoni kwasababu kuwa wakristo wengi sana ambao hawana Mungu katika maisha yao.

ukiwa na Roho Mtakatifu, atakusaidia kuomba, unajua hautakiwi kuomba kwa akili tu muda wote, kuna wakati maombi ya akili hayafiki mbinguni kwasababu kuna wakuu wa giza na wakuu wa anga huwa wanazuia maombi wakati mwingine kama maombi hayo hayana moto. kasome kitabu cha Daniel utagundua daniel alipokua akiomba siku 21 malaika alishuka kuja kumletea majibu akasema alishajibiwa sasa alicheleweshwa na mkuu wa anga la uajemi hadi alipopata msaada wa malaika mwingine kumshambulia huyo malaika wa giza/mkuu wa anga la uajemi.

maombi ambayo hayana moto wa Roho Mtakatifu yana asilimia ndogo sana kufika kwa Mungu. ila maombi yenye upako wa Roho ndiyo yana asilimia mia kuwa yamefika kwa Mungu na hakuna pepo wa kukaa angani kuyazuia. kumbuka kuwa, Roho mtakatifu hutuombea kwa Baba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, pale anapolia aba, hivyo kama hauna Roho hauna mwombezi. maombi ya Roho Mtakatifu/ukijawa Roho na kunena kwa lugha ndio maombi pekee ambayo Roho Mtakatifu anakuombea kwa mapenzi ya Mungu kwani tukiomba kwa akili tutaomba kwa upumbavu wa kidunia tu kuomba magari kuomba vyakula kuomba vitu ambavyo si vya faida, ila Roho akiomba anaomba vyooote kwa pamoja na hata mambo ambayo Mungu ameyaona yako mbele yako na atakuombea kukuokoa au kukubariki n.k. na Neno la Mungu limeandikwa kwamba '' na ishara hizi zitaambatana na wote watakaoamini, kwa Jina langu watatoa pepo, ....watasema kwa lugha mpya....", that means, ukiamini unatakiwa kusema kwa lugha mpya, na huo ndio ukristo. HAUTAJUA MAMBO HAYA KAMA HAYAJAKUPATA, ILA WALE WENYE NEEMA AMBAO WALISHAYAPATA WANAJUA KUWA ROHO HUA ANAWAFUNULIA HAYA MAMBO HALAFU UNAKUWA HUNA HATA MASWALI YA KUJIULIZA MAJIBU YOTE UNAYAPATA KWA SAUTI YA UKIMYA ROHONI MWAKO AU KWA NJIA MBALIMBALI AMBAZO MUNGU HUONGEA NA WANADAMU. Mungu akubariki sana ndugu.

Mkuu Naona umeandika mambo mengi sn bila ata andiko la kuweka nguvu hoja zako!

Hiyo acts 2:1-13 ndiko Roho mtakatifu alipowashukia wale wanafunzi 12 na wakazungumza lugha ambazo si zao kwa asili! Ktk ule Mstari Wa 7-11. Hiyo kunena kwa ligha kwa kupiga makelele na kuongea vitu visivyojulikana mmeitoa wapi?

Umetoa mfano Wa Daniel! Daniel alikua akifanya maombi Vzr sn km Yesu alivyotuelekeza Ktk Matth 6. Lkn nyie makanisani Mweny imekua zogo kubwa pindi muombapo! Je Daniel ndio alivyofanya?

Maandiko yanasema You shall test the spirit, sio kila kitu mseme Roho mtakatifu huenda zikawa Roho chafu!
 
Naomba mjadala huu ungekuwa jukwaa la dini ingependeza sana..

Jukwaa la dini sisi wengine hatuna access huko na tungependa kuona michango ya watu katika hili

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom