Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
- Thread starter
- #61
Ukitaka kujua kuwa hizo "Nchi Washirika" zina HADHI SAWA na Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania soma Ibara ya 8 (4) inayosema kama ifuatavyo:
"Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo cha dola, Ofisa wa Serikali au chombo binafsi ni sharti afuate na kuendana na masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti ya Katiba hii utakuwa batili."
Hapa zinapozungumziwa Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote maana yake ni Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote wa Jamhuri ya Muungano (ie katika mambo ya Muungano) na sio Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote wa "Nchi Washirika." Zaidi ya hapo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijatajwa kuwa ni KUU kupita Katiba za Nchi Washirika! Sasa unawezaje kuwa na MAFAHALI WATATU (3) katika zizi moja? Kwa wapenda Muungano watakubaliana na mimi kwa hili!
Hapa ndio lilipo BOMU la kuulipua Muungano wetu, amini usiamini! Kama Muungano utavunjika (endapo Rasimu hii itakuwa Katiba) basi ni kupitia Ibara hii ya 8 na nyingine nilizotaja hapo juu!